Sio kosa langu #7

Sio kosa langu #7

samnas

Member
Joined
Oct 11, 2015
Posts
35
Reaction score
1
Chidy aliamini baba yake anaemlea ni babayake mzazi, pia mama yake kadhalika, japo mzee muro alikua na wake watatu, aliweza kuwamudu wote na kuwakidhi mahitaji yao. Hakutaka kuifichua siri nzito iliyopo baina yake yeye, mkewe na chidy ambae kwa kipindi kirefu amekua akimdanganya kua yeye ni baba yake wa kumzaa. Aliliamini hilo chidy ila kilichomkwaza na kumtia mawazo ni jinsi anavyolelewa tofauti na ndugu zake wengine katika familia hio.
Mzee muro ni mtu mwenye pesa nyingi na ni mbunge wa kanda ya kaskazini mwa tanzania, alikulia tabora na kujiingiza katika maswala ya siasa miaka ya 90. Aliamini ipo siku atafanikiwa lengo lake la kuwa katika nafasi ya juu sana serikalini, alifanikiwa kupata watoto saba, mke wake wa kwanza ambaye ni KARIMA alijifungua watoto watatu wa kiume, mmoja ndie chidi aliyezaliwa nje ya ndoa, na hakulitaka hilo chidi alijue, watoto pekee wa ndani ya ndoa ni ISSA na DULLA waliolelewa kwa mapenzi ya dhati na kupewa mahitaji yote. Mke wapili wa mzee huyo ni Fatma aliyejifungua watoto wawili mapacha, wakike na kiume, ambao kiumri walikua wadogo sana, walikua na miaka minne, halikadhalika mke wa tatu ni Siti, naye alibahatika kupata mtoto mmoja aliekua bado mchanga.

Maisha yalimuelemea chidy hasa pale alipowaona ndugu zake wakiishi maisha ya raha na kupewa chochote wanachotaka, na kujikuta ni mtu wa majonzi tangu udogoni mwake mpaka sasa kamaliza kidato cha kwanza. Kaka zake upande wa mama yake mzazi walimsema sana chidy kila alipotaka kujumuika nao na kufurahia maisha,, japo ISSA na DULLA walikataa kusoma, kitu ambacho kilimpa moyo mzee muro kuendelea kumlipia Chidy masomo japo ni mtoto wake wa nje ya ndoa.
Mzee muro ni mpenda siasa sana, ni mtu mpenda maendeleo, na siasa yake safi ilimfanya apendwe sana na watu, na walishamtabiria kipindi kirefu sana kua atakuja kua raisi miaka ya baadae. Heshima ilimfanya atambulike kusi na kaskazi, na hata familia yake pia iliheshimika, baada ya kumuoa karima na kumzalia ISSA na DULLA alifunga safari na kuelekea Japan kikazi, alikaa huko kwa muda mrefu bila kurudi.
Karima akiwa katika hali ya majonzi ya kutomuona mumewe alitembelewa na aliyekua mpenzi wake wa zamani ''IDRISSA''' kwa kweli walipendana sanaaa kabla ya kuolewa na bwana muro, hakueza kuoana na idrisa kwa hali ngumu ya maisha aliyokua nayo idrissa, na pia familia ya karima haikua tayari kumuozesha binti yao kwa mtu fukara. Idrissa ni yatima aliefiwa na mama yake kipindi anajifungua, hakupata bahati ya kuona sura za wazazi wake, baba yake pia aliiaga dunia kabla ya mama yake kujifungua. Alilelewa na kituo cha kulelea mayatima mpaka alipojielewa na kuanza kutafuta maisha,,. Alifanikiwa kupata kazi ya kuuza petroli kwa miaka mingi,. Siku alipochukuliwa na kampuni ya Gapco na kumpeleka kaskazini mwa tanzania ndio siku alipoacha kuonana na kipenzi chake.
Baada ya miaka 15 idrissa alirudi Dar es salaam kwa lengo la kuwaomba wazazi wa karima wamuezeshe mtoto wao kwani sasa anajiweza kimali, si idrissa yule wa zamani, alishajenga nyumba pamoja na kupata gari ya matembezi. Aliamini kwamba yeye pekee ndie angeliweza kumuoa karima, hakuamini aliposikia karima alishaolewa na ana watoto wawili, kitendo hiki kilimuumiza sana moyo idrissa. Idrissa alidhamiria kufunga safari mpaka alipo karima huko Temeke ili moyo wake uridhike, alifahamishwa sehemu hiyo na rafiki yake kipenzi '' Denge'', hakusita kwenda mpka alipo karima.

''Idriss??....siamini macho yangu kama ni wewe!!!.'' Karima aliuliza kwa mshangao mkubwa huku akilengwa na machozi na kutoamini alichokiona mbele yake.
Kuolewa kwake na muro na kujifungua watoto wawili hakukumpa shida yeye, bado alimthamini na kua na chembe za mapenzi kwa idriss,, isingekua familia kumkatalia kuishi na idrissa basi mda mrefu angelikua kashaolewa na idrissa.
''Umenisaliti karima!! , au kisa ya umasikini na ufakiri wangu ukaniona sifai karima?''
''Hapana idriss usiseme hivyo..karibu kwanza ndani tuyaongee...'' ( alimkaribisha idriss huku akijifuta chozi kwa khanga aliyojifunika nayo)
'' enhee...nambie kwanza nini kilikusibu mpaka ukanikimbia miaka yote hio?'' Karima alimuuliza idrissa baada ya kuketi kwenye sofa kubwa lililopambwa kwa rangi ya kahawia , yalionekana ni ya gharama sana, mbele yake kulikua na luninga bapa yenye upana sawa na meza ya sebuleni hapo, mandhari ya nyumba hio yalimvutia sana idrissa na kutambua kua aliemuoa karima alikua ni tajiri wa kufa mtu. Hakusita kupapasa macho huku na kule mpaka alipoiona picha ya mzee muro ukutani alievalia suti.
''Ni story ndefu sana karima....yote ni katika kutafuta maisha ili niweze kuishi , kama unavotambua, sina mama wala baba, hakuna ndugu anaenisaidia,....'' Alisita kidogo na kumeza fundo la mate huku chozi likimlenga. Alimsimulia mkasa mzima yaliyomsibu maishani mwake mpaka alipopelekwa kaskazini mwa tanzania, na huko vipi alinusurika kufa kwenye ajali iliyoua watu wengi sana, ajali iliyoitikisa Tanzania, magari ya mafuta yaliporipuka na kuwaua watu wengi, yeye pia alikuwemo ila alinusurika na ajali hio..ngozi yake ilishamiri mabaka na makovu mengi mwilini mwake, ilikua ni story ya kusikitisha na kuhuzunika iliyomfanya karima abubujikwe machozi bila kujizuia. Alitamani sana kuolewa na idrissa kwa tabia yake ya upole na kumjali. Baada ya maongezi marefu wawili hao walipata chakula cha usiku na kwa jinsi walivyokua na hamu kwa kila mmoja wao kukaa na mwenzake siku hiyo, walijikuta wakilala pamoja kitanda kimoja na kufanya mapenzi.
Alisita karima kufanya kitendo hiko ila kwa alivomjaa idrissa moyoni alijikuta akilainika na kuondoa nguo moja moja kitandani. Watoto wakiwa wamelala nyumbani hapo ilikua rahisi kwao kufanya wanachotaka, miili yao iligusana, hamu ya kufanya mapenzi iliwajaa huku damu ikichemka kwa kasi. Haikua rahisi kwa idrissa kuikumbuka ile picha alioiona ukutani, umbo la karima lilimfanya apagawe na kumpa utamu mke wa mzee muro. Walipeana tunda usiku huo mpaka kulipokucha.
..

..

..
unahisi nini kitatokea baada ya mama yake chidy ( karima ) kulala na idrissa hali ya kua mumewe yupo japan? Nini atafanya mzee muro akisikia mkewe kalala na mtu mwengine? Usikose kufatilia mkasa huu wa kusisimua sehemu ya #8
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom