samnas
Member
- Oct 11, 2015
- 35
- 1
''Enhee,kuna nini tena hapa?'' Aliuliza mkuu akiwa na mikunjo kwenye paji lake la uso ikidhihirisha hamu alokua nayo mwalimu huyo kujua nini kinaendelea. Hakupenda hata kidgo wanafunzi wake waonewe. Akiwa anatupia macho walipokaa wanafunzi Moyo ulimpiga ''PAA!!'' Alipomuona mwalimu mashaka akivuja damu na yu katika hali ya kutojielewa, ni kipi kilimsibu mwalimu mashaka, na ni nani alifanya unyama huo,, maswali yasiokwisha yaligonga akilini mwake na kukosa jibu la uhakika, ili mbidi awaamuru wanafunzi watawanyike na wengine wamsaidie kumbeba mwalimu mashaka na kumpeleka ofisini kwaajili ya huduma ya kwanza.
Hashir akiwa na majonzi alijikunyata mithli ya ndege aliyeroana kwa mvua za masika, hakujua nini hatma yake hapo shuleni, na hakujua kwanini ni yeye pekee anakumbwa na matatizo kama hayo,,
'' kaka usijali, hili tutalimaliza mbona? Wala asikutie wasi wasi, huyu lazima tumtimue hapa shule, hakuna anaempenda..'' Chidy huku akimshika bega hashir aliyekua amekaa kwenye dawati darasani akiwa mbaaali kifikra alimpa moyo na kumfariji kwa yote yaliyotokea.
Haikua rahisi kuamini kua ni chidy ndie aliemjeruhi mwalimu mashaka mpaka akapoteza fahamu, wapo waliofurahia kitendo kile hasa wanafunzi na baadhi ya walimu , na wapo waliokasirishwa vile vile. Mwalimu mashaka aliwahishwa hospitali ya Amana kwa gari aina ya starlet ya mzee Daniel. Si kawaida kwa mzee Daniel mkuu wa shule hio kuendesha gari kwa mwendo wa kasi kama ilivyokua siku hio, alitumia mwendo wa dakika 35 mpaka kufika hospitali hapo, bila ya kupoteza muda aliwahiishwa na wauguzi kwenda chumba cha matibabu.
*****************
Hali ya Hashir bado ilikua mbaya,huku akichechemea kwa msaada wa Chidy akiwa pembeni yake, walitembea pamoja huku chidy akimpa msaada wa kutembea kuelekea nyumbani.
Haikua rahisi kwa Hashir pekee kuelekea kwao magomeni mikumi kwani afya na hali yake havikumruhusu,, ilikua gumzo kwa siku hiyo na chidy alionekana shujaa kupita kiasi kumjeruhi mtu aliekua akiogopwa shule nzima.
Kilomita chache kabla ya kufika kituoni Hashir na chidy walionana na rafiki yao wa kike waliokua wakisoma nae pamoja pale pale Hekima. Alisikitishwa na hali aliyokua nayo hashir pamoja na yote yaliyomsibu, alijikuta akitokwa machozi na kutojua aseme nini, alimpenda sana hashir kama rafiki yake wa kiume, tangu wasaidiane darasani na kufaulu pamoja alimthamini kuliko kitu chochote,, hashir ndie mtu pekee alieweza kumfumbua macho jasmin na kumuonesha jinsi ulimwengu ulivo, aliamini hamna kinachoshindikana chini ya jua, ushupavu wake na ujasiri ndivo vilomfanya awe na akili ya kishujaa na moyo wa uvumilivu, jasmin na umburula wake darasani tangu darasa la kwanza,, aliweza kushika nafasi ya pili baada ya kumfanya hashir kua rafiki yake kipenzi akiwa darasa la tatu.
'' pole jamani hashir,...ndo maisha hayo ipo siku yatakwisha....pole sana hashir..'' jasmin kwa sauti ya upole alimpa pole hashir huku akimsaidia kutembea kumpeleka kwao mikumi. Kweli mthamini watu huthaminiwa.
''Eeeh?? Kunani tenaa?! Mbona hivyo mjukuu wangu (bi Zai akiwa na mfazaiko wa hali ya juu alimkimbilia hashir na kusaidia kutembea) yamekusibu nini mjukuu wangu?'' Waliketi wote chini na kutupa macho yao yote kwa hashir aliekua akiugulia kwa maumivu.
''Mjukuu wangu wanitia presha jamani nambie yamekusibu nini??eti chidy, rafiki yenu kakumbwa na nini?'' Aliuliza bi zai
Chidy kwa ujasiri wote alianza kumhadithia bi zai mkasa mzima,. Bi zai hakua na la kufanya zaidi ya kuacha mdomi wazi mithli ya mamba anaewinda chakula chake,, alisononeka sana moyoni kila alipomfikiria Hashir, tangu wampate na kumlea, mateso yote aliyopata bado anateswa hivi, alimuonea huruma sana mtoto huyo.
''Oh pole sana mwanangu, ndo maisha hayo, jikaze tu mjukuu wangu, walimwengu hawana huruma, jitahidi usome kwa bidii yote yatakwisha hayaa,, sawa mjukuu wangu? Pole sanaa..''
Bi zai alimpa pole hashir aliekua mbali kifikra..
''Asante bibi, babu yuko wapi mbona leo sijamuona?''
''Babu yako tangu alipoamka leo ana kahoma kanamsumbua kweli, nahisi kidonda cha mguu kinamsumbuaa, pesa yenyewe ya kutafuta dawa hamna mjukuu wangu, kabaki tu ndani hana la kufanya''
''Eh...maskini babu yanguu,, dah atapona lakini, sijiskii vizuri ila ntaenda kumuona baadae maana saiv bibi nna maumiv acha tu''
''Usijali mjukuu wangu kapumzike...'' Bi zai aliwaacha akina chidy na mwenzake jasmin wakiendelea kumfariji, walimpeleka chumbani akajipumzishe na wao kwenda makwao.
Hali ya mzee kauchume ilizidi kudhoofika,kidonda alichokua nacho mguuni kilizidi kumsumbua, na mawazo ya watoto wake yalizidi kudhoofisha hali yake, Hashir pamoja na kua na hali mbaya ilim bidi akamuone babu yake anaendeleaje, alipigwa butwaa alipomkuta bibi yake akiwa amepiga magoti anamlilia mumewe mzee kauchume, povu lilikua linamtoka mzee hyo huku macho yakiwa yanaangalia juu kushuhudia jinsi roho yake inapokwenda, Hashir alimkimbilia babu yake huku akimuita kwa uchungu, chozi likiwa linatiririka mashavuni mwake, hakuthamini wala kufikiria kuhusu mguu wake ulioteguka baada ya kipigo cha mwalimu mashaka.
'' babuuuuuu!! Babuuuuu??! Amka babuuu!!! Usiondoke babuuuuu,, babuuuuuuu!!! Usituache pekeeeetu babuuuu,, ntapata wapi kama wewe babuuu? Sina baba wala mama wewe ndio tegemeo pekee na bi zai, leo waondoka ntabaki Na nani mie babuuuu? Babuuuuuuu!!!...'' Alilia sana hashir kias cha kupoteza fahamu na kumfanya bi zai apagawe na kushindwa kuelewa nini afanye.
..
..
..
Unahisi maisha gani atakayoishi hashir baada ya kumpoteza babu yake??
Usikose kufatilia riwaya hii ya kusisimua sehemu ya #5