samnas
Member
- Oct 11, 2015
- 35
- 1
Hali ya nyumbani hapo ilikua ni ya kusikitisha sana,kimali mzee kauchume alikua maskni sana,ni mtu wa kabila la wafipa aliezaliwa huko mkoani rukwa wilaya ya sumbawanga, hakua mzuri sana wa kuongea kifipa maana miaka mingi alihamia daressalam tangu kufriki kwa wazazi wake, alilelewa na baba yake mzazi aitwaye RAMA, alikua ni mwanasheria maarufu tanzania miaka ya 80,alipatwa na matatizo ya kupooza upande mmoja baada ya mkewe ZAKIA kupata ajali na kupoteza maisha papo hapo. Mzee Rama haikumchukua muda alipoteza maisha na kuacha mali nyingi sana, ndugu wa mzee Rama hawakumjali kauchume, walisomba mali zote na kumuacha kauchume akiwa hana mbele wala nyuma. Alichukuliwa na baba yake mdogo huko daressalaam na kulelewa mpaka alipofika miaka 23. Baba yake mdogo alimuozesha kauchume akiwa na miaka 24 na kumuacha ajitegemee kama mume na baba wa familia yake mwenyewe, huo ndio ulikua mwanzo wa mzee kauchume kujitegemea mwenyewe na mwisho kuishia masikini.
Katika maisha yake hakufanikiwa kupata mtoto aliyefikia miaka 10 akiwa hai, wote walichukuliwa na muumba katika matukio mbali mbali. Alipata watoto mapacha HASSAN na HUSSEIN, walipotimiza miaka 7 walipata maradhi ya kipindu pindu na kupoteza maisha kwa nyakati tofauti,hilo lilikua pigo kubwa sana kwa mzee kauchume,baada ya miaka miwili walifanikiwa kupata mtoto wakike waliempa jina la kipekee '' NINA'',alikua ni mtoto pekee aliepata kila aina ya mapenzi na matunzo ya hali ya juu, hawakujua nini hatma ya huyo mtoto kwani hamna anaejua nini kingetokea kesho, na nini muumba kampangia,,licha ya malezi na mapenzi yote aliyopewa NINA, bado na yeye hakua na bahati ya kuiona dunia na walimwengu walivo, akiwa mdogo mwenye umri wa miaka mitano alichkuliwa roho yake na muumba alipokua anatoka shuleni na baba yake, pindi wanavuka barabara walipata ajali wote wawili, NINA hakuweza kuendelea kuishi na baba yake alipata kilema cha maisha, kwa kupoteza mguu wake wa kulia, maisha yake yote mpaka anamuokota Hashir chini ya daraja na kumlea mithli ya mwanawe alikua akitembelea magongo.
Ilikua ni siku ya jumaatatu, alfaajir mishale ya saa 12, mionzi ya jua ikionekana kwa mbaali, majogoo wakisikika wakishindana kuwika, n'gombe nao hawakua nyuma wakilia sababu ya njaa, Hashir aliamka mapema kwenye kitanda cha kamba ndipo alipokua akijilaza. Mgongoni akiwa na alama za kamba mithli ya mtu aliyepigwa mijeledi, aliyazoea maisha hayo pamoja na umri wake kutomruhusu, lakini alijikuta akizoea taabu na shida za maisha, macho yake bado yakiwa na ukungu, kichwani bado anajihisi yupo ndotoni,alifata mswaki wake wa mti na kwenda kujisafisha kinywa pamoja na kujimwagia maji ili ajiandae na shule. Haikumchukua muda alitoka chooni na kuelekea chumbani tayari kujitayarisha kupika chai kwaajili ya wazee wake. Ilikua ni sehemu ambayo kwa mtu wa kawaida asingeweza kuamini kama wanatumia binadamu kufanya mapishi yao, ni kibanda kilichodhoofika na muda wowote kingeweza kuanguka, kiliezekwa na makuti yaliyokwisha oza na kuegeshwa na miti ambayo tayari ilishaliwa na wadudu kwa muda mrefu, mawe matatu yaliyokithiri weusi ndio lilikua jiko la familia hio, vyombo vilivyokwishachoka ndivyo walivyokua wakivitumia. Nani anayejali kuhusu familia hiyo? Na nani atakaye saidia?waliamini hakuna kitu kiitwacho serikali kwa sababu ya haki kutotendeka, kila aina ya wadudu walijenga nyumba zao ndani ya nyumba hyo ya mzee kauchume.
Saa 1 kamili Hashir tayari alimaliza pirika za nyumbani hapo, aliwaamsha wazee wake ili wapate uji mkavu uliokosa virutubisho wala vitafunio,ni hali ambayo walishaizoea, siku Mungu akileta basi hupata chochote na kuweza kuingiza kinywani, na siku Muumba asipopanga basi familia hyo hushindia njaa mpaka kupindukia kwa siku inayofata. Baada ya kupata chochote kitu Hashir alichukua mfuko wake wa madaftari na kukimbilia shuleni.
Foleni za magari na taabu za usafiri zilimfanya hashir asiweze kufika mapema shuleni hapo, kwani kutoka tandika mpaka buguruni ni kipande kirefu kidgo. Saa mbili na nusu (2:30) hashir alifika shuleni hapo, bila ya woga aliingia getini na kukuta wenzake mstarini
''Vipi wewe?? Mbona umechelewa??unafikiri shule ni ya babaako hii??? Piga magoti chini..!!''
Hashir alitetemeka kama mtu aliyesikia baridi la ajabu huku jasho likimtoka, alitii amri mara moja na kusubiri nini kingefuatia.
..
.
.nini kitamkuta kijana hashir baada ya kucherewa kufika shuleni?? Usikose kufatilia sehemu ya 3