Sio kosa langu#1

samnas

Member
Joined
Oct 11, 2015
Posts
35
Reaction score
1
Mama yangu yuko wapi?? Baba yangu yuko wapi?? Ndugu zangu kina nani? Ni maswali niliyokua nikijiuliza kila siku bila kupata majibu,maisha ya tabu na shida niliyazoea nikiwa bado mbichi sana huku nikiwa namsaidia bibi yangu Bi.zai apate chochote cha kuingiza kinywani. Tumeweza kuishi kwa muda mrefu sana bila kuambiwa chochote kuhusu koo yangu na wapi alipo mama yangu na baba yangu. Haikua rahisi kuitambua siri nzito iliyofichwa baina yangu na wazazi wangu,ila niliamini ipo siku nitaitambua siri hiyo.
Hashir aliendelea kujipa moyo kwamba ipo siku isiyojulikana jina lake ataweza kuonana na mama yake aliemzaa ili furaha yake iweze kuchipua na kuishi kwa amani na furaha.
Aliamini kwamba wazaz wake wapo hai na ipo sehemu wanaishi, hakuchoka kumuuliza bibi na babu yake mzee kauchume kuhusu wazazi wake, japo jibu alilokua akipewa ni tofauti na matarajio yake,
'' mjukuu wangu, maisha ni safari ndeefu, yenye kila aina ya vioja, wapo watembeao kwa miguu, wapo wanaotembea kwa magari, wapo wanaokandamiza na kukandamizwa, najua bado akili yako haijapevuka, ila ukikua utaelewa nisemayo,,...soma sana mjukuu wangu wazaz wako ipo siku utawaona..sawa baba?'' Aliongea mzee kauchume kwa upole na unyenyekevu wa hali ya juu, sura yake iliyoshamiri ndevu nyeupe na mikunjo ilidhihirisha uzee wake, alikua mzee mwenye busara na hekma ya hali ya juu, tangu amuokote hashir chini ya daraja amemfanya kama mtoto wake wa kumzaa na kumpa mapenzi yote mithli ya mwanawe.
Maneno yalimgusa sana hashir alijikuta akikimbilia chumbani kwake na kuangua kilio.
Alikua ni mtoto mwenye umri wa miaka 12, uso wake mpana ulijawa na alama za michirizi ya machozi mashavuni mwake, macho yake makubwa ya mviringo yalin'gara na kupendezesha paji lake la uso, Muumba alimjaalia akili nzuri iliyoambatana na tabia yake ya upole,ucheshi na huruma. Mawazo na maisha magumu pamoja na matatizo anayokumbana nayo yalimfanya adhoofike na kuonekana mithli ya mgonjwa wa pumu,,alidhoofika sana kiafya na wala halikumuumiza kichwa hilo,kilichomuumiza ni kutokuwepo kwa wazazi wake na hakujua lini atatia nuru macho yake kwa kuwaona watu aliowatamani kuwaona kwa miaka mingi sana,alietaman kupata malezi yao na mapenzi yao, ulikua ni wakati mgumu sana kwake kwa kua na kitendawili asichoweza kukitegua....
.
.
. Je hashir ataweza kuonana na wazazi wake? Unafikiri ni kipi kilichomfanya hashir asipate malezi bora ya wazi wake? Usikose kufatilia sehemu ya 2
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…