Sio kitu kizuri kumdhalilisha mzazi mwenzako hasa mkiwa mmetengana, mnatengeneza chuki kwa watoto

feyzal

JF-Expert Member
Apr 20, 2016
6,805
12,668
Habari ya kuamka wadau.

Sijapenda kuandika huu uzi ila nimeona wacha niseme tu ili wengine wenye tabia kama hii muache mara moja. Leo asubuhi kabla sijafanya shughuli zangu nikaona nipite kwa mzee nimsalimu kisha nikahangaike na mkate wa kila siku.

Nimefika kwake saa 12 na dk kadhaa asubuhi alifurahi kuniona tukaongea mengi sana, lakini huku mwishoni alinikwaza kwa jambo ambalo karibu kila siku anarirudia nimemvumilia sana ila leo nikaona nimtolee uvivu Mwenyezi Mungu atanisamehe kama nimefanya dhambi.

Tuliongea mengi sana mazuri lakini aliharibu padogo tu na kuondoa maana ya mazungumzo yote. Haya ni baadhi ya mazungumzo yaliyonikera.

Baba: Mwanangu ujitahidi uoe mapema ni vizuri zaidi akili yako itatulia, mimi nilimuoa mama yako nikiwa nina miaka 21 kipindi ambacho hata sina maisha mazuri lakini nikahangaika na mke wangu nikafanikiwa ila vijana wa sasa mna visingizio vingi, kuoa hampendi kabisa.

Mimi: Sawa mzee nitaoa nikimpata mwanamke muadilifu.

Hapo tuliongea mengi ila alianza kunivuruga hapa

Baba: unajua mimi nilimuacha mama yako kwa sababu tu ya umalaya, nilimfumania na wanaume. Aliniaga anakwenda kwa mama yake kumuona Morogoro lakini nikawa nina mashaka nae mienendo yake ndipo nikaanza kumfuatilia...kweli siku aliyoniaga akaenda kwa huyo hawara yake na nilimkuta pale kwa hawara yake. Nilimpiga sana mwishowe nikaona nitaua nikamuacha. (Hili suala alikua akiliongea karibu kila mara tukionana)

Akaendelea "Usije ukaoa mwanamke wa kabila la mama yako,ni wahuni sana ndo maana tangu nimemuacha mpaka leo hana maisha ya kueleweka yupo anatanga tanga,ameolewa na mwanaume wa ajabu hana mbele wala nyuma kwa upumbavu wake..

zamani nilitaka kumrudia lakini nimeona bado ana tabia zile zile na amewaambukiza tabia yake hata kaka zako wakubwa wamezaa hovyo hovyo kwa umalaya,Ona kaka yako mmoja amepata na ukimwi muda wote ni upuuzi tu sasa na wewe usifuate tabia ya mama yako"..mengine sipendi niyaongee hapa ni mengi na mazito

Uvumilivu ukanishinda nikamuuliza

Mimi:
Baba unajisikiaje moyoni mwako unavyoongea maneno ya namna hiyo kumuongelea vibaya mzazi mwenzako mbele ya mtoto wake, mbona una mdhalilisha mama, unanijengea picha gani pindi nikimuona? Niwe nadhani nimezaliwa na mama malaya? Kwanini usingemstiri mwenzio kwa watoto wake kutengana kwenu ikabaki stori yenu? Mbona una mvua nguo?

Wewe mangapi umemfanyia mama tena tukishuhudia na hakuna hata siku moja amewahi kukudhalilisha namna hii kwa watoto wake, mama leo ana maisha magumu kwa sababu yako mali zake za urithi umetapeli mbona hatusemi na anakuheshimu? Unamuongelea vibaya kila mahala ili iweje? Niliongea mengi kwa hasira sana (Mungu anisamehe)

Mzee alifyatuka na kusema kuwa ninamfokea kiufupi hali ya hewa ilichafuka nikaondoka kwa hasira sana. Niko kazini lakini moyo wangu umekosa amani sijawahi gombana na mzazi wangu kiasi hiki tangu nimezaliwa ila leo maji yalizidi unga.

Pengine siko sahihi kwa nilichofanya au nikawa sahihi pia...naomba wenye busara waniambie nini cha kufanya maana nahisi hata tukionana sasa hivi na mzee tutashikana mashati kwa hasira alizokua nazo na mimi sitaki tuwe na utofauti huo.

Lakini hii tabia si njema kabisa iwe kwa mzazi wa kike au wa kiume kumdhalilisha mwenzako kwa watoto hata kama kweli ana makosa kuachana kwenu kwanini isibaki siri yenu.

Sent using Jamii Forums mobile app

=====

Maoni

Pole mkuu. Ila naona kama kwenye familia yenu kuna kitu hakipo sawa. Wewe mwenyewe umeshindwa kumsitiri mama yako, maana umeirudia story ya mzee kuthibitisha kuwa bibi mkubwa aliachwa kwa umalaya. INATHIBITISHA KUWA UNA KIFUA KIDOGO KAMA MWANAUME, au vinginevyo ungeiwasilisha mada kwa namna ya kuwafichia siri wazazi wako. Mzee nae kukaa chini na wewe na mkaanza kupiga story za umalaya wa mkewe ambaye pia ni mama yako, nalo ni a bit strange. Hamna mipaka ya kuongea kati ya wazazi na watoto?
 
feyzal,
Asante kwa kuelimisha wanandoa, somo limeeleweka. Mungu atusaidie sana tuwe na uwezo wa kusitiriana.
 
Baba alikuwa na lengo la kukuelimisha tu. Tatizo ametumia njia isiyokuwa nzuri. Ni vyema umemuambia ukweli ili asije akarudia tena.

So far sijaona neno baya au kumkosea heshima kwa hayo maongezi yenu. Kama ulimuambia maneno ya kumkosea heshima ambayo haujayaandika hapa, nenda ukaombe msamaha.

Lakini pia hata kama haujamkosea heshima nenda kwa lengo la kupatana, hata ikibidi uombe msamaha kwa makosa ambayo haujatenda.

Kwa kuwa yeye ni mzazi, hata akigundua kuwa amekukosea inaweza ikawa vigumu kukuomba msamaha. Ndio hapa inakuja ile dhana ya mkubwa kutokukosea.
 
Ungemuomba naye aweke ya kwake ili tuweze kuyalinganisha. Hatuwezi kushindana kufanya zinaa ila sisi kina baba tunatia kinyaa kwenye hiyo sekta. sasa iweje mama yetu aonekane ndiyo corona wa umalaya. haiwezekani aiseee haaaa haaaaa
 
Ukienda mwambie akome kukuambia mabaya ya mama yako mbele yako, kama yapo wewe ni mtu mzima utajionea mwenyewe. Uko right kabisa. Wanasema mzazi hakosei si kweli, wanakoseaga tu.

Mzazi ni mzazi lakini mzazi asiye na hekima/mpumbavu wapo/yupo. Mfano, unakutana msichana anamwamkia mzee shikamoo Mzee anaikataa kisha ana mwambia binti ''Unaniamkia shikamoo unataka kuninyima nini?"

Hao ndio baadhi yao. Na mzazi wako anaingia kwenye kundi hilo la wazee. Kwa kukosa hekima ya kumsitiri mwenza mbele ya mtoto/watoto.
 
Mkuu iwe kweli ama uongo lakini...sio sahihi hata kidogo kuongea yao kwangu.Kwa koment hii yako nadhani baba ako akikueleza habari za chumbani za mama yako utashangilia si ndio?

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu feyzal
Umezaliwa mwanaume na utabaki kuwa mwanaume.

Katika familia yoyote baba hutumika kuwaeleza watoto wa kiume mambo ya kiume na mama huwafundisha watoto wa kike mambo ya kike. Baba ako anaweza kukusimulia kuhusu umalaya wa mamaako mpaka akamuacha ila hawezi kumsimulia hivyo mwanae wa kike. Pia mama ako anaweza kumueleza dada ako jinsi alivyoachwa na baba yenu kisa umalaya wake ili apate somo kuwa umalaya si mzuri asije akarudia makosa kama yake. Huyo mama ako hawezi kukwambia wewe kwa sababu haikufunzi zaidi ya kumdhalilisha yeye ila mwanae wa kike atamwambia.

Tuje kwa baba ako.

Lengo la mzee wako kukwambia hivyo ni zuri sana kwa sababu anakupa caution usije ukafanya makosa kuoa mke malaya kama mama ako. Unaweza kudhani katumia maneno makali ila kwa umri wako wewe kipi hufahamu mkuu... hata mbayo hujayaona umeshayasikia! Ameona wewe ni kidume tena mko wawili tu wewe na yeye ndio maana alikua huru kukueleza.

Cha msingi usimuhukumu baba kwa kauli zake ana maana kubwa sana coz amepitia mengi kuliko wewe. Cha kufanya muite faragha ongea nae kwa upole atafunguka mengi hata ambayo hukutarajia kuyasikia, na yawe somo kwako katika kuchagua mke.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pore sana, you don't need to fight. The message is sent, mind your own business. Muachage

Don't make a promise you can't fulfill...
 
Inawezekana pia maana nashangaa mama japo ana mchukia sana mzee kwa dhulma yake lakini hakuwahi kusema mbele yetu moja kwa moja.Hata akiumwa au akiwa na shida yeye amekua mstari wa mbele kutuambia tukamuone.
Baba ako bado anampenda mama ako. Kama mtoto hutakiwi kuside na mzazi yoyote yule.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
  • Thanks
Reactions: THT
Asante ndugu.
Ukweli sijamwambia maneno ya jeuri mengine zaidi ya niliyoandika labda kosa langu liwe niliongea hayo maneno nikiwa na hasira.
Baba alikuwa na lengo la kukuelimisha tu. Tatizo ametumia njia isiyokuwa nzuri. Ni vyema umemuambia ukweli ili asije akarudia tena.

So far sijaona neno baya au kumkosea heshima kwa hayo maongezi yenu. Kama ulimuambia maneno ya kumkosea heshima ambayo haujayaandika hapa, nenda ukaombe msamaha.

Lakini pia hata kama haujamkosea heshima nenda kwa lengo la kupatana, hata ikibidi uombe msamaha kwa makosa ambayo haujatenda.

Kwa kuwa yeye ni mzazi, hata akigundua kuwa amekukosea inaweza ikawa vigumu kukuomba msamaha. Ndio hapa inakuja ile dhana ya mkubwa kutokukosea.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom