Sio kila mchekeshaji anaweza kuwa MC

Sio kila mchekeshaji anaweza kuwa MC

MamaSamia2025

JF-Expert Member
Joined
Mar 29, 2012
Posts
19,395
Reaction score
40,221
Nawasalimu katika jina la Chama Cha Mapinduzi. Najua kuna mambo mengi ya kitaifa yanaendelea ambayo mngependa niandike maoni yangu ila kwa leo nawasihi tuangalie hili suala dogo ambalo linataka kuleta taharuki kwenye jamii.

Chanzo cha huu uzi ni tukio la Komredi Will Smith kumtwanga kofi MC Chris Rock kwenye sherehe za utoaji tuzo za Oscar. Sababu ya lile kofi ni utani wa MC uliogusa maradhi yanayomsumbua mke wa komredi Will Smith. Binafsi namuunga mkono Will Smith kwa kitendo cha kishujaa alichokifanya maana Sababu alikuwa nayo, nia na uwezo. Yule MC hatarudia tena upuuzi wake na itakuwa fundisho kwa ma-MC wengine ambao pia ni Comedians.

Tukirudi hapa nchini ni kwamba kumetokea wimbi la vijana wachekeshaji (comedians) kujiaminisha wao wanauweza u-MC hivyo kujitangaza kama washereheshaji pia na kuanza kupata kazi za hapa na pale. Baadhi yao kweli wamefanya vizuri kama vile MC Pilipili na wengine wachache. Sio jambo baya kwasababu ni kazi ya halali kabisa ya kujipatia kipato. Tatizo ni pale wengi wao kutoweza kufuata miiko ya kazi ushereheshaji na kujikuta wanafanya comedy sehemu isiyotakiwa hivyo kuleta usumbufu usio wa lazima kama ilivyotokea kwa mpigwa kibao Chris Rock. Hapa Tanzania kuna washereheshaji ambao pia ni comedians wamekuwa wakilalamikiwa mno kuleta mizaha sehemu isiyotakiwa mizaha.

Ushauri wangu ni kwamba hawa comedians kama wanataka u-MC wajifunze baadhi ya mambo muhimu toka kwa manguli wa hiyo fani kama vile Taji Liundi, Cheni na MC GaraB ili kutojichanganya wanapokuwa kwenye majukumu yao. U-MC ni kitu kingine kabisa kinachojitegemea ndo maana hapa nchini ni comedians wachache sana wanaoweza kuingia kwenye top list ya ma-MC wanaoaminika na kulipwa pesa nyingi. Nampongeza sana comedian Joti kwa kuweza kusimama kwenye fani yake bila kuendekeza njaa za kutaka kuwa MC tena. Comedians jitahidini kutafuta namna nyingine ya kuongeza kipato ili kuepuka makofi kama ya Will Smith.
 
Ndio tatzo la hawa wasaniii wetu kila kitu wanajua mmoja alijidai ni dokta kumbe hajui kuandika panadol!
 
Will smith alkosea sana kwenda kumzabua Kofi Cris..
will smith n legend katka comedy anaelewa comedy zinavyofanya kaz

Kama ww n mpenz wa comedy genre utajua tu kama wilsmith amekosea
 
Mpoki apate ujumbe huu, huwa analeta mizaha sehemu isiyo sahihi.
 
Nawasalimu katika jina la Chama Cha Mapinduzi. Najua kuna mambo mengi ya kitaifa yanaendelea ambayo mngependa niandike maoni yangu ila kwa leo nawasihi tuangalie hili suala dogo ambalo linataka kuleta taharuki kwenye jamii.

Chanzo cha huu uzi ni tukio la Komredi Will Smith kumtwanga kofi MC Chris Rock kwenye sherehe za utoaji tuzo za Oscar. Sababu ya lile kofi ni utani wa MC uliogusa maradhi yanayomsumbua mke wa komredi Will Smith. Binafsi namuunga mkono Will Smith kwa kitendo cha kishujaa alichokifanya maana Sababu alikuwa nayo, nia na uwezo. Yule MC hatarudia tena upuuzi wake na itakuwa fundisho kwa ma-MC wengine ambao pia ni Comedians.

Tukirudi hapa nchini ni kwamba kumetokea wimbi la vijana wachekeshaji (comedians) kujiaminisha wao wanauweza u-MC hivyo kujitangaza kama washereheshaji pia na kuanza kupata kazi za hapa na pale. Baadhi yao kweli wamefanya vizuri kama vile MC Pilipili na wengine wachache. Sio jambo baya kwasababu ni kazi ya halali kabisa ya kujipatia kipato. Tatizo ni pale wengi wao kutoweza kufuata miiko ya kazi ushereheshaji na kujikuta wanafanya comedy sehemu isiyotakiwa hivyo kuleta usumbufu usio wa lazima kama ilivyotokea kwa mpigwa kibao Chris Rock. Hapa Tanzania kuna washereheshaji ambao pia ni comedians wamekuwa wakilalamikiwa mno kuleta mizaha sehemu isiyotakiwa mizaha.

Ushauri wangu ni kwamba hawa comedians kama wanataka u-MC wajifunze baadhi ya mambo muhimu toka kwa manguli wa hiyo fani kama vile Taji Liundi, Cheni na MC GaraB ili kutojichanganya wanapokuwa kwenye majukumu yao. U-MC ni kitu kingine kabisa kinachojitegemea ndo maana hapa nchini ni comedians wachache sana wanaoweza kuingia kwenye top list ya ma-MC wanaoaminika na kulipwa pesa nyingi. Nampongeza sana comedian Joti kwa kuweza kusimama kwenye fani yake bila kuendekeza njaa za kutaka kuwa MC tena. Comedians jitahidini kutafuta namna nyingine ya kuongeza kipato ili kuepuka makofi kama ya Will Smith.
Kwa jina la nini? Stupid?
 
Kikubwa kama hujajipanga njoo umevaa helmet kabsaaa kukwepa makofi Makali
 
Ningekuwa ndio mimi Will Smith...
Ningerudia tena kumkata mambata kenge yeyeto atakayeingia anga zangu....
 
Wewe ndiye unasema hapo juu kuwa ungependa tusikie maoni yako juu ya masuala ya kitaifa. " Jingaz jinga" ( kwa sauti ya mama yangu)
Kesho nitatoa tamko kwa kinachoendelea ndani ya CCM... Maoni yangu ndo yatakuwa msimamo wa wanaJF
 
Mc anaweza kufanya comedy bila kuathiri mtiririko wa ratiba (anafanya comedy huku ratiba ya sherehe inaendelea kama kawaida), lakini Comedian anapokuwa Mc anajikuta anafanya comedy zake na ratiba ya sherehe inasubiri kwanza....

Mwaka fulani niliwahi kufanya kazi kwa pamoja na Masanja ukumbi wa Gold Crest hotel Mwanza, zoezi la utoaji wa zawadi aliliongoza yeye, alitutoa pale ukumbini saa 9:55 usiku.....saa kumi kasoro dakika 5.
 
Back
Top Bottom