Nimekaa sinza takriban 15yrs sasa sioni la maana zaidi ya barabara mbovu, mitaa kufurika maji, sewage water barabarani, nyumba mbovu kibao, hizo anazozungumzia mdau nyingine ni za miti zimekarabatiwa tu kwa mbele wakaweka vioo basi jamaa kachanganyikiwa. Sinza hakuna la maana zaidi ya Nyumba kuwa bei kubwa lkn hazina viwango. Kwa vile si mbali na mjini ndoo maana kila mtu mwenye kakipato ka kati anataka akae SINZA, lkn hakuna cha maana kabisaaa siku hizi uswahili kibao tuu. Zile nyumba ambazo miaka ile ta tisini zilikuwa na vyumba viine au vitatu sasa hivi zimegawanywa vyumba viwili viwili na vi master vya kubabia, so pale ambapo ulikuwa unapanga alone sasa mnakuwa wawili. Bado huko uani vimejengwa vijumba vya uani ambapo utakuta watu wawili wanakaa huko. Nyumba moja/kiwanja kimoja utakuta watu wanne wanaishi hapo uswazi mtupu.