Sawa unajua kujifariji sio kosa kikatiba na kibiblia,
Thamani ya mwanamke iko katika uchi wake, tofauti na mwanaume.
Kila mtu anafanya matusi kwa sana tu, sema ukizaa mtoto kabla ya ndoa ni doa!
Ni ishara ya;
-kutoka kwenye malezi mabaya ya wazazi/walezi wako
-utukutu/jeuri/kiburi cha kushindwa kusikiliza wazazi/walezi wako
-kufanya mapenzi holela na watu hovyo, na ndio maana hawajakuoa
Na hivyo;
-Watu wa kwanza kukupinga ni wa nyumbani kwako, wazazi/walezi wanakua na uchungu na wewe. hata mifano mibaya unatolewa wewe.yale makosa ya kawaida, kwako itaonekana makubwa zaidi.
-Watu wa pili ni wenzi watarajiwa; kutunza mtoto wa mwingine ni changamoto za kujitakia. usisahau kuna watu wana toka koo zenye roho na tabia za kurithi, zinaweza kuwa mbaya au nzuri.
-mtu wa tatu ni wewe, hata wewe huwezi kufurahi kijana wako wa kiume akuletee mke mwenye watoto!.(Ebu jifanye kukataa)
Kwamba vyema, muhimu na lazima kukwepa kuzaa mtoto/watoto kabla ya muda muafaka, kwepa kuzaa na kulea mwenyewe.
Kuna magumu mengi watu wanayapitia na hawasemi! Mitandaoni watu wanaonyesha furaha tu, ya moyoni wanayajua wao.
Hili la single maza liko kwenye kila familia, hii sio fasheni jamani Hivyo hatuwasemi kwa ubaya.