SINGLE MOTHER ANAYEFAA KUOLEWA.

SINGLE MOTHER ANAYEFAA KUOLEWA.

Barieda

JF-Expert Member
Joined
Aug 13, 2018
Posts
1,811
Reaction score
2,483
Habarini wapendwa wa jukwa letu pendwa la MMU.

Bila kurundika maandishi yasiyo na maana niende moja kwa moja maada, wapendwa hapa tusiwazungumzie single mother waliofiwa wenza wao( wajane) pamoja na wale waliotalikiwa hawa wana kundi lao.

Kina Dada waliopewa ujauzito hali wakiwa nyumbani, masomoni, au katika harakati za kutafuta maisha huko wanakoishi, hili ndo kundi ninalotaka kulizungumzia.

Aina hii ya single mother ndiyo inayoonekana kuwa kikwazo kwa waoaji na ndiyo inayolalamikiwa katika jamii kutokana na mazingira ya upatikanaji wa mtoto huyo kuwa amepatikana kwa njia isiyo halali yaani zinaa, kiuhalisia ni kweli lakini naomba dhambi hii ichukuliwe kuwa ni kama dhambi zingine ambayo mtu anaweza akafanya toba ya kweli akasamehewa na kutakaswa.

Kumbuka aina hii ndiyo inayonyooshewa kidole na kila mtu kuwa hawafai kuolewa na hii kutokana na baadhi yao kuonekana wanarudiana na wazazi wenzao ( kukumbushia) kutokana na bond ya mtoto, jambo hili ndilo kikwazo kwa kila mwanaume anayetaka kumwoa hata kama anampenda kiasi gani, na ndiyo maana hata wazazi huwachukia vijana wao wanapooa mwanamke wa aina hii.

Ili mwanamke aweze kuolewa na aweze kudumu katika ndoa yake anatakiwa awe na sifa zifuatatazo;
1. Kutofanya mawasiliano ya aina yoyote na baba wa mtoto au ndugu wa mtoto.
2. Kutokuwa na sababu yoyote itakayoweza kuwakutanisha kati yake yeye na mzazi mwenzie au ndg wa mtoto siyo za ugonjwa au kifo.
3. Kutofanya mazungumzo yoyote na mwanaye yahusuyo upande wa pili, aishiye kujua tu kuwa anayemlea siyo baba yake mzazi, ila mzazi alimkataa tangu kuzaliwa kwake. Kama atamhitaji asubir mpaka atakapoanza kujitegemea amtafute yeye mwenyewe kwa muda wake.
4. Aruhusu mwanaye kutumia majina ya mzazi mlezi ili kuimarisha uhusiano kati yake na watoto wenzie.
5. Awe kama alikata kamba na kuirusha baharini ikazama nikimaanisha hawezi irudia tena.

Mwanamke wa aina hii atadumu kwenye ndoa mpaka kifo, na ndiye anayefaa kuolewa. Nakaribisha maoni ya wadau.
 
Wengi wao huwa na stress...na wako tayari kufanya chochote baya au zuri...bora mradi liwalo na liwe...kupitia stress zao ni rahisi sana kupita nao caz wanakuwa kama wamewehuka...mioyo yao huwa na jazba na hasira mda wotee...ingawa sio rahis wao kumsahau baba wa mtoto/watoto...na pindi wakutanapo ni rahis kukutana kimwili na kutoa kinyongo..
 
Mkuu yawezekana uliyoandika yote ni sahihi lakini 10/100 ndio wanaangukia kwenye huo usahihi wako.
Kuwapata hao wenye usahihi ndio shughuli ilipo.
Wengi wanaangukia kwenye wrong ones wanaishia kujutia.

All in all wanawake wote ni wabinafsi tu.
Unaweza oa huyo aliyefresh akakupachikia watoto wote ikawa asavali ya singo maza tu.
 
Stress anakuwa Nazo pale tu anapoona kipengele cha ndoa kinakuwa kigumu kwake lakin ila akipata mme huisha.
 
Mkuu yawezekana uliyoandika yote ni sahihi lakini 10/100 ndio wanaangukia kwenye huo usahihi wako.
Kuwapata hao wenye usahihi ndio shughuli ilipo.
Wengi wanaangukia kwenye wrong ones wanaishia kujutia.

All in all wanawake wote ni wabinafsi tu.
Unaweza oa huyo aliyefresh akakupachikia watoto wote ikawa asavali ya singo maza tu.
Sahihi kabisa.
 
Hii ni bonge la ushauri wa maana.
Kwamaana
1. Kijana ukimuoa single mother hata ndugu zako huweza kukuchukia kabisaa.
2. Wanajisahau mno hasa wakipata hiyo bahati.

Ukipata bahati ya kuolewa ukiwa umeshazalia home ni jambo la kutoa hata sadaka ya shukrani.

Maana wengi wao huishia kuwa
1. Mke wa pili au hata wa tatu.
2. Kuongezwa mtoto mwingine wakiwa kwao.
3. Kuishi peke yao na watoto wao.
4.

Mwisho,jamii ya waoaji imejenga mawazo hasi juu ya watu hawa.
 
Mkuu ndugu watakaokuchukia ni wanafiki tu
Ujue tuna dada zetu kibao wamezalia nyumbani lakini ukiwaletea wifi mwenye mtoto wanaanza kukusema
Sasa huwa najiuliza, yeye ana utofauti gani na wifi yake?
Mpaka anaongoza kumsimanga?
Kawaida ya wanawake ni ubinafsi.
Wanajali watoto wao tu.
 
Back
Top Bottom