Singida United yasajili 'mashine' sita kwenye dirisha dogo

MAPUMA MIYOGA

JF-Expert Member
Jan 30, 2013
3,792
2,362
Dodoma. Wakati dirisha la usajili likifungwa saa 6 usiku wa Ijumaa, Uongozi wa Singida United umethibitisha kuwasajili wachezaji sita wakiwemo nyota wa kikosi cha Serengeti Boys.

Wachezaji wa Serengeti Boy waliojifunga Singida United ni aliyekuwa nahodha wa timu hiyo Issa Abdi Makamba, Ally Ng'anzi, Asad Juma na Mohamed Abdallah wamesajiliwa kwa lengo la kuendeleza vipaji vyao.

Mbali na makinda hao pia Singida United imemsajili mshambuliaji wa Danny Lyanga kwa mkataba wa miaka mwili akiwa mchezaji huru akitokea Oman.

Katika kuhakikisha inaziba vyema pengo la washambuliaji Atupele Green na Pastory Athanas, timu hiyo imefanikiwa kunasa saini ya mshambuliaji Mkongo Kambale Salita au Papy Kambale kutoka Etincelles ya Rwandwa.

Maoni yangu: Mwananchi please taarifa yenu mjue inakuwa na maana ikiripotiwa toka SINGIDA na sio DODOMA
 
hili la kuwachukua wachezaji wa serengeti boys ni mfano wa kuigwa, lakini wanatakiwa kuwapa nafasi ya kucheza, si kuwakalisha benchi msimu mzima.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom