Hawa hapa kuthibitishwa dirisha dogo TFF leo


kilimasera

kilimasera

JF-Expert Member
Joined
Dec 2, 2009
Messages
3,073
Likes
23
Points
135
Age
42
kilimasera

kilimasera

JF-Expert Member
Joined Dec 2, 2009
3,073 23 135
JUMLA ya wachezaji 26 wamesajiliwa na klabu za Ligi Kuu Tanzania Bara katika dirisha dogo lililofikia ukomo juzi tayari kwa kuanza mzunguko wa pili unaotarajiwa kuanza kutimua vumbi Januari 15 mwakani.
Wakati dirisha dogo likifungwa, kuna timu mbalimbali zinazoshiriki Ligi hiyo zimeshindwa kuongeza wachezaji wapya kutokana sababu mbalimbali.

Klabu kongwe za Simba na Yanga ambazo zilikuwa kwenye vita ya kuwania wachezaji, tayari zimekwishaanika majina ya nyota wao waliowasajili.

Yanga imemsajili mshambuliaji raia wa Zambia, Davies Mwape, na Juma Seif ‘Kijiko’ kutoka JKT Ruvu, wakati watani zao Simba wameimarisha safu ya ushambuliaji kwa kumtwaa mshambuliaji mwenye nguvu Ally Ahmed Shiboli kutoka maafande wa KMKM Zanzibar na kumrejesha beki wake Meshack Abel aliyekuwa African Lyon kwa mkopo.

African Lyon wao wamesajili wachezaji wanne ambao ni Shabani Aboma, Zahoro Pazi, John Njama na Hamis Yusuf huku Majimaji ya Songea ‘Wanalizombe’ wakiwatwaa Patrick Betwel, Yahaya Shaban, Kasim Kilungo, Mohamed Kijuso na Ulimboka Mwakingwe.

Toto African ya Mwanza, nayo imeongeza watano ambao ni Malegesi Mwangwa, Kamana Bwiza, Mussa Omary, Evans Paul na Saidi Manga, huku Kagera Sugar ikiwanasa Steven Mazanda na Juma Seif kutoka Gor Mahia ya Kenya, wakati Mtibwa Sugar imembeba Salum Swedi pekee.

Matajiri wa Azam FC na Maafande wa Polisi Dodoma, wamegoma kusajili na kubakiwa na wachezaji walioanza nao mzunguko wa kwanza wa Ligi hiyo, iliyoanza kutimua vumbi Agosti 21 mwaka huu.

Majina ya wachezaji hao yanatarajiwa kuthibitishwa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), leo ili kubaini wale ambao usajili wao ulikumbwa na kasoro kabla ya kuanza kwa Ligi hiyo.
 

Forum statistics

Threads 1,237,436
Members 475,533
Posts 29,288,290