Singida United vs Young African sports club niliyoyaona mimi

Matanga

JF-Expert Member
Nov 13, 2019
2,281
3,973
Nikirudi kwenye match yenyewe.
Tumepata kocha kwa hizi match tatu kwa upande wang a xxu nimeridhika naye ingawa match mbili tulipoteza. Na tulipoteza kwa mistake za kitoto za wachezaji, team kama team ilicheza vizuri. Team imeanza kupata rhythm. Teama imeanza kuimba wimbo mmoja.

Team inapoenda kushambulia. Unaona kabisa mabeki wanavyoanziasha shambulizi viungo wanavyolipokea winger zinavyofungua na kuingia ndani.
Kitu tumebakisha ni killer. Bado hatuna yule mtu wa kumaliza game. Mtu ambaye nafasi tatu za maana either mbili ama moja munashangilia. Mtu ambaye anajua kusoma move na kujua natakiwa niusubirie wapi mpira. Mtu ambaye kipindi winger na viungo wakifanya mipango tayari yeye anakuwa yuko pamoja nao kwa hiyo anakuwa tayari ana maamuzi kabla ya mpira kufika alipo.
Mtu ama mshambuliaji wa hivi ndio tunammiss.
Na sio kama hatuna, tunao ni suala la muda tu. Tunae Tariq seif huyu jamaa ni killer. Natamani apone kocha amkabidhi majukumu ya kuhakikisha nyavu hazilali njaa.
Kwa namna team inavyocheza pale mbele unakuwa Tariq tutacheka kimilionea. Kama tunacheza na double strike basi Nchimbi, molinga, yikpe hawa unawapa kazi ya kukimbia na kuwagasi mabeki ila killer aendelee na mission yake.
Na kama tunacheza na strike mmoja basi kazi ya viungo inakuwa ni kupitisha mipira hai tu watu tunacheka. Na tayari nishaanza kuona viungo wetu sasa hivi wanapitisha na kufikisha sana pasi hai kwenye 18 ya adui, sema wanakatishwa tamaa kwa vile hatuna killer pale mbele.

Ila pia ipo haja ya lamine kupewa mwenza wake wa kudumu ambaye atatengeneza naye wimbo wao kwa lugha yao ili kutengeneza ukuta wa Berlin. Kuna wakati tukishambuliwa kati panabaki uchi kwa sababu beki za kati wamekosa wimbo wao ambao unawaongoza, ile me nikienda we cover pale. Kwa sasa hamna. Tukipigwa pressure kubwa unakuta beki zote ziko sehemu moja then nyuma yao wanaacha pengo kubwa ambalo mpira ukipita tu basi tunaadhibika.

Kuhusu full back ya kulia mwambieni boxer anapokaa nje awe anajifunza kutoka kwa kaka yake Juma Abdul Mnyamani. Mnyamani mpunga unainama ila kwa anayoyafanya ni bora tu tumwachie namba yake. Boxer ni kijana ila ana mengi ya kujifunza kwa Juma Abdul. Hata msimu ulioisha ambao boxer alikuwa moto bado kuna vitu alikuwa anamiss na zaidi anapofika kwenye robo tatu ya uwanja ya mpinzani. Anaweza akafanya kazi kubwa sana alafu akaimalizia kwa fyongo.
Bado ni kijana boxer na tunamtegemea sana ila mwambieni asijitie kujua ajifunze kwa kaka yake Juma Abdul ndio anaweza kwenda ulaya.
Upande wa kushoto bado bado kidogo ila kwa waliopo kwa sasa jafari mimi siwezi mnyima namba. Wenda adeyun ni nzuri ila tu ile pressure ya yanga inamvuruga. Mwambieni atulize kichwa maana atapoteza namba yake kwa kiungo. Maana jafari ni kiungo. Adeyuni itakuwa aibu yake.
Pale dimba la chini, Mr captain kwa sasa hivi naomba muniache naye. Anakonga moyo wangu sana.
Kuhusu Niyonzima, muliobaki na kinyongo naye mutakuwa wachawi. Huyu jamaa ni anaujua haswa. Na 4anayajua majukumu yake. Na amerudi kuturudishia furaha.
Kipenseli huyu ana nia mbaya na sisi. Kwa maana sioni kama tutakuwa kwa kipindi kirefu huyu. Huyu anaondoka huyu ulayaaaaaa.
Kaseke huyu ni yanga. Ila pia hatabiriki, unaweza ukamsema vibaya Leo kesho akakumezesha maneno yako. Hana consistency tu ila jamaa anacover eneo kubwa sana ndani ya uwanja.
Yikpe bado naomba muda niendelee kutumtupia jicho. Ila tu naweza mshauri apunguze gym kidogo ili apate kauwepesi fulani hivi wana yanga tumtunze mihela.
Kwa magoalkeeper tulionao. Shikalo mwachieni namba yake tu. Metacha kabwili ni magoalie wazuri ila wana errors za kitoto. Mwambieni manyika amfunde vizuri metacha asiwe na tabia ya kudhurura dhurura uwanjani wakati kwake anakujua.

Molinga jamaa nadhani nitamfaidi sana na kuona faida yake siku atakapocheza na killer. Yaani molinga anasukumana na kuwachosha mabeki then killer anawaita kati.
Makame kasemwa sana na nadhani masemango yote kayapata. Sasa kilichobaki ni kumwelekeza namna ambavyo kiungo cha ulinzi alivyokuwa na umuhimu kwenye team.
Kwa match ya Leo dhidi ya Singida sijafurahi matokeo tu bali namna team inavyoimba.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Leo mmeshinda kocha mzuri au sio? Tutarudi Tena kuufufua huu Uzi juu ya huyo kocha wenu/dj.. mm nimeshika hiyo nukta ya kocha inshallah mechi mbili zijazo ntarudi apa kuufufua huu Uzi Mana wenzio walishaanza, kumtukana kocha
 
Back
Top Bottom