Singida: Mwanamke akamatwa kwa kukutwa na shehena ya wizi zikiwemo sabufa, kamera, pikipiki

real G

JF-Expert Member
Feb 7, 2013
5,227
5,292
Jeshi la polisi mkoani Singida linamshikilia mwanamke mmoja ambaye ametabulika kwa jina la Chitoto Paulo mkazi Singida kwa kujihusisha na wizi wa vifaa mbalimbali zikiwemo TV,pikipiki,sabufa,kamera na vitu vingine.

upload_2017-6-13_19-58-41.png



upload_2017-6-13_19-58-58.png


Kamanda wa polisi mkoa wa Singida ACP Debora Magiligimba amesema mwanamke huyo amekamatwa na vitu hivyo na uchunguzi wa awali unaonyesha anatumiwa na wezi kuhifadhi mali hizo au yeye mwenyewe anajihusisha na wizi na anatarajiwa kufikishwa mahakamaani.



Kwa upande wao badhi ya watu walioibiwa na kufika kutambua malizao,wamelisifu Jeshi la polisi mkoani Singida,kwani awali mali za wizi zilikuwa haziwekwi hadharani ili watu wazitambue.



Pamoja na Jeshi la Polisi kuwataka wananchi walioibiwa kutoka Singida na mikoa ya jirani kufika katika kituo cha kati mkoa wa Singida kutambua malizao ,amewataka wananchi kufanya kazi za halali badala ya kujihusisha na wizi.
 
Wanawake tunaweza..... :D
Tunaweza kweli jaman hapo kuna watu wamepoteza macho miguu katika kuporwa hizo Mali

Huyu mama aadabishwe kabisa mwizi namchukia sana nshaibiwa smartphone sikupata hela ya kununua mwaka mzima
 
Back
Top Bottom