Sijaambulia kitu! embu i translate ni sisi tuchangie!
Kuna kitu hapo sijaelewa aliposema "she threw out my daughters clothing......."
Kumbe Chris Brown ana binti?
CB ana mtoto mwenye miezi 10 na mrembo aliyezaa naye inaelekea hana au hapendi show offs anajielekea vyake kimya kimya bila kupiga kelele, ila imemgharimu mpenzi baada ya mpenzi wake Karruch kuamua kubwanga manyanga baada ya kusikia njemba miezi 19 iliyopita ilimpa uja uzito huyo mrembo. Picha ya chini ni CB na mrembo aliyeamua kubwaga manyanga kuashiria mwisho wa ngoma.
Dah na kweli bwana naona mtoto anafanana na Chris Brown!
Kama huyo Karruache atakua kabwaga manyanga kweli nitafurahi maana nilikua siipendi hii couple yao.
Napenda Chris akidate na Rihanna zaidi.
Ila sio ajabu wakarudiana maana hawa hata hawaaminiki.
Leo wanatukanana kesho wako pamoja!(Chris and Karruache)
lol! Wapenzi ca Chris asilimia kubwa wanataka kumuona na akiwa na RiRi kimapenzi wanapendana hawa ila kosa la RiRi ilikuwa ni kumwambia jamaa atangaze ndoa, jamaa akastuka na kudai umri wake bado mdogo kuingia kwenye ndoa maana ndoa inataka akili iliyotulia si ya kukurupukakurupuka. Karruche naye anadai anapendwa sana na Chris ila hawezi kuendelea baada ya kujua wakati wakiwa pamoja njemba ilikuwa inagegeda mrembo mwingine. Sitashangaa kusikia siku za usoni akiwa na mmoja kati ya hawa au wote sana sana itakuwa ni kuvuana picchu tu ili kupunguza genye zao sioni wa kuolewa na Chris hapo na sijui kama Chris ni muoaji. Si unajua watu wanaopendana kurushana roho kama kazi matusi wanatukanana halafu baada ya muda unawakuta wako pamoja utadhani si wao. Watu wengine wanajiwezea sana.
Kiukweli mimi ninavyoona Riri anampenda Chris kweli ila hili gumegume Karruache naona anapenda kick tu.
Hivi sasa Riri namuona hana raha kabisa yote ni sababu ya Chris.
Ila ni kweli Chris hawezi kuoa kwa sasa naona bado anakula ujana.Nasikia aliwahi kumuambia Karruache wafanye 3**s*u*m!...😕😕
Nitafurahi sana akirudiana na Riri!
Hahahahaha za kuwasoma wanaofunguka mitandaoni kuhusu 3sum lol!