Sina Mtu

ladyfurahia

JF-Expert Member
May 10, 2011
14,717
9,510
Habarini marafiki zangu;

Bado najipanga kuleta somo kwenu wakaka wa mjengo huu nilisema lazima kieleweke mpate somo ambalo litawajenga na kudumisha mahusiano yenu, hasa mnapokuwa katika mitingatinga, ila leo nimefurahishwa na nilipendelea niwaletee kawimbo haka kakuwafariji wale wote ambao wako katika njia panda.

Pengine rafiki umepambana na hali ngumu katika mahusiano yako ya ndoa au pengine mumeo amechepukia sehemu nyingine na kukuwacha wewe
na watoto ukiangaika na wala usione msaada wowote katika maisha hayo.

Pengine rafiki unapitia katika hali ya magonjwa magumu ambayo matabibu wamesema hauwezi kupona na unatarajia kifo kwako, kama yule mgonjwa aliyepooza kwa zaidi ya miaka 38 na hakuwa na matumaini yoyote ya kupona ugonjwa wake na wala hakuwa na tumaini kama ipo siku Mungu atamtokea na kumponya huyu.

Mtu tunamsoma katika maandiko matakatifu Hakuwa na mtu wa kumtumbukiza birikani wakati malaika anapokuja kuyatibua maji na na wala hujapata unafuu wowote.

Rafiki imewezakana umetumia dawa mbalimbali lakini hujapona basi wimbo huu utakapousoma taratibu utakufanya utoke na upate uponyaji na ufumbuzi wa tatizo la ndoa yako unalopitia nawe utapata afya, na Mungu atakutokea katika shida, au mambo magumu uyapitiayo.

Mungu amesema tumtwishe fadhaa zetu zote naye hujishughulisha sana na mambo yetu hivyo rafiki usinyong'onyee songa mbele. Jisemee moyoni mwako usikate tamaa liko tumaini na mlango wa kutokea katika shida.

Na barries unazozipitia mwangalie yeye mwenye kuianzisha safari yako ndiye atakayemaliza. Jenga tumaini jipya na mwelekeo mpya katika mazingira magumu uyapitiayo.

Hebu fuatilia wimbo huu moyoni mwako kimya kimya, usiniulize umetoka wapi soma maneno yake utafanya faraja toka kwa Mungu.

SINA MTU

CHORUS:

Aaaah Sina mtu, Ohooo sina mtu
mwenzenu sina mtu, ni kweli sina mtu

aaah sina mtu, ohooo sina mtu
mwenzenu sina mtu ni kweli sina mtu

Malaika anaposhuka kuyatibua maji
wenzangu watangulia mbele
bali mm sina mtu wa kunitumbukiza birikani
ohoo sina mtu, ahaaa sina
mwenzenu sina mtu ni kweli sina mtu x2

Rafiki utakaposoma maneno haya yatafanyika uzima na tumaini
kwa yale uyapitiayo usipuuzie kuwa makini, pls marafiki msi-joke
ujumbe huu ni mahususi kwa wale wanaopitia katika hali za matatizo
na shida mbalimbali na ni tumaini lao

warning: Do'nt jokes. I love u all mabestito KARIBU
Mamods msitoe hii stredi hapa ni mahususi

Wasalaam

Ladyf

cc: Mamndenyi, Kongosho, Bishanga, Mtambuzi, KakaKiiza, Asprin kiwatengu, utafiti, Passion Lady, charminglady, sweetlady, Lady doctor,
@C6, Young Master, Maxence Melo, nitonye, AshaDii, Chocs, Excel, SAYANSIKIMU, amu, Erickb52, mwallu, Heaven on Earth, Daudi1, Blue G, Joe Nyandigira, Kaizer, Eiyer, Jiwe Linaloishi, Kipaji Halisi , Mentor, Caroline Denzi,na marafiki zangu wengine wote


 
Asante sana ila kama huna mtu sogea pembeni tuongee vizuri pengine tunaweza kufanya maamuzi fulani ili siku nyingine utuletee wimbo wa NINA MTU
 
Hahahahahahaaa jamani huu ni wimbo mahususi kwa mtu ambaye hana mtu
asante sana ila kama huna mtu sogea pembeni tuongee vizuri pengine tunaweza kufanya maamuzi fulani ili siku nyingine utuletee wimbo wa nina mtu
 
Back
Top Bottom