Sina imani tena na Baraza la Mawaziri

Civilian Coin

JF-Expert Member
Dec 2, 2012
2,305
4,379
SINA IMANI NA BARAZA LA MAWAZIRI TENA

Kwa ukimya wà Mawaziri ni dhahiri wanajua fika UNGA unauzwa wapi na unatoka wapi? Wanajua fika Watoto wa vigogo wanaohusika katika biashara ya unga kupitia wasanii na watu maarufu na wao pia.

Ukimya huu unaweza kuwa ndio njia ya kufuta aibu ya matokeo ya FORM 4 mkoa wa Dar es Salaam na kuzima kelele za zilizokuwa zina hoji hotuba ya Rais Kule AU. Tusicheze propaganda kwenye mambo ya msingi.

Chama cha ACA tarajiwa kinawatakia HAPA KAZI TU njema.

Deogratius N Kisandu
Mtemi Kiongozi wa ACA tarajiwa.
 
Tatizo mkuu kawapiga pini,sifa zote za utendaji anataka zimfikie yeye binafsi.
Isitoshe inaonekana anawadharau na anampa kipaumbele Makonda.
 
shule 6 Kati ya 10 za mkiani huoni Kwanini wanapiga kelele zaidi muda huu ni kufuta aibu ya mkoa wa dsm kuwa wa mwisho. siasa ni mchezo mchafu
 
Kisandu wao wametumia sakata la madawa kuficha aibu ya matokeo mabaya ya form four,wewe umetumia sakata hilohilo la madawa kujitangaza na kukijenga chama chako.Nyie wanasiasa wote ni wanafiki.Siku zote mambo mnayofanya ni kuhusu maslahi yenu tu.
 
SINA IMANI NA BARAZA LA MAWAZIRI TENA.

Kwa ukimya wà Mawaziri ni dhahiri wanajua fika UNGA unauzwa wapi na unatoka wapi? Wanajua fika Watoto wa vigogo wanaohusika katika biashara ya unga kupitia wasanii na watu maarufu na wao pia.

Ukimya huu unaweza kuwa ndio njia ya kufuta aibu ya matokeo ya FORM 4 mkoa wa Dar es Salaam na kuzima kelele za zilizokuwa zina hoji hotuba ya Rais Kule AU. Tusicheze propaganda kwenye mambo ya msingi.

Chama cha ACA tarajiwa kinawatakia HAPA KAZI TU njema.

Deogratius N Kisandu
Mtemi Kiongozi wa ACA tarajiwa.

Hivi kweli Waziri Mwigulu yupo kimya kabisaaaa!!! au ameumizwa? Kwa kweli Makonda yupo juu sana. Mwigulu anapwaya sana heli mara dufu yule rafiki wa JPM aliyetumbuliwa. Mtazamo wangu jamani.
 
Back
Top Bottom