Sina imani na Maximo atatuharibia timu tu

Niyonzima karibu azam fc uwe bora na afya izidi kuimarika...
 

haiitaji kuwa na PhD ya soka kutambua kuwa maksimo si kocha sahihi kwa yanga. madudu anayoyafanya kila mtu anayaona. hatulalamiki kanakwamba timu iko kwenye nafasi mbaya, lahasha, tucholalamikia ni mpira usioeleweka ambao unafundishwa na maksimo. timu haishambulii kwa malengo inaishia kwenye mashambulizi ya kushtukiza yasiyo na madhara. ushindi wetu umepatikana kwa ujanja na juhudi binafsi tu za kina msuva lakini hakukuweko na mipango yoyote ile ya maana. maksimo hutufai
 
Niyonzima karibu azam fc uwe bora na afya izidi kuimarika...

Toeni kwanza taarifa Domayo yuko wapi? Kavumbagu kimemsibu nini hata ashindwe kutikisa nyavu tena? Azam jitambueni muwe mnatafuta wachezaji siyo kusubiri ku-scavange kutoka Yanga na Simba. Kwa mwendo huu timu yenu haina lolote jipya zaidi ya kununua mechi na kuhonga waamuzi.
 
Kaseja mlimuacha kwa kuwa kiwango chake kilikuwa kimeshuka mno, sasa hivi mnamtaka tena! Kwani kiwango chake kimepanda akiwa kwenye benchi la Yanga?

Kiwango kipo vile vile, tunachokihitaji toka kwake ni ile "leadership" yake
 
Kaseja mlimuacha kwa kuwa kiwango chake kilikuwa kimeshuka mno, sasa hivi mnamtaka tena! Kwani kiwango chake kimepanda akiwa kwenye benchi la Yanga?

Matale...Kati ya upumbavu ninaouona timu yangu simba inafanya ni kumsajili galasa Kaseja...Kaseja hana jipya tena.....Safu ya makipa wa Simba imetimia sana...Ndio maana nasema mpira wa kitanzania...si yanga si simba ni wa kipumbavu...At least Azam
 

Kavumbagu anaongoza ligi kwa kuwa na magoli mengi zaidi...Magoli manne
 
Omog na Phiri mmoja wao atstupiwa virago kabla ya msimu kuisha.

Nadhani Maxim ndiye atakaeachwa....Yanga sasahivi hakuna timu pale....Simba ni wavumilivu sana wameweza kumvumilia Phiri kwa droo 6 na sasa ni ushindi mechi zote zilizobakia
 

Timu haiwezi kushambulia tokea kati,ni hatari.........
 

wewe huujui mpira ni bora unyamaze
 
Kavumbagu anaongoza ligi kwa kuwa na magoli mengi zaidi...Magoli manne

Natambua hilo ndiposa nikauliza kwa nini hatikisi nyavu tena? Domayo yuko wapi? Mlimchukua akiwa mzima mmemfanyaje kijana wa watu?
 
Natambua hilo ndiposa nikauliza kwa nini hatikisi nyavu tena? Dmayo yuko wapi? Mlimchukua akiwa mzima mmemfanyaje kijana wa watu?


Domayo katoka pale mafuriko fc akiwa na majeraha ya nyama za paja,akaenda kupigwa kisu kwa Madiba!!

Ameambiwa asiguse mpira hadi January!!

Kuhusu kavu goals,ana magoli mengi kuliko Jaja,msuva,ngassa,javu na countinho ukijumlisha!!
 
Kwani ni lini Yanga imewahi kufundisha mpira na wakaelewa??

Yanga haina tofauti na taifa starz!!
 
Kwani ni lini Yanga imewahi kufundisha mpira na wakaelewa??

Yanga haina tofauti na taifa starz!!

Uko sahihi kabisa...leo ukiuliza Yanga ina mfumo upi wa mpira unaoeleweka hutapewa jibu....

Simba wao wanasifika kwa kucheza mpira wa pasi fupi fupi na wa kasi
 
kwani mwandishi wewe sio mmoja wao mlioenda kumpokea Maximo pale njiapanda ya ulaya kwa mbwembwe zote?
 
Haha watan amakweli nmeamin maneno haya, "Nyani haon Kundule!" Hy ya phile droo sita nyie ukawa inatumia mfumo gani?. Ila kwa jaja tuache unafik huyu jamaa yanga walichemka tenhe!
 
Matale, yaan hao Azam wana Mihela lakn tmu ya kbongo xaana.. TCHETCHE NA LIONEL na sureboy ndo wameibeba Azam
 
washabiki wa bongo bure kabisa hata akiambiwa amlipie bili ya umeme na maji mchezaji mmoja ataanza kumbwela mbwela
 
Haha watan amakweli nmeamin maneno haya, "Nyani haon Kundule!" Hy ya phile droo sita nyie ukawa inatumia mfumo gani?. Ila kwa jaja tuache unafik huyu jamaa yanga walichemka tenhe!


Hata mkapa anaamini hivyo
 

Attachments

  • IMG_20141117_190250.jpg
    111.7 KB · Views: 62
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…