vamda
JF-Expert Member
- Aug 1, 2012
- 919
- 599
Ndugu wana JF salamu. Leo tarehe 14.12.2014 yamenikuta ya kunikuta. Saa 3 asubuhi nilienda kituoni kupiga kura kwa ajili ya uchaguzi wa serikali za mitaa hapa jiji la Mwanza, mtaa wa Bugarika, kata ya Pamba. Nilisimama kwenye foleni ndefu hadi saa 10 adhuhuri. sijanywa chai wala chakula cha mchana. Foleni iliendelea kuwa ndefu maana msimamizi alikuwa mmoja tu. Tumbo lilianza kunisokota. Nilishindwa kuendelea kuvumilia. Nikaona isiwe tabu, nikaondoka kurudi home. Roho iliniuma sana kukosa haki yangu ya kupiga kura kutokana na utaratibu mbovu ambao ulisababisha watu wengine kuondoka kituoni bila ya kupiga kura. Tume ya uchaguzi imewanyima watanzania haki yao ya msingi ya kupiga kura. Niliona vijana wengi wakiondoka vituoni kwenda kutafuta riziki baada ya kuchoshwa na foleni ndefu kuanzia asubuhi hadi saa kumi. Hitilafu nyingine niliyoona askari polisi (FFU) wakienda vituoni ingawa hapakuwepo na vurugu zozote zilizotokea. Hali iliyoitafsiriwa kuwa ni kuwatisha wananchi. Pia wapiga kura ambao walisahau namba zao hawakuruhusiwa kupiga kura, waliambiwa waende kwenye ofisi ya mtaa kuangalia namba zao, Hali ambayo iliwapa usumbufu mwingi. Sina hamu na uchaguzi mdogo.