Simulizi Za 116 | Baraka Arudi Shule

Sema Tanzania

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2016
Posts
251
Reaction score
466
29/08/2017, Ambwene alipiga simu #116 kutoa taarifa kuhusu mtoto Baraka aliyekuwa akiishi na babu yake Mbeya. Ambwene anaishi Tunduma ila alienda kijijini kusalimia ndugu zake ikiwa ni pamoja na babu yake Baraka. Alieleza kuwa wazazi wa Baraka walifariki muda mrefu hivyo Baraka aliachwa akiishi na babu yake ambae ni mzee sana.

Baraka anasoma shule hapo kijijini kwa babu lakini aliacha kwenda shule, akilazimika kwenda kuchunga ngombe wa babu yake. Ambwene hakupendezwa na mazingira aliyokuwa akiishi Baraka. Aliona kama ndugu zake wamemtelekeza bila mtu wa kumsaidia. Alitaka kumsaidia asome.

Ambwene alipiga simu namba 116 kuomba ushauri kama anaweza kumchukua mtoto Baraka kwenda nae Tunduma ili aweze kuendelea na masomo.

Tuliwasiliana na Afisa Ustawi wa Jamii na Uongozi wa Kijiji anachoishi Baraka ili tuweze kuelewa mazingira ya babu na mtoto. Kwa msaada wa Mwenyekiti na Afisa Ustawi Ambwene alipata barua ya kupeleka kwa Mkuu wa shule ili Baraka ahamishwe shule. Uhamisho kwenda Tunduma ulikamilika na Baraka alianza masomo katika shule ya karibu.

Tuliwasiliana na Afisa ustawi wa Tunduma kujua maendeleo ya Baraka. Alituambia Baraka alifurahi sana kurudi shule. Utaratibu wote ulichukua takribani mwezi mmoja. Vilevile, watoto wake babu walimtafutia mtu mwingine wa kuishi nae na kumtunza. #SimuliziZa116 #116Stories
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…