gilbert35
JF-Expert Member
- Nov 20, 2021
- 247
- 474
SIMULIZI YA MAISHA : Mzigo wa Bosi uliharibu maisha yangu.
MWANDISHI: Gilbert Evarist Mushi
PHONE: +255621249611
SEHEMU YA 01
Kwa Majina Naitwa Gilbert Mwaitika, Nina umri wa miaka 25, Uzaliwapo mwanaume sharti upambane kwa jasho ili tu maisha yasikuendee kombo, umaweza kupambana kwa hisabati nzuri za kimaisha ama zile hisabati mbaya zinazopigwa vita. Niliamua kuzing'ang'ania hisabati mbaya lakini zilinigharimu. Amini Maisha si mteremko.
Anza Nayo
.... Ilikuwa ni jumatano tulivu yenye kiubaridi cha aina yake nikiwa stand ya mabasi Moshi Mkoani Kilimanjaro, nilikata tiketi yangu katika kampuni ya mabasi ya Kilimanjaro Expres tayari kwa safari ya kuelekea Dar es salaam. Ilikuwa ni safari ya kusafirisha mzigo nilioubeba katika tumbo langu. Hii ilikuwa ni moja kati ya misheni zangu za kusafirisha mizigo kama hii lakini kuusafirisha kupitia tumbo langu ilikuwa ni mara yangu ya kwanza katika misheni zangu.
Majira ya saa 12 alfajiri safari ilianza rasmi nami nilikuwa mmojawapo wa abiria. Nilipata siti ya mwisho kabisa tena dirishani, nilipenda kukaa karibu na dirisha ili nipate hewa safi kutokana na mzigo naousafirisha nilioubeba katika tumbo langu.
Wakati safari ikiendelea Majira ya saa 4 asubuhi nilishtuliwa na sauti ya Dada aliyeketi siti ya pembeni yangu,
"Kaka samahani, ni muda wa kwenda kupata kifungua kinywa maana naona umelala"
"ah ahsante,hapa ni wapi?". Nikakurupuka toka usingizini na kuuliza
" ni Korogwe tanga"
alijibu dada yule ambaye nilimfahamu kama abiria wangu.
Nilipotazama dirishani niligundua basi lilishafika Tanga na limepaki hoteli moja maarufu huku korogwe kwa ajili ya kuruhusu abiria kupata chai. Ndani ya basi abiria walianza kushuka kwaajili ya kwenda kupata chochote kitu.
"Hakikisha mdomo wako haugusi chochote hadi utakapofika"
Maneno haya yalipita katika kichwa changu. Nilikumbuka kauli ya bosi wangu juu ya kula au kunywa. Lilikuwa ni onyo kutokana na mzigo nilioubeba tumboni.
"kumbuka ukinywa au ukila chochote utajitafutia matatizo kwa afya yako na pia itakuwa ni rahisi kugundulika"
Nilizidi kukumbuka. Baada ya dakika 15 safari iliendelea,kila mtu alipata kifungua kinywa isipokuwa mimi.
"karibu tujumuike pamoja",
Abiria mwenzangu alinikaribisha. Nilipotupia macho nione anachokula ghafla mate yalijaa mdomoni, alikuwa akila Ndizi Roast na mishkaki ya Kuku.
Nilijikuta nameza mate lakini kabla ya kumeza nilikumbuka kitu.
"kumbuka kumeza mate ni sawa na kunywa maji. Jitahidi sana mate yakijaa mdomoni uyateme, hili ni kopo maalum utakalotemea"
Nilijikuta nazuia safari ya mate hadi kupelekea kupaliwa na mate, nilianza kukohoa kwa fujo baada ya Kipaliwa na mate.
Haraka jirani yangu alinipatia maji ninywe baada ya kuona nazidi kukohoa. Niliyakamata yale maji na kuyafungua kwa pupa. Nilianza kupeleka mdomoni na kuyafakamia, nikameza fundo la kwanza, nikakusanya fundo la pili tayari kwa kumeza lakini kabla sijameza la pili nilikumbuka tena maneno ya Bosi wangu,
"Endapo ikitokea umemeza mate jitahidi kwa haraka utafune vipande vitatu vya hizi biskuti. usizidishe wala kupunguza. maji usinywe kabisa"
"Mungu wangu nimekwisha.....nimevunja sharti ee Mungu nisaidie... "
Nilijikuta natamka maneno haya kwa sauti baada ya kutema maji yale nje. Niliyatupa maji yale chini bila kufunga chupa, kwa haraka nilifungua begi langu na kutoa pakiti ya biskuti.
"Hapa nakula vipande 6 kabisa ili vikanyonye haya maji".
Nilijisemea na kuvibugia mdomoni kisha kuanza kuvitafuna kwa pupa bila kujali macho ya watu waliokuwa wakinitazama, kila abiria ndani ya basi alinigeukia na kunitazama huku akiteta jambo.
"Una nini wewe kaka jamani"
Aliuliza dada huyu aliyenipa maji mda si mrefu, nilimtazama kwa hasira,
"kama si yeye nisingekunywa yale maji, ila uzembe ni wangu pia kwa kukurupuka. Haina haja ya kugombana nae"
Nilijisemea moyoni kisha nikakwepesha macho yangu kutoka kwa yule dada
"samahani, ni bahati mbaya si kusudi"
Nilimwambia yule dada kisha nikatazama mchezo wa kuigiza uliokuwa ukiendelea ndani ya basi kupitia tv iliyofungwa juu. Sikumbuki kama alijibu samahani yangu au lah.
Wakati natazama mchezo ule mara mlio wa ujumbe ukaita katika simu yangu, niliitoa na kufungua simu yangu aina ya Nokia Tochi
" Ukifika Dar usishukie Ubungo, Mwambie Dereva unashukia Mbezi. Pia ukishuka usipepese macho yako, utakaposhuka vua Kofia kisha Jikune kichwani Mara Mbili. Then Tazama angani kwa Sekunde Kumi. Hii itakuwa ni ishara ya Kumtaarifu atakayekupokea Umewasili Atakayekupokea amevaa Tisheti nyeupe na Track nyekundu, Miguuni atakuwa peku na atakupa salamu kwa kukuvalisha Kofia uliyokuwa umeivua. Vinginevyo ukiona kinyume Siye. Sawa?"
Ujumbe ulisomeka Hivyo. Taratibu nilivuta pumzi ndefu kisha kuitoa nje. Nilijibu ujumbe ule
"Sawa Bosi" kisha nikaendelea kutazama Mchezo uliokuwa ukiendelea Kwenye Basi kupitia TV.
Sasa ni Rasmi simulizi Hii imekamilika. Kwa malipo ya Tshs 1000/= unaweza kuipata yote kupitia Namba 0621249611
ITAENDELEA