Sehemu ya 02.
Kwa sababu aliipenda kazi yake, kila siku Catherine alikuwa akiangalia video za ngono, huko ndipo alipokuwa akijifunzia kila kitu, alichukua utundu wote huko, uchafu wote uliokuwa ukifanyika aliwafanyia wateja wake ambao walikuwa na pesa na kumfanya msichana huyo kuingiza kiasi cha shilingi laki tatu kila alipokuwa akitoka.
Kwa sababu alikuwa mtu hatari faragha, kila mmoja aliyefanyiwa michezo ya hatari alikwenda kumuhadithia mwenzake na hatimaye kila mwanaume kutamani sana kuwa na msichana huyo mrembo ambaye pamoja na fujo zake zote ndiyo kwanza alikuwa na miaka kumi na tisa tu.
Baada ya kupokea simu ya rafiki yake huyo, Catherine akainuka kutoka kitandani, alikuwa amechoka mno, siku hiyo hakutaka kutoka, alihitaji kubaki chumbani kwake, apumzike kwa ajili ya siku nyingine.
Hakutaka kwenda huko kwa kuwa alikuwa kwenye kipindi cha period. Alijiangalia alivyokuwa, hakuzoea kutoka katika hali kama hiyo lakini kwa kuwa aliambiwa na rafiki yake huyo watoke, hakuwa na jinsi, akajiandaa na kisha kumsubiria Amanda.
Baada ya dakika kumi na tano, honi zikaanza kusikika kutoka nje ya nyumba aliyokuwa akiishi, hakutaka kujiuliza mara mbilimbili, akajua kabisa kwamba alikuwa Amanda hiyo kutoka chumbani na kumfuata huku akiwa amevaa suruali yake ya jinzi ya bluu na fulana ya nyekundu ambayo aliikunja mikononi kwa juu.
“Umependeza,” alisema dereva wa Uber, japokuwa hakuwa akimfahamu vizuri msichana huyo lakini alishindwa kuvumilia, alijikuta akimsifia tu pasipo kujali kama Amanda alikuwa humo.
“Nashukuru kaka yangu!” aliitikia kwa sauti nyembambamba kabisa iliyomfanya dereva huyo kuchanganyikiwa.
Catherine alijua kutega, alijua ni kwa jinsi gani mwanaume alitakiwa kudatishwa, sauti yake ilikuwa moja ya mashambulizi makali sana ambayo alipenda kuyapeka kwa adui yake.
Mara ya kwanza tu ambapo ungebahatika kuisikia sauti ya msichana huyo ilikuwa ni lazima kumuomba namba yake ya simu kwa ajili ya mazungumzo ya faragha.