SIMULIZI: “TOKOMEZO” (03)
MTUNZI: XAVERY EMMANUEL (Starxav)
Email:
Xavemmanuel12@gmail.com
Whatsapp: 0769765748
Namba: 0672493994
Social Net: @star_xav
“Polisi?, Ndugu yangu umesema Polisi e? Loh! Polisi!, polisi!, polisi!!... Hapana walewale tu. Nimeenda zaidi ya neno nimeenda. Lakini napelekwa kubaya kulekule nilikotoka. Wametapakaa kila sehemu, hadi kwa viongozi wa dini” mgeni huyo bado aliendelea kunichanganya kwa vitu mbalimbali alivyokuwa anagusia.......
SEHEMU YA TATU
“Hhmmm!! Mume wangu me sielewi eti, kuna tatizo gani?” kama ilivyo tamaduni ya jinsia ya kike katika kuorodhesha viwango vya woga wao hadharani. Mke wangu alionyesha hofu ya juu kabisa kuonja kiu ya majibu kwa maswali anayouliza. Nilimtazama na kumwomba atulie chini.
“Mama eh!! Huyu ni mgeni humu ndani kama unavyojua, nimemsaidia huko mtaani kutokana na kutafutwa na watu wabaya. Hapa halipo sijui kama anaona sawasawa.
Mke wangu si unajua kazi yangu inahitaji ushuhuda mkubwa? Naachaje kumsaidia wakatika mimi pia ni sehemu maridhawa na kufanikisha nia yake!” nikajitapa kwa Mama watoto wangu kwa kile ninacho jivunia. Nilikuwa namaanisha nina uwezo wa kufikisha taarifa za mgeni wangu sehemu husika.
“Nisiwatie shaka! Mimi nahitaji tu vyombo vya habari!! Basi. Ukinipa msaada huo utakuwa umeokoa hadhi yangu na kizazi changu kilicho teseka duniani.. naomba msaada wako tafadhari” Mgeni aliendelea kuongea
“Vyombo vya habari!!!” tukajikuta tunasema wote mimi na mke wangu kwa pamoja.
“Ndio! Nataka mwandishi mahili na shupavu wa kutumia karama yake ya uandishi kuandika maneno yanayouma haswa kwa wahusika, nahitaji mtangazaji mahiri wa kutoweza kukosea majina yangu hadi mwisho wa habari, nahitaji vifaa imara vya kurekodi saiti yangu ili palipo na machozi yasikike kisawasawa.... naitaji tafadhali!, roho yangu ipo katika nungwe za mwisho katika kuutafuna uhai wa dunia. Wamenifuata hadi nimechoka. Wameniwinda hadi wamechoka. Wamenichezea hadi tumechoka. Sasa ni muda wangu wa kufungua kinywa na kueleza kile nilichoficha kwa muda mrefu...”
Tulivuta pumzi ndefu kwa pamoja mimi na mke wangu bila kutegeana, nikamwangalia mke wangu na yeye akatikisa kichwa kuashilia niseme kila nilichonacho: Nikasema.
“Pole sana!, dah! Pole kaka. Kama msaada huo umeupata, hakuna tatizo kabisa nakuambia!. Labda nikuuliza swali moja, ushawai kusikia tetesi za mwandishi bora wa magazeti Tanzania? Na ambaye anawika kwa sasa?” nilimtupia swali ambalo lilikuwa katika utani lakini likiwa na maana kubwa.
“Wanasema ‘mchagua jembe sio mkulima’ siwezi kuchagua nani asimamie kazi yangu, sipendi nikae hapa mda mrefu nitawasababishia matatizo. Nawaomba nipate huduma hiyo mapema kabla sijatokomezwa tena!, waandishi wengi nawajua, nawajua kwa majina na sauti ila kwa waandishi magazeti Mmmh!..... yah! yupo huyu Xavery Emmanuel. Nadhani ni bora kwa sasa, nafuatilia sana maandiko yake!”. Hapo aligusia pale ambapo mimi nililenga. Nilishukuru mungu kwa kurahisishiwa kazi yangu maana ingekuwa ngumu mno kuaminika.
“Sasa bila shaka umefika sehemu sahihi! Huyo mwandishi ambaye maneno yake yanatembea katika maandishi ndio mimi ninayeongea na wewe hapa. Ni vigumu kuamini ila ndio hualisia. Nafanya kazi na kampuni changa ya StarXav Entertainment ambayo makazi yake yapo hapo hapa Songea Mjini, ina wafanyakazi wachache sana na mahili nikiwemo mimi. Tumejizolea umaharufu mkubwa sana hasa katika sekta ya fahisi ya Kiswahili. Nakuomba nikusaidie tafadhari!!, mimi ndiye mtu sahihi na nilijitokeza kukusaidia hadi sasa.”
Baada ya utambulisho huo kwake hakuongea lolote kwa mda. Tukabaki kumsikiliza nini ataongea maana ukiona ‘kobe kainama ujue anatunga sheria’. Mgeni huyo hakuonyesha ishara yeyote ile kama amekubali au amekataa, aliinua kichwa na kukirudisha chini, akatikisika kidogo kwenye kochi kama mtu anayetaka kunyoosha misuli ili apambane na mshindani wake. Mwishowe akakaa sawa na kutoa neno.
“whwwwwww!, nilihisi ilo mda mrefu uliopita, ni sahihi kuwa ni wewe, sijawai kudanganywa toka nijitambue kuwa mimi ni mkubwa. Hizi ndizo hekima ambazo Mama yangu alinishushia. Na wewe ni miongoni mwa wahusika mwa mkasa huu.” Mgeni huyo alipoendelea kuongea, akaanza tena kulia.
“Ni kweli nipo sehemu sahihi lakini.., bado, bado nahitaji kutoka hapa. Nimekumbuka mtu ambaye anaratiba nzima ya siku yangu. Maisha yangu ni robo tu yapo hapa. Robo tatu kilo yapo kwa mpenzi wangu!, Mwandishi tafadhali mpenzi wangu hajui nipo wapi hadi mda hu. Nataka nikamuone jamani. nimemkumbuka” Kilio kilizidi ndani mule huku tusijue nini cha kufanya.
“Hapana baba, mda umekwenda sasa, nje ni hatari sana si kwema kama mlivyotoka. Nakuomba vumilia pumzika, kesho atafuatwa huyo mpenzi wako asubui, utamuona!, ukitoka tu nje tumepoteza kila kitu” mke wangu alidakia, na hakusubili neno kutoka kwa mtu akaendelea kuongea.
“Kwani hana simu?” akauliza,
“Ndio! Ndio!!, ipo ipo simu mwandishi, naomba uwasiliane nae. Hatakuwa yupo katika hali mbaya, sio kuto kula tu hata kujifungia ndini bila kutoka!, ongea naye tafadhali!”. Haraka nikatoa simu yangu mfukoni na kuanza kutafuta uwanja wa kuandikia namba ngeni.
“Namba yake tafadhali!” nilimuamuru huku nikiwa nipo makini kuandika bila kukosea.
“0769765........” nikapiga.. iliita kwa sekunde nne tu ikapokelewa. Nikampa simu ili aongee mwenyewe.
“Rose!, Mimi mume wako mpenzi, nipo salama, eh! mikono salama kabisa..... nahakika, eeh! kesho Mama. Nashukuru eh!. Ondoa hofu bhasi. Kumbuka kusali unapolala... Amina.” Simu ilikuwa fupi kisha ikakata. Tulishajua jina la mpenzi wake kuwa ni Rose, ndiye aliyekuwa anaongea naye mda huo. Lakini hadi wakati ule bado mgeni wetu hakujitambulisha. tulikuwa hatumjui.
“Sasa kaka jisikie hupo huru kabisa, hapa ni sehemu salama. Hawawezi jua kama hupo humu, mtaa wetu pia hupo na ulinzi wa kutosha, lakini bado hatujakufahamu hata kwa majina, mimi kama nilivyojitambulisha, huyu ni mke wangu anaitwa Marry. Tupo wawili tu hatujabahatika kupata mototo bado.” Nikamaliza na kusubili mpenzi wa Rose azungumze.
“Kama mnavyoniona sio nyinyi tu ambao mmekosea umri wangu. Wengi huko nje wananiita babu, kutokana na udhoofu wa mwili wangu, lakini katu nawaambia hata mwaka arobaini na kenda bado sijafika, mikunjo na hadaa za uso pamoja na mwili wangu ni kutokana tu na maangaiko mbalimbali ambayo nimepitia kwa takribani miaka na ushee sasa!, kwa jina Naitwa..” akasita kidogo kisha kuendelea,
“Abdul”. Akataja huku akiinamisha uso chini na kilio cha chinichini kikaanza tena, tulisikia tu jina hilo likitajwa tena katika kilio. Kulitaja tena alimaanisha hajakosea “Ab...dulii”. aliinama kuzuia machozi yake yasimchafue mbele ya mwanamke. Tukamtia moyo na kumbembeleza ili apunguze japo theruthi ya maumivu yake.
“Abdul, Shida nini?” mke wangu akuridhika, akaendelea kudadisi. Lakini cha ajabu Abdul sasa aliinua uso wake juu na kufuta machozi kwa mkono wake wa kushoto, baada ya hapo akatabasamu.
“Ndugu! Nitaeleza yote hadi mpenzi wangu awepo hapa. Kwa maana miaka yote niliyokaa na msichana huyo sijawai mwambia sababu ya mimi kutafutwa kwa namna hii, kila siku nampiga chenga tu kwa maana ilifikia hatua hata kumwamini mtu ilikuwa ni sumu. Siri hii naijua mimi tu peke yangu, labda kwa uchache ni hao wanaonitafuta kwa sababu wanaogopa kutolewa kwa siri yao. Mwenyezi mungu wa rehma kesho mapema pindi afikapo mpenzi wangu basi nitaweka kila kitu hadharani...... aaaagh! Ndio samahani kwa hilo mama!” alimaliza kwa kumtaka mke wangu radhi kwa kuto jibu alichoulizwa..
ITAENDELEA...
Starxav