TEMBELE LA UWANI
SEHEMU YA ISHILINI NA NNE
MTUNZI
Mbogo EDGAR
ILIPO ISHIA SEHEMU YA ISHILINI TATU: aliwaza Idd huku anaendesha gari kwa speed kama vile amechanganyikiwa, akikatiza eneo la daraja la bomba mbili, kitendo ambacho kilichangia Idd asimuone mzee mmoja mwendesha baiskeri, alie kuwa aingia barabara kuu, akitokea kwenye barabara ya pembeni, βIdd angaliaaaβ alipiga kelele Soraya, na Idd akazinduka toka kwenye wenge na kujaribu kumkwepa yule mzee mpanda baiskeri, lakini alishachelewa, maana katika kumkwepa alijikuta amemgonga kwa ubavu wa gari na kumsukuma pembeni kiasi cha kumfanya mzee huyu na baiskeri yake kuangukia mtaroni, kisha Idd akakanyaga mafuta na kuongeza mwendo.β¦ ENDELEA NAYO
Kwalengo la kukimbia msala, βwe Idd, hebu simamaβ alipiga kelele Soraya, huku anageuka kutazama kule mtaroni aliko angukia yule mzee mpanda baiskeri, βwa nini bwana msala huoβ alisema Idd huku anazidi kukanyaga mafuta, βtabia gani hiyo bwana, hebu simama huko, hatuwezi kumuacha mzee wa watu wakati umemgonga alisema Soraya kwa sauti ya ukali, huku anamtazama yule mzee na kumuona akijizoa zoa na kujiinua toka kwenye mtaro, βhaa mi ndio maana sipendi kufanya kitu mbele ya mademuβ alisema Idd akiwa anapunguza mwendo kisha akatazama kushoto na kulia halafu akageuza gari na kurudi pale walipo muacha yule mzee, ambae sasa alikuwa amesha toka mtaroni na kuanza kuikagua baiskeri yake, ambayo ilikuwa imeponde pondeka baadhi ya sehemu, βpole sana mzee wanguβ alisema Soraya huku anashuka toka kwenye gari akimuacha Idd ndani ya gari akiwa amekunja sura kwa hasira na kujisonya sonya, βasante mwanangu, lakini nashukuru sijaumia sanaβ alisema yule mzee ambae alionekana kuwa ni mpole na mwenye hekima, βhuwezi kujuwa mzee wangu, pengine umeumia ndani kwa ndani, tungeenda kwanza hospital ukatazame afya yakoβ alisema Soraya huku akimkagua mzee huyu kwa macho, βSoraya mbona unajitafutia mzigo bwana unajuwa tabia za hao wazee, ataanza kusingizia magonjwa kibao ili tutoe fedhaβ alisema Idd ambae alikuwa bado yupo ndani ya gari amekunja sura kwa hasira, βIdd mbona upo hivyo lakini, unajuwa kama tume mgonga mzee wa watu?β aliuliza Soraya kwa sauti ya kuchukizwa, βusijari mwanangu wala sijaumia nisiwapotezee muda wenuβ alisema yule mzee na Idd akadakia, βtena yeye mwenyewe ndie mwenye makosa, aliingia barabarani bila tahadhariβ kauli ambayo Soraya haikumpendeza kabisa, βsasa kama ni kosa lake?β aliuliza Soraya kwa ukali na kumfanya Idd atulie kimya, hapo kijana Idd akiwa amekaa ndani ya gari, Soraya akamsaidia mzee na pasipo kufunga buti safari ya hospital ikaanza, βwote watatu wakiwa ndani ya gari, βpole sana mzee, nashukuru kuona unaweza kutembea mwenyewe, kwani unakaa wapi?β aliuliza Soraya, ambae bado alikuwa amevaa niqab yake usoni, βnakaa luhila sekoβ alijibu mzee yule, βhooo jamani mbali, itabidi tumpeleke, maana baiskeri yake imearibikaβ alisema Soraya na hapo ni kama Idd alishindwa kuvumilia upuuzi wa Soraya, βhapo utanisamehe kwa kweli, si unajuwa inabidi niende kupeleka ujumbe kwa babaβ alisema Idd, akionyesha kuwa hakuwa anatania, βwala usiwe na shakaβ alisema Soraya, huku anatoa simu yake na kupiga kwa dereva wake Laylah.*******
Yap! mara baada ya kupigiwa simu na rafiki yake mkubwa wa siku nyingi na kupewa taarifa za kutaka kuchumbiwa kwa mwanae, hakika mama Joan alionekana kufurahi sana, βkweli huyu ni rafiki wa kweliβ alisema mama Joan, ambae sio mara moja amekuwa akiongea na rafiki yake huyo yaani shangazi yake Higgno na kumshtakia juu ya tabia za ajabu za mwane Joan, ambazo aliamini hakuna mwanaume atakae jaribu kujitoa muhanga na kumchumbia, βlakini leo licha ya kumfahamu Joan, anakubali aolewe na mtoto wa kaka yake?β alijiwazia mama Joan, sasa inabidi Joan abadilike, vinginevyo ataachika mara mojaβ aliwaza mama Joan na kutoa simu yake Mfukoni, akapekuwa namba kadhaa na kuipata namba ya Joan, kisha akaipiga na kusubiria ipokelewe, simu iliita mpaka ikakatika, na wakati ana jiandaa kupiga tena akaona ujumbe unaingia, kwenye simu yake hiyo hiyo, βtafadhari nipigieβ mama Joan akapiga tena, na safari hii haikuita hata mara mbili ikapokelewa, βniambie mama, siku sikia simu nipo kwenye keleleβ ilisikika sauti ya kike, ambayo haikutanguliza salam, ikienda sambamba na kelele za music mkubwa sana na sauti za watu kwa mbali, βyaani we mtoto, nyota yako ina nguvu sana, nikikuambia kitu we mwenyewe unaweza kuzimiaβ alisema mama Joan, βkuna dili gani tena mama nipe mchongoβ alisema Joan akionyesha kuwa alikuwa anatembea kusogea pembeni ya zile kelele, βumepata mchumba mwanangu, mtoto wa kaka yake yule rafiki yangu wa bomba mbiliβ alisema mama Joan, kikapita kimya kifupi, βlakini mtu mwenyewe ana hela?β aliuliza Joan, kwa sauti ya mashaka, βata takaje kuoa pasipo kuwa na fedha, lazima takuwanazoβ alisema mama kwa sauti ya kupambisha, βafadhari mama, niachache na mambo ya kudanga, maana mh!β alisema Joan, ambae kiukweli, anasiku mbili hajaonana na mama yake, kutokana na kushinda kwenye ma bar na kumbi za starehe, na mwisho kulala kwenye nyumba za wageni vyumba vya wanaume ambao wangehitaji kula kitumbua kwa usiku kucha, sio kwamba mama yake alikuwa hajuwi tabia ya mwanae, alikuwa anaijuwa vyema kabisa, tabia hii ambayo alianza kuionyesha toka akiwa shule, kabla haja feli mtihani wa kidato cha nne na kubakia nyumbani, sema alishindwa kumzuia, wala kumkataza, kwasababu wakati mwingine Joan ndie alieilisha na kuisaidia familia ile ya watu wawili, yaani yeye na mama yake, ambae aliachana na baba yake miaka kumi iliyopita, baada ya kugundua kuwa Joan hakuwa mtoto wake, na hapo ndipo mama huyo alipoanza kuishi kwa kutegemea kuuza kitumbua chake, ambapo soko lake lilianza kushuka kila umri ulipozidi kumuacha, na sasa hakuwa na soko kabisa na kuanza kumtegemea mwanae Joan kama duka lake la vitumbua, kuna wakati yeye ndie aliemtafutia soko.
Basi mwisho wa siku Joan na mama yake, wakakubaliana kuwa, kesho kutwa wakutane mapema ili waende bomba mbili kukutana na mchumba wake, ambae mpaka sasa hakuwa anamjuwa jina wala sura.*******
Mzee Frank, baada ya kufikishwa hospital na wale vijana wawili yaani yule wakike na wakiume, walio msukuma na gari lao, ambao mwanzo alidhania kuwa ni mtu na mke wake au wachumba, akamuona yule wa kiume ambae kiukweli hakuwa muuwangwana kama yule wakike ambae mpaka wanafika pale hospital hakuwahi kuiona sura yake, yule wakiume alishusha baiskeri ya mzee Frank na kuondoka kwa hasira,
Mzee Frank akamshuhudia yule mschana ambae kwa kuitazama mikono yake alionyesha wazi kuwa alikuwa ni mwarabu kama sio chotara, akiomba kuonana na doctor bingwa, na hata alipotokea yule doctor na yule mschana kufunua niqab yake usoni, βhoo Soraya, kulikoni tena jioni hii hapa hospital?β aliuliza yule doctor ambae akionyesha kumfahamu vizuri sana mschana yule, na kila walivyo zidi kukaa pale hospital na kupata huduma za vipimo na matibabu, mzee Frank alizidi kugundua kuwa yule mschana anaheshimika sana, japo hakuweza kumtambua ni nani na anatoka kwenye familia gani pale mjini ambayo inaheshimika namna ile, ila kiukweli aliweza kushuhudia sura nzuri ya mwanamke ambayo hakuwahi kuwaza kama hapa songea kuna mscana mzuri kama huyu, hakuweza kuthubutu kuwaza kama ingetokea Higgno akawa na mschana kama huyu, maana ingekuwa ni ndoto za Ali Nacha, maana unapo mzungumzia Soraya unamzungumzia mschana mrembo kweli kweli,
Kwasababu ya heshima ya Soraya mzee Frank alipewa huduma nzuri pale hospital, japo mzee huyu hakupatikana na tatizo kubwa katika mwili wake, zaidi ya mikwaruzo michache sehemu za mikono na miguu, Soraya akalipia huduma ile kisha wakatoka kuelekea nje ya jengo la hospital, huku kila mmoja akimshangaa mschana huyu mrembo, kabla hajashtuka na kujifunika ile niqab yake.
Pale nje walimkuta Laylah ameshafika na gari la Soraya, wakapakiza baiskeri na safari ikaanza, βdah! Soraya, imeishia wapi ziara yenu na kaka Idd?β aliuliza Laylah, wakati wa safari yao ya kuelekea Luhila, βmwehu yule ndie aliesababisha yote hayaβ alisema Soraya, huku safari ikiendelea.*******
Gari la aina ya Toyota Chaser, mali ya mzee Mahadhi Salum, lilikuwa limesimamishwa nje ya mtini pub, kwenye maegesho ya nyuma kabisa, βinawezekanaje Soraya awe na mwanaume halafu wazazi wake wasijuwe?β aliwaza Idd ambae ni wazi kabisa alikuwa amechanganyikiwa kwa kusikia Soraya tayari ana mchumba, ambae sasa alikuwa amekaa ndani kabisa ya bar hii anakunywa pombe kwa fujo, βnikimjuwa huyo fala, lazima ni mpoteze kwanza, halafu mengine yatafuata, hawezi kunizuia katika mpango wanguβ aliwaza Idd, lakini akapanga kuto kumuuliza mtu mwingine yoyote zaidi ya Laylah, ambae aliamini ndie mtu pekee ambae atakuwa anajuwa kila kitu kinacho muhusu Soraya.
Hivyo Idd alinunua chupa kadhaa za pombe na kuelekea karibu na kwa kina Soraya akasimamisha gari mita kadhaa toka kwenye lango la tajiri Mahamud, macho akiyaelekeza kwenye lango hilo kama vile anasubiri mtu atoke au aingie.******
Wakati huo mipango ya Talib ya kumteka na kumuuwa Soraya, bado ilikuwa inaendelea kusukwa kwa namna ambayo wao waliiona kuwa ni mikubwa sana, mpango huo ambao Talib na wenzake yaani Vitus na Zido, waliamini kuwa uta waletea fedha nyingi na kumsaidia mwenzao Talib kupewa nafasi za juu kwenye miradi ya mjomba wake, baada ya Soraya ambae atakuwa amesha uwawa.
Na mpango wao walipanga waufanye siku Soraya akienda nje ya mji, na sehemu nzuri ikiwa ni shambani kwake, βlakini kumbukeni kule anakuwa na dereva wakeβ alisema Talib, akiwakumbusha wenzake, βhilo jambo dogo, inabidi tutumie mbinu zote kumzuwia dereva wake asiende huko shambani na aende peke yakeβ alisema Zido, hivyo wakaendelea kupanga mipango yao.*****
Naam taarifa za mzee Frank kuletwa na gari nyumbani kwake zilisambaa karibu mtaa mzima, wakisimuliana kuwa βwamekuja na mwanamke mwingine amejiziba usoniβ hiyo ilikuwa kwenye kilabu cha ulanzi, ambapo wakina Nyoni, Komba na wakina Ngonyani walikuwa wanaongea, mwingine akatania βpengine ana ukoma ndio maana amejifunika sanaβ ilimradi kila mmoja alitania na kudharau.
Lakini ukweli ni kwamba kwa mara ya kwanza Soraya kutembelea familia ya hali ya chini na kujikuta wakiizoea kwa ucheshi na ukarimu wa familia ile, ambayo mpaka hapo walimkuta mke wa mzee yule na kuelezwa kuwa kijana wao anaishi mashambani, kitu cha ajabu Soraya alijikuta akiipenda sana ile familia na kuahidi kesho anakuja kuwaletea baiskeri mpya kufidia ile iliyoharibika,
walipofika nyumbani na Laylah kuegesha gari na kuondoka zake akielekea kwenye kituo cha dala dala, mara akashangaa kuliona gari aina ya Toyota Cherser likisimama pembeni yake, halafu akaonekana Idd akishusha kioo, βLaylah, ingia nikupeleke, alisema Idd kwa sauti ya kilevi na kumfanya Layla amtazame kwa macho ya mashakaβ¦β¦β¦ ITAENDELEA
TEMBELE LA UWANI
SEHEMU YA ISHIRINI NA TANO
MTUNZI
Mbogo EDGAR
ILIPO ISHIA SEHEMU YA ISHIRINI NA NNE: walipofika nyumbani na Laylah kuegesha gari na kuondoka zake, akielekea kwenye kituo cha dala dala mara akashangaa kuliona gari aina ya Toyota Cherser likisimama pembeni yake, halafu akaonekana Idd akishusha kioo, βLaylah, ingia nikupelekeβ alisema Idd kwa sauti ya kilevi na kumfanya Laylah, amtazame kwa macho ya mashaka.... ENDELEA NAYO SASA
βHoo! kaka Idd wala usisumbuke nitapanda dala dalaβ alisema Laylah kwa sauti ya shukurani, βhapana Laylah ingia kwenye gari kuna inshu nataka tuongeeβ alisisitiza Idd kwa sauti ya Kilevi, huku anamfungulia mlango, βLaylah, hakuwa na ujanja, akaingia ndani ya gari na kukutana na chupa kadhaa za pombe akashindwa kuhoji inakuwaje mtoto wa kiongozi wa dini anakunywa pombe kiasi kile.
Yap!! safari ikaanza kuelekea Mateka anakoishi Laylah, βLaylah, najuwa wewe ndie unayejuwa mambo ya Soraya, hebu niambie huyo jamaa yake ni nani?β aliuliza Idd bila kujiuma uma, akiamini kuwa huyo jamaa alieambiwa na Soraya atakuwa ni jamaa fulani handsome, mwenye mkwanja wa maana, βmh! kaka Idd mbona kama sijakuelewa, una ulizia jamaa yupi?β aliuliza Laylah, huku akijaribu kumtafakari Idd ambae alionekana wazi kuwa amelewa vibaya sana, βinamana ana wanaume wengi kiasi cha kushindwa kujuwa namuulizia yupi?β aliuliza Idd, kwa mshangao wa kilevi, βwanaume wengi awatoe wapi wakati hata huyo mmoja hajawai kuwa nae?β alijibu, Laylah, kwa sauti iliyojaa uhakika kwa kile alicho kisema, jibu ambalo sio tu kumsababishia mshtuko wa furaha Idd, pia ulimfanya asimamishe gari kati kati ya barabara, nusu asabishe ajari kwa magari yaliyokuwa yana kuja nyuma yao, βunasema kweli Laylah, kwahiyo alinidanganya?β aliuliza Idd, kwa sauti ya kuto kuamini, hapo Laylah akahisi kosa alilolifanya, kwa maana Soraya alidanganya kuwa anamchumba pengine kwa lengo la kumuweka mbali Idd asimfuate fuate, βsijuwi kama ni kweli au sio kweli, ila mimi ninacho juwa ni hichoβ alisema Laylah na kumuona Idd akiachia tabasamu la ushindi, βameisha, lazima nichukuwe ile ngomaβ alisema Idd, kwa majigambo kisha akageuza gari kwa mtindo wa U turn na kuanza kurudi alikotoka, βkaka Idd, mbona unanirudisha mjini? aliuliza Laylah kwa sauti ya mshangao, βhooo! samahani bwana nilisha sahauβ alisema Idd, ambae kiukweli alikuwa amelwa ile ile, huku anaweka gari pembeni, βpoa basi tutaonana keshoβ alisema Idd, akimaanisha kuwa Laylah ashuke toka kwenye gari, βkwahiyo hapa ndiyo umenipeleka nyumbani au?β aliuliza Laylah, kwa sauti ya mshangao na kutoamini, βkwani hauna hela ya dala dalaβ aliuliza Idd, kwa sauti ile ile ya kilevi.
Hapo Laylah, akajuwa kuwa hakukuwa na maelewano tena, kilichobakia ni kushuka na kusubiri daladala, hivyo akashuka na kumuona Idd anaondoa gari kwa speed kali, Laylah, ambae alishaona dalili za wazazi wa Soraya kutumia ujanja kuwaweka karibu Soraya na Idd kwa lengo la kutengeneza mahusiano ya wawili hawa, alijikuta anahisi maumivu ya moyo endapo Soraya ataingia kwenye mtego wa mpuuzi huyu na kuolewa nae.******
Siku ya pili Laylah alikutana na boss wake, yaani Soraya, ambae hakuweza kumueleza kilicho tokea jana baada ya wao kuachana, zaidi walienda pamoja mpaka nyumbani kwa mzee Frank, wakiwa na baiskeri mpya kabisa waliyo inunua siku hiyo hiyo na kumkabidhi mzee yule ambae walimkuta anahangaika kutengeneza baiskeri ile, βasante sana mwanangu, maana huu ndio usafiri wa kijana wangu toka akiwa shuleβ alisema mzee Frank wakati anashukuru kwa kuletewa baiskeri, βkumbe una kijana yupo wapi dar mwanza au mbeya?β aliuliza Soraya, ambae ni kama aliwazowea sana wanafamilia hawa, yaani mzee Frank na mke wake yaani mama Higgno, βyupo hapa hapa songea anahishi mashambani hukoβ alisema mama Higgno.******
Wakati huo huo, kijana Idd alikuwa amejifungia chumbani kwake anawaza jinsi ya kumnasa Soraya na kujimilikisha kuwa mke wake, βila jana nilibugi sana kukasirika mapema, kumbe alikuwa ananitegaβ aliwaza Idd akijilaumu kwa kosa alilolifanya, βsijuwi Laylah atamuambia kama nililewa sanaβ aliendelea kuwaza Idd, ambae baada ya kuwaza na kuwazuwa, akapata jibu, βyes nimepata wazo, kesho nikitoka nae, nitanywesha maji yenye dawa, akilegea tu na kula mzigo, nikimkuta bikira hatokuwa na ujanja, lazima atakubali nimuoeβ aliwaza Idd na kujitapa kuwa yeye ni mtoto wa mjini, hawezi kushindwa kitu, βtena ngoja nianze kumlainisha kuanzia sasaβ alijisemea Idd huku anachukuwa simu yake na kupiga kwa Soraya.******
Soraya na Laylah, Hawakukaa sana nyumbani kwa mzee Frank kule Luhila, waliaga na kuondoka zao, huku mzee Frank na mke wake wakiwakabidhi baadhi ya mazao ya shambani ikiwa kama zawadi, βkaribuni tena jamaniβ alisema mama Higgno ambae baada ya wakina Soraya kuondoka alimtania mume wake, βyaani jana uliporudi na huyu binti nikajuwa kuwa ndio mchumba wa Higgno aliekukabidhi wifiβ walicheka kwa pamoja kwa utani huo wa mama Higgno, βhiyo ndoto tuote kwa wajukuu zetu, mtoto huyu Higgno atamlisha niniβ alisema mzee Frank, akimaanisha kuwa isingekuwa rahisi kwa mschana kama Soraya kukubali kuolewa na Higgno.
Upande wa Soraya na Laylah wakiwa njiani, wanaongea na kusifu familia karimu ya mzee Frank, mara Soraya akasikia simu yake inaita, alipotazama akaona kuwa mpigaji ni, βkaka Iddβ ndivyo alivyo msave, sijui anataka kusemaje anaonekana ni mkorofi sana huyuβ alisema Soraya huku anaipokea simu, βhallow Soraya, mamboβ alisikika Idd akisalimia, salamu ambayo kwa maadili ya dini yao haikupaswa kuwa salamu ya kwanza, βassalaamu alaykumβ alisahihisha Soraya kwa sauti tulivu, βwaalaykum salaam, za toka janaβ aliitikia Idd, akiwa ameituliza sauti yake, βnjema tu sijui za kwako?β alijibu Soraya kwa sauti ile ile tulivu, na nyororo, ndivyo ilivyo sauti yake, βmimi kwangu sio njema, nimejisikia vibaya sana nilivyoghadhibika kwa ile ajali ya yule mzee wa shambaβ alisema Idd, akijitahidi sauti yake kuwa tulivu, βok! kwa hiyo jazba imekuisha?β aliuliza Soraya, ambae pia alishahisi kitu ambacho Idd anakitaka kwake, ni penzi na sio kingine, βkwa kweli nime jiona mkosefu sana mbele yako, naomba uniwie radhi, naahidi kesho tukienda bombambili nitayafuta makosa yanguβ alisema Idd, na hapo Soraya akatabasamu kidogo, βhebu nijulishe utayafutaje?β aliuliza Soraya kwa sauti iliyojaa shauku, akamsikia Idd anacheka kicheko cha kivivu, βkwanza nitakupeleka pale kwenye kachori, pili nitakupeleka sehemu tukapate juice nzuri ya bungo, hakika utakua umefurahi sanaβ alisema Idd kwa sauti fulani ya kirafiki iliyojaa ushawishi na utamanishi, βhakika utakuwa umefuta makosa yakoβ alisema Soraya, kabla hawajaagana, βhuyu mpuuzi jana nilimuambia nina mchumba akakasirika huyoo, ndio kisa cha kumpamia mzee wa watu, alisema Soraya baada ya kukata simu, βkumbe! kwa hiyo anawivu na weweβ alisema Laylah, wote wakacheka, βshauri zake mtu anaonekana anatamaa kama niniβ alisema Soraya, akionyesha kuto kumuamini Idd, βila da Soraya, we unamuonaje kaka Iddβ aliuliza Laylah, akishindwa kumueleza moja kwa moja matukio ya jana, βna muona kama wengine tu, macho juu juu, mwenye tamaa halafu yupo vile vile hata huko south sijui alikuwa anafanya niniβ alsema Soraya, βbasi inabidi uwe makini, si unajuwa hatujui huko South alikuwa anafanya niniβ alisema Laylah, huku safari ikiendelea.
Ukweli kitendo cha Idd kupiga simu na kuomba msamaha ni kama kilimvutia sana Soraya, na kufuta makosa yote na dosari za kijana Idd, maana ni kama alianza kuuteka moyo wa Soraya, na kumfanya aiwaze ahadi ya kesho kwenye juice ya bungo (ni aina fulani ya tunda zuri sana kwa kwa juice,) βpengine jana alichukizwa nilipo muambia nina mchummba anaonyesha kuwa ananipenda sana, tatizo anaonekana anatamaaβ, aliwaza Soraya.******
Jioni ile mzee Frank alitoka nyumbani kwake na basikeri yake mpya mpaka shambani kwa mwanae akamkuta yupo busy na mazoezi ya karate, na hata alipo muona Higgno alishangaa sana kuona baba yake ana baiskeri mpya, βnaona umechukuwa chuma kipyaβ alisema Higgno, mara baada ya kumaliza kusalimiana na baba yake, βnimechuku wapi, hii nimepewa tu! sijui tuseme ni fidia au sijui ni zawadiβ alisema mzee Frank na kumsimulia Higgno jinsi ilivyokuwa jana jioni wakati anatoka bomba mbili, βok! ndio umekuja kuni onyesha au unaifanyia test?β alitania Higgno, βhapana, nimekuja kukuambia kuwa kesho inabidi twende bomba mbili ukamuone mchumba wako, shangazi yako amekuchagulia kitu cha uhakikaβ alisema mzee Frank, ambae hakuwa ana mfahamu huyo mschana ambae dada yake amemchagulia Higgno, βkwa hiyo kesho saa ngapiβ aliuliza Higgno ambae alionekana wazi kuingiwa na kiwewe,
Ukweli ni kwamba, licha ya kuwa siku za nyuma hakuwa na mzuka mkubwa wa mapenzi, hasa baada ya kufanyiwa mambo ya kijinga na Hilda, lakini siku za hivi karibuni kijana huyu ambae umalizia haja zake ndotoni, ameanza kupata mzuka wa kula kitumbua, hivyo kuna wakati alitamani kuwa na mwanamke wake mwenyewe, lakini hakuwa na uwezo wa kusimama na mwanamke na kumueleza anavyo jisikia, alisha ingia uoga mkubwa sana, kutokana na yale aliyo fanyiwa na Hilda, hivyo akajiona kuwa ni dhaifu hakuwa na fedha za kuweza kupata mwanamke mzuri, na kwamba wanaopata wanawake wazuri ni wale wenye fedha pekee, βdah! ndio na muweka sawa halafu namβ¦β aliwaza Higgno huku ana geuka kutazama kibanda chake kilicho jengwa na kwa udongo na kuezekwa na bati chakavu.
Hata baba yake alipoondoka huku wakiahidiana wakutane mida ya saa tisa maeneo ya shule ya msingi Sokoine mita kama mia mbili toka nyumbani kwa shangazi yake Higgno, Higgno alisitisha mazoezi na kuanza kufanya usafi wa kina ndani ya kibanda chake, huku akipanga vitu ndani kwa utaratibu mzuri, akitarajia mgeni wakati wowote aje azindue kitumbua na kupata utamu ambao alikuwa ana upata ndotoni, na katika upangaji wake alizingatia sana maeneo ya kitanda, ambacho alikifanyia marekebisho kuhakikisha kina mudu kubeba watu wawili wanaopeana kitumbua.
Baada ya kumaliza hayo Higgno alihamia kwenye mitego, ambayo aliisambaza sehemu mbali mbali msituni na mtoni, akitarajia kuwa mgeni wake akija kumtembelea akute kitoweo cha nguvu kiasi kwamba asitamani kuondoka, βmchumba wangu, hapa ninakaa kwa muda tu, nikipata kazi tutahamia mjiniβ aliwaza Higgno jinsi atakavyo muambia huyu mwanamke, ambae hakutambua kuwa alikuwa ni mschana ambae anamfahamu nje ndani, βkesho mapema naenda kumnunulia zawadi moja bombaβ aliwaza Higgno.******
Mahamud na mzee Mahadhi waliwasiliana kupeana mrejesho wa mpango wao wa kuwa unganisha watoto wao, βnadhani kuna mafanikio maana leo Idd ameniambia wanatoka tena keshoβ alisema mzee Mahadhi Salum, βbasi maendeleo ni mazuri, βmaana hata jana naona Soraya alichelewa kurudi, inaonyesha aliipenda sana hiyo safariβ alisema bwana Mahamud, hawakujuwa kuwa kuna mambo ya ajabu yana endelea kati ya Soraya na Idd,
Siku iliyofuata siku ambayo, Idd aliapania kumaliza kazi kwa show moja ya maana pale atakapo kula kitumbua cha Soraya, na akipania kukuta akiwa bado hajawahi kuingiziwa dudu, kwa maana atakuwa ameuwa ndege wawili kwa jiwe moja, ikiwa ni kuonja kitumbua cha mwanamke bikra kwa mara ya kwanza na pili kumfanya Soraya asiwe na ujanja kwake, kwa maana ya kwamba tayari atakuwa amesha muondo lea anacho jivunia na kinachompa heshima yeye mwenyewe na wazazi wake, na kwa kupania kutunza siri lazima Soraya ataogopa kuwa na mwanaume mwingine na kutulia na yeye, hivyo itamfanya yeye amuendesha anavyotaka, kwasababu hatokuwa na pakwenda kwa kukwepa aibu ya kutolewa uschana wake kabla hajaolewa.
Mida ya saa nne za asubuhi, Idd alichuwa kiasi cha fedha laki tano toka kwa baba yake na kulekea kwenye hotel moja ya wahindi, na kununua juice ya bungo lita moja, kisha akaingia nayo kwenye gari na kuiweka madawa ya kulevya kiasi fulani na kuifunga kisha akaitikisa vizuri, halafu akawasha gari na kuelekea bomba mbili, alitumia gari la baba yake, yaani lile lile la jana Toyota Chaser, moja kwa moja akaenda kwenye bar moja kubwa na maarufu ya Kuchile bar, akamtafuta mmoja wa wahudumu na kuongea nae jambo fulani, βusjali nitakupatia laki moja, ukinifanikishia mpango huoβ alisema Idd, katika mpango wao, βwala usijali kaka yangu, wewe tu, si umesema saa kumi utakuwa hapa, mimi nita hakikisha umesha muingizia chumbani umemaliza nitakusaidia kumtoa ndio niondoke zangu, maana mimi namaliza zamu yangu saa tisaβ alisema mwanadada mmoja ambae hata ukimtazama tu ungejuwa ana roho ngumu, kwa jinsi sura yake ilivyo, basi Idd alimkabidhi yule mwanamke lile chupa la juice, yaani ukiniona tu njoo fasterβ akija mwingine na kuagiza lazima ata mwambia hakuna juice mahali hapaβ alisisitiza Idd kabla hajaondoka na yule mschana kwenda kuhifadhi juice ile kwenye friji.******
Wakati Idd anaanza mipango ya kujilia kitumbua cha Soraya kiulaini kabisa na kujijengea ngome, Soraya mwenyewe alikuwa njiani na dereva wake wanaelekea shamba la mbengu huko lumecha kwenda kufuata miche ya mitunda ambayo waliagiza, maana siku iliyofuata ambayo ni ijumaa walipanga waipeleke shambani kule mahilo mara baada ya swala ya ijumaa, βvipi bado safari yako ya bomba mbili ipo pale paleβ aliuliza Laylah, βipo pale pale, lakini unadhani ina madhara yeyote?β aliuliza Soraya, ambae siku zote akiwa kwenye gari lake hukaa seat ya nyuma, βunadhani ukaribu anao uleta kaka Idd ni wakawaida kweliβ aliuliza Laylah, βniwazi kabisa kaka Idd ananitakaβ alisema Soraya, βkwa hiyo we unaamua nini?β aliuliza Laylah, ambae ndie mshauri wake wa karibu, βlakini jana aliniomba msamaha kwa kile alichokifanya juzi, naweza kuwa na busara kidogo, istoshe baba na mama wanaonekana wanampenda Iddβ alisema Soraya, na hapo kikapita kimya kifupi, Laylah akiwa kama vile ana tafakari jambo, βvipi Laylah, kwani kuna ubaya wowote kama nitaolewa na Iddβ aliuliza Soraya, βkikubwa ni kutazama moyo wako unavyosema, ila ungefanya uchunguzi kwanza kabla ya loloteβ alishauri Laylah huku safari inaendelea.******
Siku hii ya leo ambayo ni al khamis, kijana Higgno aliwahi mjini mapema saa sita mchana, kwa lengo la kununua zawadi nzuri ya mchumba wake ambae anaenda kuonyeshwa leo, βnitaomba tusogee pembeni ili tupange juma pili nije nimchukue nimpeleke ghettoβ aliwaza Higgno huku anatabasamu na kuvuta picha ya mschana mzur na mpole akiwa ndani ya kibanda chake kule shamba.******
Siku hiyo mida ya saa saba za mchana ndio mida ambayo Joan alifika nyumbani kwao, akiwa mwenye hangover mbaya na kukutana na mama yake, ni baada ya kuto kuonana kwa siku tano mfululizo, akimkuta mama yake amesha jiandaa, nae akavaa gauni lake refu huku baadhi ya nguo zake kama vile suruali yake ya kubana na kijishati kifupi akakiweka kwenye mkoba wake,
Saa tisa ndipo walipoanza safari yao kueleka bomba mbili, huku njiani wakijadili jinsi maisha ya uchumba mpaka ndoa yatakavyo kuwa, βwakina mama Sinachangu wataziba midomo mwaka huu, watakavyoona unafanyiwa send off, alisema mama Joan wakati wanatembea kwa miguu kueleka nyumbani kwa shangazi baada ya kushuka kwenye dala dala, βsana, na walivyo kuwa wananisema vibaya pale mtaani, mbona lita washuka, alisema joan kabla hajapata wazo, βsasa mama ngoja kwanza nipitie pale nikashtue hata bia mbili za kutoa hangover nipate na nguvu ya kuongea na mchumba mwenyeβ alisema Joan, βmh! tungefika kwanza si unajua pale nyuma ya sokoine kuna ile bar nzuri, halafu usinywe bia inaharufu kari, kunywa hata pombe kari tena kidogo tu!β alishauri mama Joan, hapo umenena, tena mpigie shangazi muulize kama bado hawajafika nisije kushindwa kutoka paleβ alisema Joan, wala usiwe na wasi wasi, hata tukiwakuta nitajifanya nakutuma dukaniβ alisema mama Joan, ndio maana nakupendaga mamaanguβ alisema Joan, ambae kama ungebaatika kumuona alivyovaa wala usinge amini kuwa anakunywa pombe, kumbe alikuwa anavuta mpaka bangi.******
Mida hii mzee Frank alikuwa amesimama kwenye duka moja dogo lililopo kwenye safu ya maduka na bar pembezoni mwa barabara ndogo ya vumbi inayoelekea kuchile bar, inayo tazamana na shule ya msingi sokoine, akitazama watoto wa shule waliokuwa wanacheza kwenye viunga vya shule wakisubiri muda wa kutawanyika kueleka makwao, alicho kiona kilimkumbusha wakati mwanae Higgno anasoma shule ya msingi Luhila B, kipindi binti Kommba yaani Hilda au
TEMBELE LA UWANI kama wanavyo muita, akiwa anamsonga Higgno kila anakokwenda, βkalianza kupenda hela mapema sana kale katotoβ aliwaza mzee Frank huku anatazama watoto wa shule, waliokuwa wanaendelea kucheza, βhuyu atakuwa wapi mpaka sasa? au amesha kimbia mke?βaliwaza mzee Frank huku anatazama saa kwenye simu yake, βna yeye inabidi anunue simu kijana mzima anakosaje simu sasaβ aliwaza mzee Frank akionyesha mashaka juu ya uchelewaji wa Higgno, βkwa miaka hiyo haikuwa ajabu kwa mtu kukosa simu, kwasababu bado mambo yalikuwa ni mageni).*******
Naam saa kumi kasoro, Soraya alikuwa nyumbani kwao amesha jiandaa, akatoka na kuungana na Idd ambae toka masaa mawili yaliyopita alikuwa anamsubiri pale sebuleni, akiwa na mzee Mahamud wanaongea hili na lile, maana alifika hapa kabla hata Soraya hajarudi toka Lumecha, βkumradhi kwa kukuchelewesha, alisema Soraya kwa sauti iliyojaa upole na unyenyekevu, usijari da Soraya, hata baba aliniambia kuwa ulienda Lumechaβ alisema Idd kama vile aliridhika kweli toka moyoni, lakini ukweli alishatukana matusi ya kila rangi na kutoa ahadi nyingi za kumkomesha leo hii.
Wawili hawa waliaga na kuondoka zao, wakitumia gari lile lile la mzee Mahadhi, yaani Toyota Chaser, safari ilianza kimya kimya mpaka walipo uacha mji na kukamata barabara ya bombambili, βleo umezidi kupendeza Soraya mpaka namuonea wivu huyo mchumba wakoβ alisema Idd, akimchezea akili Soraya, maana alikuwa anafahamu fika kuwa Soraya hakuwa na mchumba wala mwanaume yoyote, βnimtoe wapi mwanaume, nilikudanganya tu janaβ alisema Soraya, huku safari inaendelea, hapo Idd aliachia tabasamu pana kweli kweli, βnilisha juwa toka kitambo kuwa unanidanganyaβ alisema Idd, wakati anapunguza mwendo kwenye kituo cha daladala cha kwa Sanga one na kukata kona kushoto kuelekea kule walikoelekea juzi kupeleka mzigo, βmh!!! muongo, mbona uliβ¦β kabla Soraya ajaongea neno, akasita na kutazama mtu aliekuwa anavuka barabara akionyesha ana haraka sana, akiwa ameshika kijikapu fulani kikionyesha kilikuwa na vitu fulani toka suka la urembo na vitu vya wanawake, βvipi mbona kama unashangaa sana aliuliza Idd, akiwa amesha ingia barabara ya upande wa kushoto, βkama kuna mtu kama nimemfananisha, hebu simamisha kwanzaβ alisema Soraya akimaanisha kuwa amemuona yule kijana mpole aliemsaidia miaka mingi iliyopita, lakini wakati Idd anatafuta sehemu ya kusimamisha gari, Soraya alimuona yule kijana akiwa amesha vuka barabara na kukodi piji piki wakati huo songea walikuwa wanaziita yebo yebo, kisha kuondoka zake akionekana ana haraka sana, βamesha ondokaβ alisema Soraya kwa sauti iliyopoa, ni nani huyo?β aliuliza Idd huku akikanyaga mafuta kuondoa gari, βhuwezi kumfahamu, hata mimi mwenyewe sina hakika maana nilimuona miaka mingi iliyopitaβ alisema Soraya.****
Wakati huo pia Joan na mama yake walishafika kwa shangazi, na baada ya kusalimiana na kupeana mikakati, Joan akaaga na kuondoka kuelekea kule alikomueleza mama yake ili akashtue kidogo kukata lock na kupata stimu.
Kitu cha kwanza kabisa mara baada ya kufika eneo husika, joan aliipita bar na kulifuata duka moja la jirani yake, akanunua sigara moja na big G kumi, kisha akaiwasha ile sigara yake na kutokana nayo nje ya duka, akatazama kushoto na kulia kama kunge kuwa na mtu wa kumuonea aibu, lakini hakuona mtu yeyote ambae angeushtua hata mshipa mmoja wa aibu, zaidi ya mzee mmoja aliekuwa amesimama huku ameshikilia baiskeri yake japo alionekana kumtazama kwa mshangao lakini Joan hakumjari, akapiga pafu la pili la sigara yake, huku anatembea kuelekea ndani ya bar, na wakati huo huo Joan akasikia mlio wa pikipiki, alipogeuka na kutazama nyuma akaiona pikipiki inasimama na akashuka Higgno, βhooo! Higgno, za masiku mshkaji wanguβ alisema Joan kwa sauti ya kuchangamka, huku moshi wa sigara ukimtoka mdomoni mwake, akimsogelea Higgno na kumfanya yule mzee mwenye baiskeri mpya ashangae..., Haya hayaaaaa soraya yuleee anaenda kutolewa bikra Higgno nae kakutana na joan akiwa pamoja na mzee wake, mpaka sasa wote tumefahamu kuwa joan rafiki wa hilda ndio mchumba alieitiwa Higgno, je nini kitajiriiiii? Idd atafanikiwa kutoa bikra ya sorayaaaaaa? Kumbuka hiyo ni siku ya al khamis na siku ya ijumaa talibu nae ana mpango wake wa kumteka soraya, je atafanikiwaaaaaaaa, usikae mbali nami kwan nitakuletea mkasaa huu mwanzo mwisho hapa hapa
jamii forums