Simulizi tamu ya bibi mwenye miaka 101 Moshi

Simulizi tamu ya bibi mwenye miaka 101 Moshi

REDEEMER.

JF-Expert Member
Joined
Feb 22, 2015
Posts
8,918
Reaction score
14,894
pelagia.jpg

Bibi Pelagia John Maina akisoma Biblia bila kutumia miwani ya kusomea, nyumbani kwake Kilema, Moshi Vijijini, mkoani Kilimanjaro.
By Rehema Matowo, Mwananchi,

Moshi. Kutokana na mfumo wa maisha tunayoishi, vyakula tunavyokula na mabadiliko ya tabia, maisha ya mwanadamu kuishi duniani ni mafupi sana ukilinganishwa na maisha ya zamani walivyoishi wazazi wetu.

Hata vitabu vya Maandiko Matakatifu kama Biblia, vinasema kuwa maisha ya mwanadamu ni miaka 70 ya kuishi lakini ukiwa na nguvu ni miaka 80 na tena yamejaa tabu na mateso .

Kwa miaka ya sasa ukisikia mtu amekufa akiwa na miaka 70 anaonekana kuwa ni mzee sana na tena kila mmoja atasema kwa kweli Mungu amempa maisha marefu.

Kutokana na umri wa mwanadamu kufupishwa kutokana na mfumo wa maisha, nilipata taarifa kuwa kuna mtu mwenye umri zaidi ya miaka 101 katika Kijiji cha Marawe Kyura, Kata ya Kilema Chini Wilaya ya Moshi Vijijini, mkoani Kilimanjaro.

Umri wake ulinivutia na hivyo nikaona nimwone ni mtu wa aina gani lakini pia niijue siri ya mafanikio yake ya kuishi miaka mingi kiasi hicho tena akiwa na nguvu .

Nilianza safari ya kuelekea Kilema nikiwa na shauku ya kumwona kwa kuwa nilikuwa nikisikia mtu akizeeka hubadilika na kurudi kuwa mtoto sasa nilitaka kujua mtu mzima anarudi vipi kuwa mtoto.

Pamoja na kuishi miaka 101 akiwa na, macho yake yanaona vizuri na yenye uwezo wa kusoma bila kutumia miwani na masikio yanasikia bila shida yoyote. Haya ndiyo yaliyonifanya kumtembelea. Jambo ambalo lilimshangaza kila mtu anayesikia habari zake na kushangaza ni pale anapoweza kuamka mapema asubuhi na kusali pamoja na kusoma biblia bila shida yoyote bila kutumia miwani. Pamoja na kusoma bila miwani anao uwezo mkubwa wa kuona mbali bila matatizo yoyote.

Itakumbwa kuwa ziko taasisi nyingi na shule nyingi za sekondari na seminari na vyuo katika eneo la Kilema kama vile Mandaka TTC, Chuo cha Veta, Seminari ya Kilema, Sekondari ya Olaleni, Sekondari ya Mivinjeni, Sekondari ya wasichana na Kituo cha Convent ya masista Masaera, Parokia ya Mandaka, Parokia ya Kilema, Sekondari ya Lombeta, Seminari ya Maua, Parokia ya Maua, Sekondari ya Ruwa, bila kukosa kutajaHospitali Teule ya Kilema ambayo inawahudumia wagonjwa wa eneo la Moshi vijjini.

Hatimaye nilifika nyumbani kwa Marehemu Mzee John Maina, mume wa Bibi Pelagia, aliyefariki dunia mwezi Julai 2004 akiwa na umri wa miaka 94. Hapa ni Kitongoji cha Makere. Kwa mbali nilisikia sauti ya nyimbo za dini nikidhani ni redio lakini kila niliposogea karibu niligundua kwa siyo redio bali ni sauti ya mtu anaimba tena akimsifu Mungu.

Nilibisha hodi na kukaribishwa na dada mmoja anayeitwa Mary Chacha. Huyu niligundua kuwa ni mjukuu wa bibi aliyezaliwa na mtoto wake wa kike kwa jina la Lusina John Maina anayefanya kazi mjini Moshi katika Idara ya Mahakama. Huyu ndiye anayemhudumia bibi huyu kwa kumpikia na kufanya usafi wa nyumba. Nilimfuata mhusika Bibi Pelagia John Maina na kunikaribisha ndani kwa tabasamu. Nilikutana na tabasamu la Bibi Pelagia Maina mwenye umri wa miaka 101.

Baada ya kuniona, Pelagia anaacha kuimba na kuitikia salamu yangu na kunikaribisha nikae nami nakubali na kumweleza shida iliyonifanya nimtembelee. Kwanza alishangaa na kuniuliza,“Nani kakuambia kuwa mimi naishi hapa na nina umri mkubwa?” Nilimweleza kuwa ni jukumu langu kuwatembelea watu wa aina mbalimbali.

Akizungumza maneno machache Pelagia, ananieleza kuwa amezaliwa mwaka 1914 wakati Vita Kuu ya Kwanza huko Marangu Kyala, Moshi Vijijini. Baba yake alikuwa Mzee Kipasika Mamiro na mama yake akiitwa Msengutze. Kwa bahati mbaya hakumbuki majina yao ya ubatizo ilipoanza na kubatizwa mwaka 1924 akiwa na miaka 10.

Baada ya hapo alisoma shule ya msingi ya Kilema Misheni. Hii ni misheni ya kwanza ya Kanisa Katoliki katika Jimbo la Moshi. Ilianzishwa na mapadri kutoka Ufaransa mmoja wao akiitwa Padre Tetsie. Aliolewa na Mzee John Maina mwaka 1935 ambaye ni mtoto pekee wa mke wa Maina aliyeitwa Kisaro.

Bibi Pelagia alibahatika kulelewa na Bibi Kisaro mama mkwe wake lakini Mzee Maina baba mkwe wake alikuwa ameshafariki dunia tangu mwaka 1922. Alipoolewa mwaka 1935 alikuwa na umri wa miaka 20 na kufanikiwa kuzaa watoto tisa.

Pelagia akiwa mama wa nyumbani anasema jambo kubwa katika maisha yake ni kufanya kazi na muda wote alikuwa akitegemea kilimo cha mahindi na maharage lillikuwa katika maeneo ya tambarare karibu na mji mdogo wa Himo. Kilimo hiki kilikuwa ni cha wakati wa mvua za masika Machi hadi Mei.

Kilimo cha vuli kilikuwa ni wakati wa Oktoba hadi Desemba. Pamoja na kilimo hiki cha mahindi na maharagwe, alikuwa pia akishughulikia kilimo cha kahawa ambalo lilikuwa ni zao la biashara na migomba kwa ajili ya chakula pamoja na kufuga ng’ombe, mbuzi na kondoo. Kahawa na migomba ni mazao ya kuduma kwa hiyo palizi ilikuwa ni kazi ya muda wote.

Kwa hiyo wakati wote alikuwa anajishughulisha na kazi na mapumziko pekee ni siku za Jumapili ambazo ni za ibada. Alikuwa anapinga sana uvivu na hakupenda kuona mtu yeyote anakaa bila kazi. Tabia hii ya kufanya kazi ameirithi kutoka kwa mama yake na amewarithisha watoto wake.

Watoto

Kama alivyoeleza hapo awali, Bibi Pelagia amejaliwa watoto tisa; wanne wa kiume na watano wa kike.

Kati ya hao walio hai ni wanne; wawili wa kiume na wawili wa kike. Kwa majina mtoto wake wa kwanza ni Jaji William John Maina ambaye amewahi kuwa Katibu wa Bunge na Mkurugenzi wa Uchaguzi, Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda za Dodoma, Mtwara na Dar es Salaam.

Pia amekuwa ni mwanzilishi wa Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma kwa kipindi cha miaka kumi na baadaye mjumbe wa Tume ya Kurekebisha ya Sheria na mjumbe wa kufuatilia msongamano katika Magereza.

Sasa amestaafu. Mwingine ni Stephen John Maina mwalimu mstaafu aliyewahi kuwa mwalimu wa shule za sekondari na vyuo vya ualimu, mratibu wa uandishi wa vitabu katika mradi wa UNESCO/UNDP Mpango wa Kisomo Mwanza, Katibu Mtendaj wa Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA), Mratibu wa lugha ya Kiingereza kwa walimu wa shule za sekondari na vyuo vya ualimu chini ya ufadhili wa Shirika la British Council, mratibu wa asasi ya elimu, Tanzania Education Network (TEN/MET) na mwanzilishi wa asasi ya kiraia ijulikanayo kama RESTE inayojishughulisha na ufundishaji wa Kiswahili na utamaduni wa Kiafrika kwa wageni. Kwa upande wa watoto wa kike, mmoja ni Rose John Maina ambaye ni mjasiriamali na mama wa nyumbani. Wa pili ni Lucina John Maina ambaye ni mfanyakazi katika Idara ya Mahakama, Mahakama ya Wilaya, Moshi.

“Nini siri ya kuishi miaka mingi”

Bibi Pelagia anasema anaamini maisha anayoishi duniani ni zawadi aliyopewa na Mungu kutokana na yeye kuishi maisha ya kumtukuza na kumtumikia Mungu lakini pia mfumo wa maisha yake ya kupenda kufanya kazi na kujishughulisha bila kuchoka. Pia kula vyakula vya kurutubisha mwili cha kuongeza nguvu. Anapendelea kula vyakula vya asili kama vile vinavyotengenezwa na ndizi, maharagwe, kunde, magimbi.

Matumizi ya chumvi yalipokuja alikuwa bado mdogo kwani hapo awali walikuwa wakitumia magadi (mbala) na ikati kupikia. Vyakula vingine anavyopenda ni mtori, kitawa na ng’ande.

Hivi ni vyakula laini vilivyopondwapondwa na kuwekwa supu au maziwa. Kwa bahati mbaya ugali ni chakula kilicholetwa na wageni na wenyeji wa Moshi hawana utamaduni wa kula ugali labda kwa siku hizi baada ya Wachagga kusafiri nje ya maeneo yao na kukutana na utamaduni huu. Hivi sasa ugali ni chakula cha kawaida sana Moshi.

Anasema dunia ya sasa siyo kama ya zamani kwani maisha yamebadilika sana siku hizi. Vijana wamemsahau Mungu na ndiyo maana magonjwa ya ajabu ajabu yamejitokeza na yanaongezeka kila siku.

Hii ni adhabu tunayopata kwa kumsahau Mungu. Maradhi kama kansa, kisukari, shinikizo la damu na hata magonjwa ya moyo yalikuwa ni adimu sana kuwepo miongoni mwa watu wakati wa ujana wake.
 
Wapo wengi sana huko vijijini.. Tembelea Uru nenda Old Moshi, Kilema, kirua, Mamba mpaka rombo ndani ndani huko utakuta wazee wengine wamegonga hata 120 na bado wanadunda
 
Hawa ukisema uwatoe kijijini awapeleke sehemu ya kunyoosha miguu bila kufanya vikazi vyao wanavyofanyaga unawamaliza Mara moja..

.Mungu ni waajabu kwelikweli..
 
Nina bibi yangu huyo ni marehemu kwa sasa yeye alifikisha miaka 103 ,anaona vizuri ,ana meno karibia yote ya chini na juu ,anatembea vizuri ,shida ilikua akichukuliwa ama na watoto wake au vijukuu ama vitukuu kukaa mjini ,anaweza kukaa siku moja ya pili utasikia ng'ombe wangu watakua wanaumwa nirudisheni kijijini kwangu hapo hakuna ubishi atarudishwa tu haijalishi mmetumia gharama gani

R.I.P Bibi
 
Nina bibi yangu huyo ni marehemu kwa sasa yeye alifikisha miaka 103 ,anaona vizuri ,ana meno karibia yote ya chini na juu ,anatembea vizuri ,shida ilikua akichukuliwa ama na watoto wake au vijukuu ama vitukuu kukaa mjini ,anaweza kukaa siku moja ya pili utasikia ng'ombe wangu watakua wanaumwa nirudisheni kijijini kwangu hapo hakuna ubishi atarudishwa tu haijalishi mmetumia gharama gani

R.I.P Bibi
Hahahahahaa basi huyo atakua pacha na bibi yangu awali alikua anasumbua tumpeleke mjini tukampeleka mjini hajamaliza hata siku tatu akasema nirudisheni nyumbani mara moja lasivyo nawataka ng'ombe wangu wote kesho asubuhi hapa yaan tulisarenda ilibidi apelekwe mapema sana.
 
Hahahahahaa basi huyo atakua pacha na bibi yangu awali alikua anasumbua tumpeleke mjini tukampeleka mjini hajamaliza hata siku tatu akasema nirudisheni nyumbani mara moja lasivyo nawataka ng'ombe wangu wote kesho asubuhi hapa yaan tulisarenda ilibidi apelekwe mapema sana.
Hahahah hawa wazee bana ila mimi nilifurahi sana kuwa na bibi ,babu zangu wote sikuwakuta hai ,natamani ningepata kuwa na babu aisee nijue upande wao wakoje
 
Hahahahahaa basi huyo atakua pacha na bibi yangu awali alikua anasumbua tumpeleke mjini tukampeleka mjini hajamaliza hata siku tatu akasema nirudisheni nyumbani mara moja lasivyo nawataka ng'ombe wangu wote kesho asubuhi hapa yaan tulisarenda ilibidi apelekwe mapema sana.
Kiukweli ni mabibi/mababu wa Enzi hizo wote hawataki kusikia kabisa maisha tegemezi ya kuletewa kila kitu. Tofauti na vijana wa siku hizi si wanawake wala wanaume wote wanataka kulelewa tu.
 
sijui kwanini wanaume wanakufa mapema hivyo aisee, asilimia kubwa ya wazee wote ni wakina mama na umri wao ni wa maana . namkumbuka bibi yangu ni wa 1915 mumewe alifariki. kingine wakifiwa na waume zao hata kama walikua bado mabinti hawaolewi tena
 
Nina bibi yangu huyo ni marehemu kwa sasa yeye alifikisha miaka 103 ,anaona vizuri ,ana meno karibia yote ya chini na juu ,anatembea vizuri ,shida ilikua akichukuliwa ama na watoto wake au vijukuu ama vitukuu kukaa mjini ,anaweza kukaa siku moja ya pili utasikia ng'ombe wangu watakua wanaumwa nirudisheni kijijini kwangu hapo hakuna ubishi atarudishwa tu haijalishi mmetumia gharama gani

R.I.P Bibi
Huyo bibi yako asije akawa ndo shangazi yangu aliyekuwa akiishi Kwimba! Naye alifariki akiwa na miaka 103 mzima wa afya yake kabisa! Alikuwa hataki kabisa kukaa mbali na ng'ombe wake! Aliacha uzao wa watu zaidi ya 300! R.I.P shangazi yangu Mpejiwa!
 
bibi yangu alifariki na miaka 118 alikua anashida ya kutembea, ila mpaka amefariki anasoma bibilia bila msaada wa miwani.
R. I. P
 
Huyo bibi yako asije akawa ndo shangazi yangu aliyekuwa akiishi Kwimba! Naye alifariki akiwa na miaka 103 mzima wa afya yake kabisa! Alikuwa hataki kabisa kukaa mbali na ng'ombe wake! Aliacha uzao wa watu zaidi ya 300! R.I.P shangazi yangu Mpejiwa!
Hahahaha aisee huyu mwenyewe uzao wake ni hatari ,zamani wakiwa mabinti walikua wanaitwa wanawake wa tofali ndio stori alizokua ananipa yaani wengi wenye miaka kuanzia 90 na kuendelea kizazi chao kilikua cha kazi hasa ,mimi bibi yangu ni wa Arusha ,ila naona tabia zao zilikua zinafanana

Watoto wake tu wa kuwazaa wako 12

Acha sasa bibi ana dada yake huyo nadhani alikua na miaka 110 hivi alikuta kobe anakula maindi yake akawa eti anampasua na shoka yaani ni vituko tu,huyu alizeeka akapinda kama upinde lakini anatembea na fimbo yake
 
Back
Top Bottom