ChikoTz
Member
- Feb 26, 2019
- 37
- 33
Simulizi: SALHAT
Sehemu: 03
Mtunzi: Salma Rashid
Ni baada ya Samia kuhitaji kurudi nyumbani kwao na mwanaye Salhat.
***** ******* ***
" itabidi tumzike Kwani hatutaweza kusubiri siku nyingne zaidi!! Aliongea shehe ambaye aliamuru maiti ya Naseeb ichukuliwe na kuanza kufanyiwa utaratibu wa mazishi.
Mr Matata ndye ambaye alishindwa kuelewa mtoto wa mwanaye Yuko wapi sasa!! Kwani tayri alishamtafuta bila mafanikio yoyote, alishindwa kuizuia maiti ya mwanaye isizikwe Kwani hakuwa na lakufanya tena.
"Abdul nakuahidi mwanangu nitamtafuta Mtoto wako na nitamlelea mimi" aliongea huku akitizama nguo za Salhat na baadhi ya vitu vilivyoletwa baada ya kupatikana katika nyumba waliyokuwa wakiishi.
Badra alitizama kwa hasira sana Kwani kila kitu sasa katika jumba lile kubwa la kifahara lilitawaliwa na Salhat pasina uwepo wake.
Aliingia ndani ya chumba chake na kutizama chumba kuzima hakukuwa na Mtu alitoa kijiti ndani ya kabati lake na kukupiga mlangoni kisha akapotea katika hali ya kutatanisha sana.
Alitokea katikati ya msitu ambao miti yake majani yake yalikuwa vichwa vya watu huku ardhi yake ikitawaliwa na mifupa ya binadamu, mito yake ikiwa inatiririsha damu kwa wingi pasina kukoma alipofika mtoni hapo pembeni yake kulikuwa na kiganja cha mkono wa Mtu ambapo alikichukua na kukitekea damu ile kisha kuinywa na baada ya hapo alipotea tena na kutokea sehemu nyingne.
Huko alikotokea sasa kulitawaliwa na nyoka kila mahali waliokuwa wazima wakipisha katikati ya miguu yake na wengine wakimpanda.
Kitendo hicho hakikuweza kumtishia Kwani tayri alishawazoea na huwa anakuja kila Mara anapohitaji msaada zaidi. Alitembea hadi kufikia Mti mmoja ulioko pekee yake na uliochongoka kisha kutoa shepu ya mlango alipofika hapo aliinama na kuingia ndani hatimaye Mti ule ulijifunga na hakukuwa tena na alama yoyote ya mlango wala Mti wowote pale.
Alitokea sehemu nyingne akiwa tayri ameshavalia mavazi meusi yani akiwa amejifunga kaniki ambayo ilianzia kifuani na kuishia juu ya magoti yake cheni zilizoweza kubebana ndani ya shingo yake pamoja na bangili zenye rangi nyeusi huku akisindikizwa na ngozi yenye rangi nyeusi miguuni mwake na kuonekana kama vikuku ndan ya miguu yake yote miwili.
Alitembea kwa hatua kadhaa baada ya hapo alifika mahali na kupiga magoti.
"Nimewasili eeee malikia wa kuzimu wa ukoo wetu wa Abandandi Alizungumza kwa heshima Kubwa sana huku akiwa amekiinamisha kichwa chake.
"Nimepokea heshima yako Mtoto wa malikia wa kuzimu wa ukoo wa Abandandi" alijibu mwanamk Yule ambaye aligeuka na kuweza kuonekana sura yake ikiwa ya kutisha na kustaajabisha Kwani ilikuwa imejaa mabaka ya nyoka na macho makali sana yenye kuwaka mithili ya pakaa.
"Razzio kwanini mpka sasa umeshindw kumuuwa yule adui yetu kwann mpaka sasa Yuko hai!!!?? Aliuliza malikia wa kuzimu.
"Nisamehe malikia wangu, ila nilijitahidi kwa kila mbinu ikashindikana Kwani kwa mbinu za kishetani hatumuwezi hata za kibinadamu pia ziligonga mwamba" aliongea Badra ambaye jina lake la kuzimu ni Razzio.
"Tulikupeleka duniani mapema kwaajili ya kuidhibiti nyota ya Naseeb ambayo ingeweza kumleta mshindani mkubwa katika ukoo huu wa Abandandi, tulitumia nguvu zetu nyingi kukupeleka duniani na kukupa sura ya kibinadamu kwaajili ya kumuulia mbali Naseeb lakini ulishindwa kutokana na upumbavu wako wa kumpenda binadamu, tukakupa sharti la kulala naye ili umchafulie nyota yake hilo nalo ulishindwa na ukaishia kulala na baba yake ambaye hana faida kwetu. Pia ukashindwa zuia asikutane na msichana ambaye anatoka koo pinzani na sisi na hatimaye wakampata Mtoto atakayekuwa tishio kwa ukoo wetu sasa hata huyo mtt kummaliza umeshindwaaa!!!!, alizungumza kwa kueleza na kwa hasira zaidi malikia huyo wa kuzimu.
"Kama kazi imekushindana sasa nitaenda mimi mwenyewe duniani kwaajili ya kupambana naye" alizungumza na kusimama juu yake chake na hapo ndipo tulipogundua ya kuwa hakuwa na miguu ya kawaida Bali miguu ya mikono ya wanadamu.
***** ****** *****
Tukirudi duniani Mwili wa Badra ulikuwa uko kitandani tu pasina kujigusa wala kufanya chochote kwasababu nafsi yake tayri iisharudi kuzimu na alipatiwa adhabu baada ya kushindw kufanya kazi aliyopewa na mama yake.
***** ***** *****
Samia aliwaaga na kuamua kuondoka.
"Sasa lakini utawezaje kutoka hapa watu wamejaa kila mahali wakikutafuta wewe na nihatari sana" aliongea Joseph.
"Sasa tutamsaidiaje mume wangu?? Aliuliza mkewe Lidia.
Samia alitabasamu na kuwatizama kisha akayazungumza haya yafuatayo.
"Hakuna Mtu atakayekuwa na uwezo wa kuniona kama mimi sijataka yeye anione labda mpaka awe na imani Kali sana"
"Unamanisha nini?? Aliuliza Lidia.
"Mimi siyo binadamu!! Alizungumza na hapo hapo alijibadilisha katika umbile lake la kijini.
Alivaliaa gauni jeupe ndefu mpaka chini taji lililoweza kurembwa na mauwa ya kila rangi likiwa limezunguka nywele zake ndefu zilizokuwa kichwani mwake na kujiachia mpka kufika makalioni mwake uso wake ulioweza kurembeka kwa nakshi nakshi za Mtoto wa kike na harufu Kali ya marashi iliyoweza kupenya katikati ya tundu zao mbili za pua baina ya Lidia na Joseph.
Walibaki wakimtizama na kushindwa kuelewa ni kipi kinatokea mbele ya macho yako.
Ni kweli Samia hakuwa binadamu Bali ni Jini aliyeweza kutoka katika ukoo wa Sultan Shariphu baada ya kumpenda Naseeb na kuamua kuishi naye maisha ya kawaida kama waishivyo binadamu wengine.
**** ***** ***** ****
Katika kitu ambacho kilimshangaza Mr matata ni picha za Samia Kwani ziliweza kuonekana kwenye simu tu lakini alipotaka zitolewe katika majarida kwaajili ya kuandika matangazo ya kuwa anatafutwa hazikuweza kutoka kabisa.
"Kwanini iwe hivi alijiuliza wakati huo akiwa hospitalini na akiwa amekaa pembeni kabisa ya Badra ambaye hakuwa yeye Bali mwili tu alioutumia pindi anapokuwa duniani.
Hapo hapo dactar aliingia jina lake aliitwa Hassan huyu alikuwa dactari bingwa sana na alijulikana Africa nzima kutokana na kazi zake za kuweza kufanya operation pasina Mtu yoyote aliyemfanyia operation kupoteza maisha.
"Ammmnhhh Mr matata najaribu kulitizama ni lipi tatizo la mkeo lakini nimeshindwa kugundua Kwani tumepima vipimo vyote na hatujaona sehemu yoyote yenye tatizo Kwani blood pressure yake iko normal, mapigo yake ya moyo yako kawaida tu presha pia iko kiasi, labda nahisi kafaint kutokana na mawazo yake kuwa mengi ila atarejea katika hali yake ya kawaida baada ya kurelax hivyo ungeweza kumpeleka tu nyumbni kwaajili ya kuendelea kupumzika zaidi aliyatoa maelezo hayo na kumpatia Mr matata.
"Sawa docta Hassan nakushukuru lakini kuna jmbo lingne linaniumiza kichwa sana ni kuhusu hii picha aliitoa simu na kumuonyeshea picha ya Samia.
"Nashangaa kwanini haitaki kutoka ndani ya hii simu ikiwa na hali hii hii Mara ukiweka katika laptop utaona picha zote hizi zake hutoziona nikitaka itoke katika majarida picha zake hazionekani vizuri hili nalo litakuwa tatizo gani ???!! Aliuliza baada ya kuhisi hilo nalo laweza kujibiwa na docta Hasan.
Dr alizitazama zile picha kisha akamtizama Mr matata ambaye alionyesha anahamu kubwa kulisikia jibu lake.
"Kwa kweli sijui" alijibu tu kwa ufupi kisha akamwambia.
"Mr matata nafikiri hata wewe hali yako siyo nzuri basi naomba nikufanyie vipimo kidogo" alizungumza Dr Hasan baada ya kuona ya kuwa Mr matata anachokizungumza hakiwezi kuwa ni cha kweli. Ila alizungumza ukweli mtupu na picha hizo za Samia alibahatika kuziona yeye mwenyewe tu ila watu wengne waliona ni peusi tu hivyo walifikiri ya kuwa mzee huyo anaanza kuwa kichaa.
**** ***** ***
Samia akiwa na mwanaye na kuelekea ngomeni kama alivyosema alianza kuona miti mingi ikicheza huku upepo mkali ukivuma.
"Jitokezee, sipendi kupigana Vita vya mafichonimekwambia jitokeze"
Ghafla ulisikika mlio wa Mtu kutua nyuma ya mgongo wake na hapo Samia taratibu kabisa alianza kugeuza shingo yake na kutaka kujua ni nani huyo"
Je kipi kitafuta!!, na unafikiri ni nani aliyoko nyuma ya Samia don't miss it
CHANZO
bongosimulizi.com