Simulizi: Penzi zito

Simulizi: Penzi zito

Casuist

JF-Expert Member
Joined
Jul 23, 2014
Posts
1,189
Reaction score
2,971
SIMULIZI: PENZI ZITO
MTUNZI: Prosper Mgowe


SEHEMU YA KWANZA

Alikuwa akitoka shuleni kuelekea nyumbani kwao. Alikuwa na mawazo mengi juu ya masomo pamoja na maisha yake hakuelewa ni kwanini toka asubuhi ya siku hiyo alikuwa akitafakari juu ya jambo hilo.

Akiwa tayari amekwisha yaacha mazingira ya Shule, Ghafla mawazo yake yalikatishwa na sauti iliyotokea nyuma yake "Bryan …….Bryan". Ilikuwa ni sauti ya kike lakini ilikuwa vigumu kwake kuitambua, inawezekana ni kwa sababu ya mawazo aliyokuwa nayo. Lakini hiyo sauti kwake haikuwa ngeni, Aligeuza shingo taratibu ili kuona ni nani aliyemuita, alikuwa ni Mercy aliyemuita. Bryan alimsubiri kando kidogo ya njia. " Mambo vipi Bryan? Mercy alianza kwa kumsabahi Bryan" Ah safi tu" alijibu Bryan.

"Mbona leo uko hivyo? Aliuliza Mercy. Badala ya kujibu alinyamaza kwa sekunde kadhaa kasha naye akamuuliza kwani nikoje? Nakuona kama una mawazo mengi au naogopa? Hapana ni kweli siku ya leo siko kawaida, Sasa unawaza nini Bryan ili hali wewe bado mwanafunzi? Nawaza maisha Mercy " Kwa nini unasema hivyo wakati wewe bado mwanafunzi tena ndio kwanza uko kidato cha pili" Nina haki ya kuwaza hivyo kwa sababu sina hakika kama nitaendelea na shule mpaka mwisho. "He! Hebu acha utani wako Bryan" Mercy alisema huku akionyesha kutoamini Bryan kwa kile alichokiongea.

Ni kweli Mercy kwa sababu maisha ya nyumbani kwetu ni magumu mno, Mama yangu hana kipato cha kutosha kuweza kuniendeleza na masomo yangu ya Sekondari na isitoshe hana karo ya term hii kuipata kwake kwenyewe ilikuwa shida, yaani mpaka mama auze mandazi,vijisenti atakavyodunduliza ndio aniwekee kwa ajili ya karo, hapo bado nyumbani hatujala wala hatujavaa. Na isitoshe safari hii ngano imepanda bei na mama yangu hata hela ya mtaji hajafikisha, Yaani hata sielewi tutaishije maisha haya.

Bryan alijaribu kumuelezea Mercy maisha ya kwao kwa uchungu mwingi mno. Muda wote huo Mercy alikuwa akimsikiliza Bryan kwa makini huruma ilimjaa ila hakuelewa ni vipi angemsaidia Bryan.

"Bryan" Mercy aliita "Ndio nakusikiliza unasemaje aliita na kuuliza.
"kuna kitu kimoja naomba nikuulize kama hutojali" "hakuna shida we uliza tu"
"Hivi bana yako alishafariki au bado yupo hai? Bryan alinyamaza kama sekunde kadhaa kisha akaguna "Duh" ni story ndefu sana lakini nitakueleza kwa ufupi tu. "Hakuna shida kwani shida yangu ni kutaka kujua kuhusu hilo tu.

Lakini kabla hata Bryan hajaanza kumsimulia Mercy juu ya Baba yake walikuwa tayari wamefika kwenye kituo cha daladala.

"Oya nyie madent hamuendi?Sauti ya konda iliwashitua .
"Mercy twende tupande hii" Bryan alimwambia Mercy. Hapana ngoja kwanza mpakatumalize maongezi yetu Bryan alikubali na kumruhusu konda waende.

Mercy ni binti wa pekee katika familia ya Mzee Josephat. Familia hiyo ilikuwa na watoto wa nne, wa kwanza Irene na wa pili Jacobo akifuatiwa na Isack na kitindamimba ambaye ni Mercy. Hawa wote walikuwa na maisha mazuri kwa sababu wote walikuwa na Elimu nzuri na kila mmoja alikuwa anakazi yake kasoro Mercy ambae alikuwa bado anasoma ndo kwanza yupo kidato cha pili.

Mzee Josephati pamoja na Mkewe Mama Irene walijitahidi kumpatia Mercy kila hitaji ilimradi tu Binti yao asome kama ndugu zake.

Mercy na Bryan hawakuwa wakisoma darasa moja, Mercy alisoma kidato cha pili B, wakati Bryan alisoma kidato cha pili mkondo A .Lakini wote walikuwa kidato kimoja. Hawakuwa marafiki kiasi kwamba wakutane na kuanza kuongea zaidi ya dakika tano,hiyo haikuwahi kutokea. Ilikuwa kila walipokutana ni salamu na kila mtu anaendelea na shughuli zake.

Toka siku nyingi Mercy alikuwa akimpenda Bryan lakini tatizo lilikuwa likimtatiza ni vipi ataweza kumueleza Bryan anavyojisikia juu yake.Alihofia kuwa baada ya kumueleza Bryan jinsi anavyojisikia juu yake angeonekana kuwa yeye Malaya, Lakini alijiapiza ipo siku lazima angemtobolea.

Wakati Mama yuko kidato cha nne alipewa namba na mvulana mmoja aliyekuwa anasoma Chuo Kikuu Dar –es-salaam aliitwa Enock Mwansasu.Mama yangu alifukuzwa Shule baada ya kugundulika kuwa ni Mjamzito.Baada ya kufukuzwa Shule Mama alimuendea yule Mwanaume aliye mpa Mimba na kumueleza kuwa ana mamba yake.

Yule Mwanaume ambaye ndio Baba yangu alikubali ile Mimba na kuhaidi kuwa atamtunza yeye na kiumbe kilichokuwa Tumboni. Baba aliendelea kumtunza Mama na kumtimizia kila hitaji ambalo mama alihitaji mpaka nilipozaliwa mimi. Baadaye baba alihitajika aende Urusi kwa Masomo yake kwa kipindi cha miaka mitano, Lakini Baba alimuomba Mama asijali kwani safari sio kifo, kwa hiyo ipo siku atarudi kama Mungu akijalia basi watafunga ndoa. Kwahiyo waliagana na kila mmoja akiwa na majonzi ya kumkosa mwenziwe kila mmoja alionyesha kuwa ana penzi la dhati kwa mwenziwe. Baada ya hapo Baba alisafiri na kwenda nje kusoma.
Huku nyuma Mama aliendelea kutumiwa misaada mbalimbali na baba.Hali hiyo iliendelea takribani miezi sita (6) halafu hali hiyo ikakatika ghafla, kukawa hakuna msaada wala msaidizi. Mama kuona hivyo akaamua kufungua genge kwa akiba ndogo aliyokuwa nayo. Hilo banda ndio lilimsukuma mpaka akajenga nyumba ndogo ya udongo yenye vyumba viwili na sebule na hilohilo banda limenisomesha shule.

Tuliendelea kuishi hivyo na Mama yangu huku tukiwa tumepoteza matumaini ya kumuona Baba katika maisha yetu.
Ilipofika mwaka 1994 tulivamiwa na wezi wakavunja nyumba yetu pamoja na genge letu wakachukua kila kitu walichokiona kuwa kwao ni cha thamani na kasha wakatokomea.

Hali hiyo ilimlazimu Mama yangu awe omba omba tuliendelea kuishi kwa kazi hiyo mpaka Mama alipopata mtaji wa kuanzisha biashara yake ya maandazi ambayo mpaka sasa ndiyo inatusaidia. Na sasa hivi ninavyoongea na wewe Mama yangu ni Mgonjwa sana na mimi peke ndio tegemeo lake sijui nitafanya nini.

Bryan alipomaliza kusema hayo macho yake yalilengwalengwa na machozi. Na kwa upande wa Mercy yeye uso wake uliingiliwa na simanzi kuu. "Pole sana Bryan kwa matatizo hayo".Alisema Mercy kwa upole huku akimtazama Bryan machoni. "Asante japo sijapoa". "Usijali sana Bryan kwani Mungu hamtupi mja wake"Mercy alijitaidi kumfariji Bryan.

Maneno yale kidogo yalimtia nguvu Bryan, Muda ulikuwa umekwenda sana kwa hiyo wote wakakubaliana wapande Hice lakini kabla ya kupanda kwenye daladala Mercy alitoa noti ya shilingi Elfu mbili na kumpatia Bryan. Nashukuru sana Mercy kwa wema wako naomba Mungu akuongezee. "Usijali Bryan" Alisema Mercy huku akitabasamu.

Mercy na Wazazi wake walikuwa wakiishi mtaa wa Area D Mkoani Dodoma na Bryan alikuwa akiishi katika mtaa wa Chadulu katika Mkoa huohuo.
Daladala ilipofika njia panda area D Bryan alimuaga Mercy na kuteremka kuelekea kwao. Moyo wake ulikuwa ukimuenda kasi ambavyo si kawaida yake.
"Hivi kwa nini moyo wangu uko hivi? Mh Sio bure huko nyumbani lazima kutakuwa na jambo"Aliwaza Bryan na kuanza kuongeza ukubwa wa hatua. Alipofika hatua chache kabla ya kufika kwao alisikia kelele. "Jamani majirani naombeni msaada."Alikuwa ni mama wa Makamo alikuwa ni jirani yao Mama Musa. Alionekana akitokea upande wa Maliwatoni kwa akina Bryan huku akiwa anamkokota mtu. Mtu huyo alionekana amelegea mno na mdomo wake ukiwa wazi huku povu jingi likimtoka.

Alionekana anahema kwa taabu sana. Mtu aliyekokotwa hakuwa mwingine bali ni Bi Sara ambaye alikuwa ndiye Mama yake Bryan. Bryan alishituka sana alipomuona Mama yake yupo katika hali ile. Akaanza kukimbilia kule aliko Mama Musa na Mama ili kufahamu kumetokea nini.
"Hah Mama amekuwaje? Bryan alishitukiaamemuuliza Mama yake swali hilo bila kujali hali aliyokuwa nayo.
"Fanya haraka kaite Taksi" Alisema Mama Musa huku akiwa anaendelea kumkokota Bi Sara kuelekea kiliko kituo cha taksi.
Bryan hakuuliza swali zaidi alitoka pale mbio kuelekea kwenye kituo ch Taksi.Ulikuwa ni mwendo wa dakika. Ulikuwa mwendo wa dakika tano kutoka kwao mpaka kituo cha taksi.

Huku nyuma wakina mama wajirani walishakwishafika kumsaidia Mama Musa.Baada ya muda mfupi taksi ilifunga breki miguuni kwao kwa kundi la wakina mama "Tufikishe General" Alisema Mama Musa huku akifungua mlango wa wa siti ya nyuma ya taksi alisaidiana na wakina mama wenzake kumpakia ndani ya taksi.Bryan alikaa siti ya mbele.Mma Musa na jirani yake Mama Rashidi pamoja na Mgonjwa Bi sara wlikaa nyuma. Na safari yakwenda hospitali ikaanza. "Jikaze bwana wewe ni mtoto wa kiume"Alisema Dereva walipokuwa njiani, baada ya kumuona Bryan analia. Bryan hakujibu zaidi ya kuendelea kulia kilio cha kwikwi.

Mama Bryan alikuwa mgonjwa takribani wiki sasa. Japo hakuwa serious sana alikuwa ansumbuliwa na BP pamoja na Athima.
Siku moja akiwa ndani amejipumzisha akaja jirani yake mama Musa kumtakia hali, "Haya wajionaje leo mama Bryan" Mama Musa alianza kwa kumsabahi jirani yake.

"Namshukuru jalia leo ahueni" alimjibu mama Bryan. Waliendelea na maongezi kwa muda kama robo saa. Baadae Mama Bryan alimtaka radhi mama Musa kuwa anaomba amsubiri kwa nukta chache anaenda chooni mara moja. Naomba nikusindikize kwa sababu siamini kama utajiweza" Alisema mama Musa. "Usijali nitajikongoja"Alijibu mama Bryan. Mama Musa alimuacha mama Bryan aende peke yake japokuwa alikuwa hamuamini sana hali yake.

Baada ya Mama Bryan kutoka nje kwa kulegalega hukunyuma Mama Musa hisia zake zikawa hazimpi kabisa kuendelea kubaki mule sebuleni, akatoka nje na kusimama mlangoni. Zilipita dakika 5 bila Mama Bryan kutoka msalani. Baada ya dakika hizo kupita Mama Musa alisikia kishindo kutoka msalani kama mtu amedondoka vile.

Mama Musa aliuendea ule mlango wa choo kwa haraka na kusukuma kwa bahati nzuri ulikuwa umerudishiwa, ulipofunguliwa hakuamini kile alichokiona kwani Mama Bryan alikuwa ameanguka pembeni ya shimo la choo huku povu likimtoka mdomoni. Mama Musa alimuinua na kumbeba mpaka nje.

Ndani ya taksi wakielekea hospitali Mgonjwa alikuwa bado hajazinduka, kufika maeneo ya bunge Mama Musa na Mama Rashidi wakamuona mgonjwa kwa taabu anafumbua macho. Mioyoni mwao wakaanza kupata matumaini kuwa mgonjwa wao anapata ahueni katika siti ya mbele hakuna aliyeelewa kinachoendelea nyuma si Bryan wala Dereva.
Katika siti ya nyuma mambo yakawa sivyo na matarajio kwani Mama Bryan alianza kutupa miguu pamoja na mikono na baadaye akaanza kugeuzageuza macho halafu akajinyoosha na kisha kukakamaa.
Mama Musa alikuwa kaduwaa na Mama Rashidi kubung'aa wasijue cha kufanya.

Mzee Josephati na Mkewe Bi Maua walikuwa wamepumzika sebuleni wakiangalia TV na mara wakasikia hodi, "karibu mlango umeludishiwa tu" alijibu Bi maua na mara akaingia Mercy. Usoni mwake alivaa sura ya simanzi kana kwamba kulikuwa na msiba mkubwa mno.
"Shikamooni" aliwasalimu wazazi wake "Marahaba" waliitikia kwa pamoja. "Vipi huko utokapo ni kheri au shari"? Bi maua alimuuliza binti yake baada ya kugundua hayuko katika hali yake ya kawaida. "Heri tu mama" alijibu Mercy huku akijilazimisha kutabasamu.
Mama yake alielewa kuwa kuna tatizo linalomtatiza binti yake lakini hakutaka kumsonga sana kwa maswali alimuacha aende kwanza akapumzike.
Mercy alipoingia chumbani kwake alijitupa kitandani bila hata kubadili uniform hata kula chakula hakikukumbuka tena kwa kipindi hicho. Hiyo yote ilisababishwa na fikra juu ya Bryan ni jinsi gani ataweza kumsaidia?. Ni vipi ataweza kumtatulia matatizo yake aliyonayo na kumfanya aweze kuishi kwa furaha na ni vipi ajieleze mpaka aeleweke juu ya hisia zake kwa Bryan. Na si hivyo tu alikuwa anatamani siku iishe upesi akaonane na Bryan.

Dereva hakujua kilichotokea bali aliendelea kutereza akielekea hospitali.
Walipita getini na kuingia ndani kabisa hospitalini. Dereva alifunga breki na kufungua mlango wa upande wake alishuka na kasha akazunguka upande wa pili na kumfungulia Bryan.

Huku nyuma Mama Rashidi na Mama Musa walishuka na kumuomba dereva awasaidie kumbeba mgonjwa. Na Bryan naye bila kuambiwa alitaka kushiriki katika hatua hiyo. "Ah hapana Bryan we acha pumzika tu" Mama Rashidi alimkataza Bryan. "Kwanza shika hii mia tano ukale mgahawani kwa sababu toka utoke shule haujagusa chakula aliongea Mama Musa.

Bryan ikamlazimu aichukue ile hela japo kwa shingo upande. Lakini akili na mawazo yote ni juu ya mama yake ambaye kwa yeye anavyomfahamu ni Mgonjwa Mahututi alianza kutembea kwa hatua ndogondogo huku akiwa amenyong'onyea kuelekea kwenye mgahawa uliopo pembeni kidogo na hospitali ya General. Alipofika Mgahawani akaagiza chakula na badala ya kukila akawepo anakitazama utafikiri ndo kwanza anakiona.
Aliendelea kukitazama kile chakula takribani dakika tano kana kwamba kile chakula hakikuagiza yeye.

Mercy alikuwa ndani ya daladala akielekea Dodoma Sekondari shule ambayo alikuwa akisoma. Moyoni mwake alikuwa na furaha tele akiamini hiyo akiamini ni siku nyingine tena ya kwenda kuonana na Bryan. "Oya kuna anaeshuka hapa bohari"? ilikuwa ni sauti ya konda.
"Shusha" Mercy alijibu. Mercy alishuka na kumlipa konda nauli kisha akavuka barabara akielekea shuleni kwao.

Alipofika shule alikuta wenzake wametawanyika kutoka assembly kuelekea madarasani. Aliangaza macho yake huku na kule asijue wapi kwa kumpata Bryan. Baadaye akaamua kwenda darasani kwa akina Bryan ili kuuliza kama amekuja.

Alipofika darasani kwa akina Bryan alimuendea moja kwa moja rafiki yake Martha ambaye ni Monntress wa darasa hilo. "Sema shoga mambo vipi"? Mercy alimsabahi shoga yake huo. "Safi tu, issue vipi?" Martha alijibu na kuuliza, "Poa alijibu Mercy". "Bryan ameshafika?" "hapana naona leo kachelewa kidogo lakini atafika muda si mrefu" kwa maneno yale alinyong'onyea lakini alijipa moyo kuwa bado nukta chache Bryan angetokea kipindi kipindi cha kwanza kiliisha, hakuna Bryan kuonekana cha pili na hatimaye cha tatu Bryan hakutokea.

Mercy ilikuwa ni huzuni kubwa mno kwani alijihisi ni ni mpweke kuliko.Katika vipindi vyote hivyo vitatu hakuelewa somo hata moja na zaidi aliona walimu wote wanaofundisha ni kero kwake. Alijishangaa kwa nini Bryan amemuingia kiasi kile, ukizingatia Bryan mwenyewe hawana siku nyingi toka wazoeane. Alizikusanya daftari zilizokuwa juu ya meza yake na taratibu alinyanyuka kwenye kiti alichokuwa amekalia na taratibu akaulenga mlango wa kutokea kwenye ofisi ya walimu.

Alipoingia Ofisini alimkuta mwalimu wake wa darasa Mr Innocent "Morning Sir"
"Have a good day what's ya problem", "I'm not feel well I think this is Malaria" "So you want go to the hospital", "Yes Sir" Okay you may".

Alikula robo ya chakula kile kasha akalipa hela na kunyanyuka. Mapigo yake ya Moyo yalikuwa yakienda mbio mno. Mwendo wake ulikuwa wa haraka mno pindi alipotoka mgahawani hapo akielekea hospitalini.
Pengine ungemuona usingeweza kuelewa anatembea au ankimbia. Ilikuwa nusu kutembea nusu kukimbia akaingia hospitalini na moja kwa moja akaenda mapokezi. "Samahani dada sijui mgonjwa aliyeletwa muda mfupi kabla ya sasa sijui yupo sehemu gani? "Salamu kwanza kaka angu. Lakini usijali sana wameingia katika chumba cha docta" "Samahani kwa hilo dada angu, shukrani" Bryan alijibu na kuondoka kwa mwendo wake uleule kabla hajasukuma mlango wa docta, mlango huo ulifunguliwa na Mama Musa pamoja na Mama Rashidi walitoka ndani ya chumba hicho."Vipi?"Akina mama hao walimuuliza Bryan kwa pamoja.
Bryan kabla hajajibu aliwatazama wakina mama hao machoni kwa nucta kadhaa, Na kugundua macho yao yameiva na kuwa mekundu kuliko kawaida. Hivi ilimaanisha wametoka kulia muda si mrefu na hilo alilitambua na mara ghafla fikra zake zikaunda picha nyingine katika ubongo wake "Nataka kumuona mama yangu" alijibu Bryan huku mapigo yake ya moyo yakizidi kumuenda kasi.

***JE? Nini kitaendelea…..

Khantwe
davidson689 Toplady ram BPM Sangomwile Mamamercy jonnie_vincy mbalu byb sac mlyn VAN HEIST nrango mangimezamuuza ubuyu Jullie ZIgunga Mojaculbby mugaru
 
SIMULIZI: PENZI ZITO
MTUNZI: Prosper Mgowe.


SEHEMU YA PILI


Alikula robo ya chakula kile kisha akalipa hela na kunyanyuka. Mapigo yake ya Moyo yalikuwa yakienda mbio mno. Mwendo wake ulikuwa wa haraka mno pindi alipotoka mgahawani hapo akielekea hospitalini.
Pengine ungemuona usingeweza kuelewa anatembea au ankimbia. Ilikuwa nusu kutembea nusu kukimbia akaingia hospitalini na moja kwa moja akaenda mapokezi. "Samahani dada sijui mgonjwa aliyeletwa muda mfupi kabla ya sasa sijui yupo sehemu gani? "Salamu kwanza kaka angu. Lakini usijali sana wameingia katika chumba cha docta" "Samahani kwa hilo dada angu, shukrani" Bryan alijibu na kuondoka kwa mwendo wake uleule kabla hajasukuma mlango wa docta, mlango huo ulifunguliwa na Mama Musa pamoja na Mama Rashidi walitoka ndani ya chumba hicho."Vipi?"Akina mama hao walimuuliza Bryan kwa pamoja.
Bryan kabla hajajibu aliwatazama wakina mama hao machoni kwa nucta kadhaa, Na kugundua macho yao yameiva na kuwa mekundu kuliko kawaida. Hivi ilimaanisha wametoka kulia muda si mrefu na hilo alilitambua na mara ghafla fikra zake zikaunda picha nyingine katika ubongo wake "Nataka kumuona mama yangu" alijibu Bryan huku mapigo yake ya moyo yakizidi kumuenda kasi.

"Hebu ngoja kwanza Bryan" Mama Musa alimtuliza, "Ni ngoje vipi wakati nataka nimuone mama yangu? Bryan alijibu kwa sauti kali kiasi. "Tulia kwanza utamuona tu mama" Mama Rashidi naye alijitahidi kumbembeleza.
"Hivi kwa nini mnizuie na mama yangu amekwishafariki?" Bryan aliongea huku na yeye macho yake yakiwa yamemuiva na machozi yakimlengalenga hii ilimaanisha ana hakika na kitu anachokiongea. Kabla mama Musa na Mama Rashidi hawajajibu maswali ya Bryan yalikuwa yakija mfululizo, mlango wa chumba cha daktari ulifunguliwa na daktari akijitokea mlangoni.

Uso wake ulikuwa kama wa mtu aliyepoteza matumaini fulani. "Jamani akina mama "nasikitika kuwajulisha ya kuwa mgonjwa Bi Sara hatunae tena" Alipokuwa akizungumza hayo Doctor alikuwa amewaelekea akina mama Musa kumbe kwa nyuma yake kulikuwa na Bryan.
Kauli hiyo ya daktari ilipelekea kilio kikubwa kilichoanguliwa na mama Rashidi na mama Musa kwa upande wa Bryan alikuwa kama kapigwa na butwaa. Alijitahidi asiyaamini masikio yake lakini ukweli ukabaki palepale, mama yake alikuwa hawezi kuongea tena, hawezi akafumbua macho tena, roho iliisha achia mwili tayari alishafariki.

Alikuwa bado katika hali ya mshangao mkuu, mara kwa ghafla akaanguka na kupoteza fahamu. Mara wakaja manesi na kumbeba Bryan kwenda kumuhudumia. Maiti ya Bi. Sara ilipelekwa Mochwari. Baada ya hapo Mama Musa na Mama Rashidi waliondoka na kwenda kutoa taarifa kwa majirani wengine, ili taratibu za mazishi zianze kufanyika.

Katika wodi aliyokuwemo Bryan kwa mbali alianza kufumbua macho na baada ya kufumbua macho akaanza kuyafikicha mara tatu ili aweze kuona vizuri. Hakupaelewa vizuri mahali alipokuwepo, baada ya kuangalia vifaa vilivyokuwamo mule ndani akatambua kuwa yupo wodini.
"Iweje mpaka niwe sehemu hii"?

Hili ndio swali la kwanza lilimjia katika ubongo wake, ndipo hapo akaanza kuhangaika kuvuta kumbukumbu kwa kuunda baadhi ya matukio yaliokuwa yakimjia kichwani. Na kujikuta akipata mfululizo kamili wa tukio.

Huku akiwa katika lindi la mawazo mara mlango wa chumba alichokuwemo ukafunguliwa, akaingia nesi huku kachana tabasamu.
"Una jisikiaje kakangu? Nesi alimuuliza Bryan huku bado kaachia tabasamu.
"Sijambo" Bryan alijibu kwa kifupi bila kuongeza neno.
Hujisikii maumivu sehemu yeyote? Nesi aliendelea kumuuliza, "Hamna" Bryan alijibu.
"Basi pumzika kesho utarudi nyumbani" nesi alimwambia.

Bryan baada ya kujibu akaanza kulia huku akimtaja mama yake ama kwa hakika alileta simanzi mno. Nesi ikabidi afanye kazi ya ziada amfariji na kumtuliza., ilimchukuwa muda mrefu hadi Bryan kutulia na hata hivyo bado alikuwa analia kilio cha kwikwi.

"Usilie Bryan kichwa kitakuuma." Nesi alizidi kumtuliza zaidi.Bryan ilikuwa haimuingii kabisa kuwa mama yake hayuko tena duniani lakini ndo imeshatokea huna budi kukubaliana nayo. Imeandikwa na imeshatimia, kazi yake haina makosa, ameumba sasa katwaa.

Mercy alikuwa anashuka katika daladala katika kituo ambacho huwa anashukia Bryan. Lengo lake lilikuwa ni kufika kwa akina Bryan japokuwa hakuwahi kufika kabla.
"Eti anti samahani" Mercy alimwambia dada mmoja aliyekuwa akipishana naye njiani.
"Bila samahani" alijibu yule dada huku akimwangalia Mercy usoni kwa macho ya utafiti
"Sijui utakuwa unapafahamu kwa akina Bryan"? aliuliza Mercy.
"Yukoje huyo Bryan"?Aliuliza yule dada badala ya kujibu.
"Okey ni mwanafunzi wa Dom sekondari eeeh? "That's right ndiye huyo kwao ni wapi?
Nyoosha huo hapo uchochoro utatokezea Galax salon, halafu kunja kushoto, nyoosha hiyo njia utakayokutana nayo utahesabu nyumba nne zilizo upande wa kushoto nay a tano inamkungu nje basi ndio hapo utakuwa umefika.

"Asante sana dada yangu nashukuru kwa msaada wako" Mercy alishukuru.
"Hamna tabu, usijali mdogo wangu" Yule dada alijibu na kuanza kuendelea na safari zake. Naye Mercy akaendelea na safari yake.

Bryan alikuwa yumo ndani ya taksi ya jirani yao Baba Musa akielekea kwao, ambako ni yeye pekee aliyekuwa anasubiriwa ili amuage mama yake. Bryan alikuwa amelia mno kiasi kwamba macho yamevimba nab ado machozi yanatiririka, Bryan aliyafuta machozi lakini baada ya sekunde kadhaa machozi yalikuwa yakiteremka chini ya mashavu. Naye bila kukoma aliendelea kuyafuta akisaidiwa na dereva Baba Musa.

Akiwa anaendelea kufuta machozi kwa mbali Bryan alimuona mwanafunzi mwenye sare zinazofanana na shuleni kwao lakini katika mood nyingine kabisa lakini kadri alivyozidi kumsogelea ndivyo alivyozidi kumfananisha.

Bryan alimwomba Baba Musa akimfikia yule mwanafunzi anaomba asimame na ikibidi amchukue. Baba Musa akamjibu hakuna shida, lakini wakati huo anaposema maneno hayo hajamtambua aliye mbele ya upeo wa macho yao ni nani na ni kwanini asubuhi yote ile awepo mtaani anarandaranda.

Walimfikia Mercy na gari ikasimama pembeni kidogo ya Mercy.
"Binti ninaweza nikakufikisha? Aliuliza dereva,"Lakini sio mbali sana alijibu Mercy.

Bryan alisikia sauti ya Mercy akanyanyua uso wake ili kuhakikisha kama amdhaniaye ndiye. Bryan alikuwa halii tena isipokuwa macho yake yalikua mekundu mno na yalikuwa yamevimba.

"Aise kumbe ni wewe ingia twende" Bryan alimwambia Mercy kwa sauti yenye masikitiko.
"Wooow kumbe uko humu Bryan basi ngoja tuwe sote"Mercy alijibu kwa furaha kwa ajili amemuona Bryan akaingia ndani ya gari akakaa siti ya nyuma. Lakini ghafla furaha yake ikakata pindi alipomwangalia Bryan usoni kwa makini, Bryan alionekana mnyonge na mwenye majonzi huku wakiwa wanaendelea na safari Mercy uvumilivu ulimshinda na kuanza kumuuliza Bryan kulikoni. Bryan badala ya kujibu swali la Mercy aliangua kilio upya. Ndipo Baba Musa akaona ni vyema ajibu kwa niaba japo kwa kifupi.

Wakafika nyumbani kwa akina Bryan wote wakiwa wanalia yaani Mercy na Bryan kasoro Baba Musa baadhi ya waliokuwepo kilioni walimchukua Bryan na Mercy kuwapeleka ndani, ilikuwa ni muda kwa kuaga maiti. Bryan walikuwa wameongozana na Mercy katika mstari wa waagaji ilikuwa ni zamu la Bryan kuaga mwili wa marehemu mama yake.

Alipofikia jeneza alisimama kando ya mwili wa mama yake na kumuangalia kama dakika tatu hivi kama kwamba haamini kuwa yeye ndiye aliyelala ndani ya jeneza lakini hata hivyo ukweli ukabaki palepale majivu hayawezi kuwa mkaa. Aliondoka na kuwaacha watu wengine wauage mwili wa marehemu. Mercy naye ilifika zamu yake alimuangalia marehemu kwa umakini kisha akajikuta machozi yakimdondoka naye akasogea mbele kwa kupisha waagaji wengine.

Baada ya zoezi hilo kwisha msafara wa kwenda makaburini ulianza. Taratibu za mazishi zilienda kama zilivyopangwa.

Mpaka arobaini ilipokwisha matanga yaliinuliwa na watu kurudi makwao. Katika kipindi chote hicho Mercy alikuwa karibu mno na Bryan katika kumfariji na kumpa moyo, pamoja na hayo Mercy alimuhaidi Bryan kuwa atakuwa tayari kutoa msaada kwa kila atachohitaji.

"Mama kuna maongezi naomba tuongee endapo utapata nafasi" Mercy alimwambia mama yake wakati wanakula chakula cha mchana.
"Hakuna tabu mwanangu" mama yake akajibu walipomaliza mama yake alimuita bintiye Mercy sebuleni kwa ajili ya mazungumzo.

"Ehee kina tatizo gani tena? Mama yake alimuuliza huku akimtazama usoni". Hapana tatizo ila kuna kitu nataka nikueleze na ikibidi nitahitaji msaada wako."Enhee kitu gani ambacho unataka kuniambia" Mercy alitulia kimya kwa sekunde kadhaa kisha akakohoa kikohozi cha uwongo na kweli kisha akaanza kwa kusema.

Mama kuna kijana mmoja ni mwanafunzi mwenzangu ambaye tunasoma naye kidato cha pili ni rafiki yangu sana. Huwa ananisaidia katika masomo ambayo huwa na feli na ananiheshimu sana na mimi hivyohivyo yaani inshort tunaishi kama ndugu (kaka dada ).
"Huyo kijana anaitwa nani"? Mama yake alimkatiza, "Anaitwa Bryan" Mercy alijibu kwa utulivu. "enhee"maana yake aliashiria aendelee.
"Sasa huyo kijana anamatatizo makubwa mno" "Matatizo gani"Mama yake aliuliza kwa mshangao.

"Ni kwamba Bryan ni kijana mwenye maisha duni sana kiasi kwamba school fees yenyewe kulipa ni mgogoro, yaani mpaka afanye biashara zake pamoja na mama yake ndio wadundulize hiyo karo ya shule.Ameishi hivyo toka form one mpaka sasa form two, Uniform zenyewe zimesha chakaa yaani toka mwaka jana mpaka sasa ninavyoongea ndizo hizo alizonazo.

"Anaishi na nani?" Mama yake alimkatiza tena kwa kumuuliza swali.
"Alikuwa anaishi na mama yake" Na sasa?
"Mama yake amefariki wiki iliyopita" "Oooh masikini" mama yake alionekana kuingiwa na simanzi Mercy akaendelea, sasa tatizolinapofikia Bryan hana hata ndugu hapa Dodoma.

Baba yake je? "Baba yake alienda kusoma akiwa mdogo nje toka kitambo tena Bryan akiwa bado mdogo mpaka leo haifaamiki alipo.

"Okey nimeshakumbuka aliwahi kiniambia ana mjomba wake ambaye anaishi chang'ombe, ila huyo mjomba wake mwenyewe matatizo matupu yaani ye na pombe, pombe na yeye, yeye pombe kwake ndo kila kitu na maisha yake ni mara kumi na maisha ya akina Bryan. Naye anaishi hivyo hivyo kwa kuungaunga, ilimradi siku zinasogea.

" Sasa ombi langu kwako ni kwamba naomba umsaidie aje kukaa hapa nyumba halafu ile nyumba yao ataipangisha. Angalau umfanye houseboy itakuwa afadhali ilimradi utakuwa umemsaidia na ndio itakuwa nafuu yake kwani hakuna wakumpa msaada zaidi, mama naomba naiwe hivyo alimaliza Mercy.

Kwa sauti aliyokuwa anatumia Mercy na umakini aliokuwa nao katika kuongea vilimgusa sana mama yake Mrcy na mara ghafla ulimjia moyo wa kumsaidia kijana huyo japokuwa hakuwa akimfahamu.

"Sasa mwanangu nimekusikia na nimekuelewa vizuri sana". "sasa mama uwamuzi wako uko vipi katika swala hili"?

"Siwezi nikakupa jibu moja kwa moja mpaka nimueleze Baba yako kwa sababu yeye ndio kichwa cha familia tuone naye atalichukuliaje swala hili, lakini kwa upande wangu mimi sina neno yaani nimeridhia.

"Sawa mama naomba ujaribu kuongea na Baba mpaka akuelewe"
"Usijali nitamueleza na kesho nitakuambia ameamua nini"?
"Thank u mama Ilove u " "Thank u my doughter and me too"
Mercy alinyanyuka sehemu aliyokuwa amekaa na kuelekea chumbani kwake mama yake hali kadhalika.
Bryan kwa kipindi hiki alikuwa akiishi kwa mjomba wake huko cha ng'ombe. Msoto ndio ukazidi tena baada ya kupoa kwani aliyokuwa akiishi kwa mjomba wake ni hafadhali hata ya kwa mama wa kambo,kwani shangazi yake alimfanya ndio kijakazi wake, yote hayo tisa, kumi ni kwamba ilifika kipindi mpaka Bryan ananyimwa chakula, Bryan alipouliza kwa nini hakuna la zaidi ya kuambulia matusi na kejeli.
"eti unauliza chakula we unajua hizo pesa za hicho chakula zinavyotafutwa, nenda kaone mwanaamke wa kumuuliza chakula, eti chakula" shangazi yake Bryan aliongea tena kwa kubana pua.

Mambo yote hayo alishushiwa Bryan baada ya kuuliza chakula baada ya kutoka shuleni. Bryan hakumjibu kitu shangazi yake zaidi ya kuguna tu.

"Duh" kweli ng'ombe wa masikini hazai na akizaa dume tena lina matege. Bryan alijikuta machozi yakimteremka kila anapomfikiria marehemu mama yake.

"Laiti mama yangu angekuwepo haya yote yasingekuwepo, japokuwa maisha yetu yalikuwa ya kubangaiza" Aliwaza Bryan huku akifuta machozi.

Bryan alipojaribu kumueleza mjomba wake juu ya matatizo ya pale nyumbani mjomba wake alionekana kutoyatilia uzito mambo hayo.
"Huyo ndio shangazi yako we mchukulie jinsi alivyo au wewe unafikiri kuna mwingine? Aliongea mjomba wake Bryan kwa sauti ya kilevi.

"Oh. Mungu hivi mimi nitaishi katika hali hii mpaka lini? Eee mungu nauhitaji mwangaza wako"
Bryan aliongea hayo baada ya jibu alilopewa na mjomba wake.Aliachana na mjomba wake na kuelekea chumbani kwake.

Alipoingia humo ndani alisimama takribani dakika mbili, tatu kabla hajaamua afanye nini.
Taratibu alipiga magoti katika chumba chake kisichokuwa na sakafu kisha akaikusanya mikono yake pamoja na kuifumbata pamoja mbele ya kifua chake, kisha uso wake ukaelekea juu ya paa la chumba kisha akaanza kusali kutokana na matatizo aliyonayo.
"We Mercy"
"Abee mama"
"Baba yako anakuita yupo sebuleni"
"Nakuja mama"
Ilikuwa ni saa 3 asubuhi siku ya jumapili Mercy alikuwa akijiandaa kwenda kanisani ndipo mama yake alipokuja kumuita. Mercy nyuma ya drensing table alikuwa anazibana nywele zake kwa nyuma kwa banio lake la njano.

Siku hiyo alivaa blauzi ya njano na sketi ya pinki yenye kubana juu wastani na chini ilimwagika. Viatu alivyovaa siku hiyo ni vya rangi ya manjano vyenye maua ya pinki.

Hakika Mercy alipendeza kama sio kuvutia. Alijigeuza geuza pale kwenye drensing table baada ya kuridhika kuwa vile alivyo ndivyo atakiwavyo kuwa akaanza kupiga hatua za taratibu kuelekea mlango wa chumbani kwake ili aende sebuleni akawasikilize wito alioitiwa na babake.
"Shikamoo Dady"
"Fine how u doing" alijibu kwa umombo babake Mercy" "Well" aliitikia Mercy.
"Okey mama yako amenieleza juu ya matatizo yako"
"Ndio baba"alidakiza mercy
Nimekueleweni na nimekubali huyo kijana aje kuishi pamoja nasi, lakini ataishi kama houseboy"
"Woow" Asante sana baba endapo atakuwa hivyo" Lakini akija huyo kijana sitaki mambo ya upuuzi" akijaribu kwenda wrong na sheria zangu ataondoka mara moja.
"Sawa baba" Aliitikia Mercy kwa heshima zote.
Mercy alichukuwa biblia yake na kutoka kwenda kusubilia daladala ili kuelekea kanisa kuu, hiyo ni siku nzuri kwake.
Asubuhi ya kuamkia jumapili Bryan aliamka mapema kabisa na kuanza kufagia uwanja kuzunguka nyumba yao, baada ya kufagia aliingia chumbani kwake kufanya usafi, japokuwa chumba hicho kuta zake hazikuwa na rangi wala sakafu lakini yeye alikipenda sana na muda wote kilibaki nadhifu.

***BRYAN yatima anapata kibarua nyumbani kwa binti ambaye anampenda kwa dhati….Maisha yataendeleaje??


Khantwe davidson689 Toplady ram BPM Sangomwile Mamamercy jonnie_vincy mbalu byb sac mlyn VAN HEIST nrangomangimezamuuza ubuyu Jullie ZIgunga Mojaculbby mugaru
 
Huu ndio mtindo wako ​Casuist, unatudondoshea tone baada ya tone, yaani utamu utukolee!
 
hiii misiba sasa balaa hatupumziki...tumetoka kumzika deusi kwenye bondia ..tukaja joyce kwenye hatia leo tupo huku....daaaaah...wewe mercy halahala na mtoto wa watu...r.i.p bi sara.
 
SIMULIZI: PENZI ZITO
MTUNZI: Prosper Mgowe

SEHEMU YA TATU

Hakika Mercy alipendeza kama sio kuvutia. Alijigeuza geuza pale kwenye drensing table baada ya kuridhika kuwa vile alivyo ndivyo atakiwavyo kuwa akaanza kupiga hatua za taratibu kuelekea mlango wa chumbani kwake ili aende sebuleni akawasikilize wito alioitiwa na babake.
"Shikamoo Dady"
"Fine how u doing" alijibu kwa umombo babake Mercy" "Well" aliitikia Mercy.
"Okey mama yako amenieleza juu ya matatizo yako"
"Ndio baba"alidakiza mercy
Nimekueleweni na nimekubali huyo kijana aje kuishi pamoja nasi, lakini ataishi kama houseboy"
"Woow" Asante sana baba endapo atakuwa hivyo" Lakini akija huyo kijana sitaki mambo ya upuuzi" akijaribu kwenda wrong na sheria zangu ataondoka mara moja.
"Sawa baba" Aliitikia Mercy kwa heshima zote.
Mercy alichukuwa biblia yake na kutoka kwenda kusubilia daladala ili kuelekea kanisa kuu, hiyo ni siku nzuri kwake.
Asubuhi ya kuamkia jumapili Bryan aliamka mapema kabisa na kuanza kufagia uwanja kuzunguka nyumba yao, baada ya kufagia aliingia chumbani kwake kufanya usafi, japokuwa chumba hicho kuta zake hazikuwa na rangi wala sakafu lakini yeye alikipenda sana na muda wote kilibaki nadhifu.

Wakati ananyunyizia maji aridhini katika chumba chake ili kuondoa vumbi mara ghafla akasikia mlango wake ukigongwa kwa fujo, fujo hizo zilifuatiwa na sauti kali na yenye hasira.

"Fungua we mbwa" alisema shangazi yake Bryan. Bryan kwa unyonge aliachilia shughuli aliyokuwa akiendelea nayo na kufungua mlango.
"Shikamoo shangazi"
Baada ya kupokea hiyo salamu, shangazi yake bryan alimkata jicho Bryan toka miguuni mpaka utosini na kasha akarudia halafu akamsonya msonyo mrefu na kasha akaukamata mkono wa Bryan kwa nguvu na kuanza kumvuta kuelekea nyumba ya nyumba yao.

"Nimekwambia hizi nguo ziishe, na ole wako usizimalize" Aliongea shangazi yake Bryan huku akimtolea macho Bryan.

"Lakini shangazi nitachelewa kanisani"
"Nitachelewa kanisani" shangazi yake alibana pua na kuigiza maneno yale.

"Sasa nasema hivi usipomaliza hizo nguo huko kanisani utapasikia ti". Na ukidiriki kwenda hapa nyumbani usirudi, Ufungashe kilicho chako na usirudi tena hapa" Aliongea shangazi yake.

Ulikuwa ni mlima wa nguo, nguo hizo zilikuwa ni za shangazi yake pamoja na mjomba wake. Bryan akageuza shingo akaangalia hizo nguo zenyewe. Alipoziona tu mpaka uvivu ukamwingia.

"Nimalize" na sizimalizi potelea mbali lakini saa tatu ikifika mimi najiandaa kwenda kanisani, mimi sijali hata wakinifukuza "Aliwaza Bryan baada ya shangazi yake kurudi kulala tena. Mpaka kufikia saa tatu zilibaki asilimia 25 kati ya asilimia 100 ya zilizokuwepo, Bryan aliamua aziache akaanza kujiandaa kwenda kanisani.

Akachukua maji kwenda kuoga alipotoka kuoga aliingia chumbani kwake na kuchukua kikopo chake cha mafuta aina ya rays na kuanza kujipaka kasha akafunua godoro lake la futi 3 kwa 6 na kutoa fulana yake aina ya form 6 pamoja na suruale yake ya shule.

Baada ya kuvaa fulana yake yenye mistari ya bluu na myekundu akavaa suruale yake na kisha akachukua soksi zake za pundamilia na kuzivaa pamoja na viatu vyake vya shule. Akachukua chanuo na kuanza kuchana nywele zake zenye urefu karibu na nchi moja na nusu. Akachukua kipande cha kioo chumbani humo. Baada ya kujitazama na kujiona yuko sawa alichukua kitabu cha Agano jipya na kutoka kwenda kusubiri daladala ili aende kanisani.

Mjomba ake Bryan alikuwa bado hajaamka kwa sababu ya pombe alizokuwa amekunywa jana alikuwa bado ana hang over.

Akiwa usingizini akahisi kama kuna mtu anampiga mgongoni. Akashtuka na kugeuza shingo kuangalia aliyekuwa akimpiga piga mgongoni.
"Za asubuhi dear" kumbe alikuwa mkewe
"Safi" Alijibu kichovu
Amka basi unafahamu sasa hivi ni saa ngapi? "kwani sa ngapi?"
"Saa si hiyo hapo juu ya droo, pembeni ya kitanda. Akanyoosha mkono na kupapasa juu ya droo na kuchukuwa saa yake aina ya Disco isiyo na mkanda.
"Aisee kumbe saa tatu" Mjomba wake Bryan aliongea huku akinyanyuka na kukaa kitandani mara na mkewe naye akanyanyuka na kukaa kitandani na kuanza kumsugua mabegani mumewe, Akiwa bado anaendelea na zoezi hilo mara mjomba ake Bryan alishangaa kusikia mkewe analia kilio cha kwikwi.

"Vip Darling"
"Si huyo Bryan" alijibu mkewe
"Bryan ?"
"Ndiyo huyo huyo Bryan"
"Kafanya nini?"
"Mume wangu yule si mtoto" Aliongea shangazi yake Bryan huku akijiliza kilio cha kwikwi.
"Enhe" mjomba'ke Bryan aliguna kuashiria mkewe aendelee na maongezi.
"Hivi Bryan anaweza kunichungulia bafuni mimi" Aliongea huku akizidisha kilio.
"Halafu ninamkanya na hiyo tabia yake eti ye ananitukana anasema eti siwezi kufanya chochote kwanza hapa kwa mjomba ake kwa hiyo ninaweza kuondoka muda wowote.

"Ha, ha, ha," Mjomba'ke Bryan alipigwa na butwaa na bila kufikilia wala kufanyia utafiti maneno yaliyosemwa na mkewe akachukua hatua ya moja kwa moja.

"Pole sana dear, usijali akija tu ataondoka nitamwambia aelekee anakojua" Aliongea mjomba wake Bryan huku akimpigapiga mkewe mgongoni kumtuliza.

Mkewe akatulia na moyoni mwake alifurahia sana kitendo cha Bryan kufukuzwa.
"Mme wangu utakuwa umefanya jambo la maana kwa sababu huyu Bryan anaweza kuharibu ndoa yetu.

"Usijali, Basi nenda kaandaye chai"
" Sawa mume wangu"
Shangazi yake Bryan alitoka na kwenda jikoni.

Bryan hakuwahi kusali kanisa kuu la mjini Dodoma kabla ya siku hiyo, lakini siku hiyo hata yeye alijishangaa kwa nini siku hiyo anajisikia kwenda kusali kanisa kuu lakini kuna roho iliyozidi kumwambia aende kwenye kanisa hilo.

Bryan aliamua kutii roho hiyo na kuingia kwenye daladala na safari ya kwenda kanisani ikaanza. Walipofika maeneo ya kanisa kuu Bryan aliomba msaada ashushwe karibu na kanisani.

Alilipa nauli na kushuka na kwa mwendo wa haraka akaanza kuelekea upande wa kanisani ili kuwahi ibada. Aliingia kanisani na kukaa benchi la nyuma ambalo lilikuwa limejaa watu.Ibada ilikuwa imeanza kama dakika 10 hivi kabla ya Bryan kuwasili. Ibada ikaendelea na ndipo ikafika wakati wa kutoa sadaka, ulianza upande wa wanawake.

Bryani alijikuta akimtumbulia macho binti mmoja aliyekuwa amempa mgongo. Alijikuta akimsindikiza kwa macho mpaka alipotoa sadaka mpaka alipokizunguka chombo cha kuwekea sadaka Bryan ndipo alipomtambua kumbe ni Mercy. Bryan aliendelea kumsindikiza kwa macho mpaka alipoenda kwenye sehemu yake.

"Kijana vipi? Ni zamu yetu sasa" Bryan alishtushwa na mzee mmoja aliyekuwepo pembeni yake ndipo akasimama tayari kwa kuelekea kwenda kutoa sadaka.

Bryan alipokuwa akirudi kutoka kutoa sadaka alimuangalia tena mercy kwa jicho la wizi lakini kwa bahati nzuri au mbaya macho yao yaligongana na wote wakatabasamu. Kutoka hapo kila mmoja alikuwa akitamani ibada iishe haraka au ikatishwe ili kila mmoja akaonane na mwenzake.

Baada ya ibada kuisha watu walitoka nje ya kanisa tayari kwa kwenda makwao. Aliyekuwa wa kwanza kutoka ndani ya kanisa kati ya Bryan na Mercy, Bryan ndiye aliyekuwa wa kwanza kutoka kwenda kujiegemeza katika mazingira ya kanisani, pale Bryan alipokuwa amesimama alimuona kila alitekuwa akitoka ndani ya kanisa na mara ghafla akatoka Mercy.

"Wooow" Mercy alipiga kelele huku akimkimbilia Bryan.
"Hallo Bryan mambo vipi?"
"Safi habari yaw ewe?"
"Swadakta"
"Nimefurahi sana kukuona aliongea Mercy. "Vipi kuna jipya? Bryan alimuuliza Mercy huku akicheka.
"Yapo mengi tu" Alijibu Mercy huku naye akitabasamu.
"Haya basi nipe hiyo michapo" aliongea Bryan huku akitoka nje ya kanisa.

Mercy alimueleza Bryan mikakati juu yake na pia alimueleza jinsi wazazi wake walivyokubali aende kuishi kwao. Bryan alifurahi mno kwenda kuishikwa akina Mercy na hakujua amshukuru vipi binti huyo kwa wema wake huo kwa maana alishachoshwa na matatizo ya kwa mjomba wake.

Bryan naye alimueleza Mercy matatizo aliyoyapata kwa mjomba wake na alimueleza jinsi shangazi yake alivyo mchimbia mkwara eti kwamba asirudi kama hatakuwa hajamaliza nguo alizopewa azifue. Mercy alimuone huruma sana na kwamba asijali kwani yeye yupo pamoja naye, kwa hiyo toka nukta ile alikuwa yupo huru kuhamia kwao.

"Nyumbani kwetu si unapakumbuka?" Mercy alimuuliza Bryan kama bado anapakumbuka nyumbani kwao kwa maana alishawahi kumuonyesha siku moja tu.
"Ndio bado napakumbuka" Alijibu Bryan.
"Okey nitakuwepo kukusubiri"
Baada ya hapo kila mmoja akaingia ndani ya daladala ya kwao na kuondoka.

Mjomba wake Bryan alikuwa anamaliza kufungasha kila kilichokuwa cha Bryan tayari kabisa kwa kumtimua na shangazi mtu alikuwa ni mmoja wa washiriki wa shuhuli hiyo ya ziada. Baada ya shughuli kuisha, virago vya Bryan vikaanza kutolewa nje ya nyumba yao, hii inamaana kwamba pindi Bryan atakaporejea toka kanisani afikie kubeba kila kilicho chake na apotelee anapokujua yeye mwenyewe.

Shangazi yake Bryan alifurahi sana moyoni kwani alishaona kuwa ndoto yake aliyotarajia sasa inakwenda kutimia.

"Vipi mjomba mbona unatoa vitu vyangu ndani kwangu?" Ilikuwa ni sauti ya Bryan baada ya kurudi kanisani. "Ishia hapohapo, Mwana haramu mkubwa wewe, Sasa nakwambiaje? Kuanzia nukta hii chakula kila kilicho chako na sitaki tena kukuona katika mboni za macho yangu"

"Kwani mjomba nimekukosea nini? Bryan aliuliza kwa uchungu.
"Anhaa kumchungulia na kumtukana shangazi yako unaona uko sahihi eeh?"
"Mbona sijafanya hivyo mimi?"
"Nimekwambia potea kabla sijakutolea panga", muda wote huo shangazi yake Bryan alikuwa dirishani akishuhudia jinsi mambo yalivyo huko nje.

Moyoni mwake alifarijika mno kuona ya kuwa Bryan anaondoka humo chumbani alikuwa akicheka cheka na kurukaruka peke yake mithili ya mwehu.

"Afadhali hili Ibilisi liondoke kwa maana lilikuwa likininyima raha" Alijisemea shangazi yake kimoyomoyo.

* * *

"Kama nimefanya hivyo Mungu anajua" Bryan alijisemea hayo huku akilia, kilichomliza si kuondoka kwa mjomba wake bali manyanyaso ya pale. Alikusanya kilichomuhusuna kuondoka zake.

* * *

"Hodi,hodi,hodi," Bryan alibisha hodi mbele ya jumba moja lenye geti jeupe, lakini hakuna aliyeitika wala kutoka.
Aliendelea kubisha hodi takribani dakika 10 nzima bila ya dalili ya mtu yeyote kuja kufungua.

Baada ya muda mfupi ulisikika mngurumo wa gari nyuma yake, wakati huo Bryan alikwisha kata tamaa kabisa kugonga hili geti kwani hakukuwa na dalili yoyote ya mtu kufungua.
Ile gari ilikuja moja kwa moja kwa karibu na miguu ya Bryan. Kisha milango ya ile gari ikafunguliwa kisha ndani ya ile gari akatoka mzee wa mmoja wa makamo.

"Shikamoo baba", Bryan alimsalimu mzee aliyeshuka garini.
"Oh Marahaba kijani habari yako?"
"Nzuri tu baba"
"Bila shaka wewe ndiye Bryan? Mzee Josephat alimuuliza.
"Ndio Baba"

Mzee Josephat alibonyeza kitufe cha kengele kilichokuwako pembeni kidogo ya geti na mara moja ya geti likafunguliwa aliyefungua alikuwa mamayake Mercy.

"Karibu" Alisema mama Mercy baada ya kufungua geti.
"Asante mama, shikamoo" Bryan aliamkia kwa nidhamu
"Marahaba mwanangu" Aliitikia mama Mercy
Mzee Josephati alirudi ndani ya gari na kuingia moja kwa moja car parking. Mama Mercy alimpokea mizigoyake nakuifikisha vyumba vya uwani na baada ya hapo akampeleka sebuleni

Baada ya Bryan kukaribishwa na kuketi sebuleni walianza kujuliana khali na kutambulishana wakati huo Mzee Josephat alikuwa ameshapaki gari yake na kujumuika pamoja nao. Pindi utambulisho ulipokuwa ukiendelea Mercy naye alikuwa akiingia sebuleni akitoka bustanini alipokuwa amepumzikia.

"Wooow Bryan karibu sana" Mercy alikuwa amefurahi sana baada ya kumuona Bryan alitamani amkumbatie ila kwa heshima ya wazazi wake aliishia kumpa mkono tu.

"Asante sana Mercy nishakaribia"Bryan aliongea kwa aibu kidogo akichekacheka.
Mercy akatoa utambulisho kamili kwa mara nyingine tena. Baada ya utambulisho kukamilika mzee Josephat alimueleza Bryan majukumu aliyotakiwa kuwa nayo katika nyumba hiyo.

Bryan alizidi kufurahi kwani hakuona gumu lolote ambalo angeshindwa kulitekeleza.
"Mercy kamwandaliye mwenzio chakula" alisema mama Mercy.
Mercy alifanya shashaa na baada ya muda kidogo Mercy alileta chakula na kwa pamoja wakajumuika kwa furaha.

Usiku wa usiku hiyo Bryan alipewa chumba cha upande wa upande wa uwani kilikuwa kizuri, ndani kilikuwa na rangi ya blue bahari na silingboard nyeupe, kilikuwa na kitanda cha 5 kwa 6, meza ya wastani pamoja na kochi moja watu wa tatu.

Bryan alipokuwa amepumzika katika chumba hicho ni mambo mengi yalikuwa yakipita katika ubongo wake.
Kwanza alikuwa akifikiria ni kitu gani ambacho Mercy aliwaza mpaka akaamua kumtendea wema kiasi hicho, na kwa nini asiwe mwingine isipokuwa yeye, hakuelewa angemlipa nini binti huyo kwa hakika alimuona ni kama mkombozi wake ila alijiapiza ni lazima ipo siku lazima atamlipa fadhila zake baada ya kuwaza hayo alipiga magoti na kumshukuru mungu kwa kumtuma mwakilishi wake kuja kumkomboa katika sakata alilokuwa nalo. Baada ya kumaliza sala zake alijitupa kitandani na kuvuta hayo yote yalikuwa ni kama ndoto lakini ni kweli.

Kwa upande wa Mercy alikuwa na furaha isiyokifani, furaha hiyo ilitokana na kuwa karibu na Bryan. Kwa Mercy aliamini ndoto zake za kummiliki Bryan zilikuwa zinaenda kutimia.

Mercy kwa kipindi hicho alikuwa amekaa juu ya kitanda chake, miguu yake akiwa ameikunja na mikono yake ikiwa imekumbatia mto wenye umbo la kopa.

Huku akisugua mto huo kwa taratibu fikra zake zikimpa kana kwamba yupo pamoja na Bryan.
Wakiwa wamesimama pamoja tofauti ya hatua moja.
"Bryan naomba nikumbie kitu"
"Kitu gani hicho Mercy?"
"Mmh, mmh?
"Mmh,mmh,kitu gani wakati umesema kuna kitu unataka kuniambia"Alihoji Bryan
"Naomba usinifikirie vibaya naheshimu hisia zangu ndo maana nimeamua kukuambia, Nafahamu mapenzi sio kitu rahisi, Lakini naomba unimiliki, NAKUPENDA SANA BRYAN". Kabla Bryan hajaongea kitu Mercy alinyoosha mkono ili kumkumbatia Bryan lakini huyo Bryan hakuwepo kwa Mercy yalikuwa ni mawazo tu ya kufikiria tu.

Akiwa juu ya kitanda chake alichanua tabasamu hafifu la kujifariji kwamba iko siku lazima mawazo yake aliyokuwa anayawaza nucta chache zilizopita ni lazima yatatimia.

Je! NDOTO ZITATIMIA???


Mokoyo
Khantwe davidson689 Toplady ram BPM Sangomwile Mamamercy jonnie_vincy mbalu byb sac mlyn VAN HEIST nrangomangimezamuuza ubuyu Jullie ZIgunga Mojaculbby mugaru
 
mhhhhhh huyu nae asije kumuhalibia mtoto wa watuuuu
 
Back
Top Bottom