Sehemu ya 22
“Hawa!” aliita Hamisi.
“Niambie!”
“Poa! Naomba kuzungumza nawe kidogo,” alisema Hamisi huku akimvuta Hawa pembeni, msichana huyo akakubali na hivyo kusogea pembeni.
Kwa kumwangalia tu, Hawa alikuwa msichana mrembo, aliyevutia, nywele ndefu, suruali ya jinzi na macho yake alibandika kope, midomo iliyopakwa lip stick, alionekana kuvutia.
“Kuna nini?”
“Kuna kitu nahitaji unisaidie,” alisema Hamisi.
“Kitu gani?”
“Unamfahamu yule rafiki yangu, Rahim?”
“Yule Mzanzibar?”
“Yeah!”
“Kafanyaje?”
“Ninataka umtege, uende naye chumbani, yaani umtege kwa staili hiyo!” alisema Hamisi, Hawa akashtuka.
“Nimtege?”
“Ndiyo!”
“Halafu!”
“Nitakulipa pesa! Kama laki moja hivi kama ukifanikiwa kulala naye,” alisema Hamisi, alijiahidi hata kulipia pesa lakini alihitaji kujua mengi kuhusu rafiki yake huyo.
“Mzanzibar?”
“Ndiyo!”
“Hivi wewe hujui michezo ya Wazanzibar?” aliuliza.
“Ipi?”
“Hahaha! Haloooo...”
“Mbona unacheka! Si uniambie!”
“Hivi unahisi siuthamini?”
“Huuthamini nini?”
“Nauthamini sana! Siwezi kudate na Mzanzibar! Naanzaje kudate naye! Eti natoka niende kwa Mzanzibar! Haiwezekani! Nauthamini sana! Wana michezo ya kifirauni sana wale,” alisema Hawa huku akionekana kugoma kabisa kumfuata mwanaume huyo.
Hamisi hakutaka kushindwa, alijitahidi kumbembeleza kijana huyo kukubaliana naye lakini ilishindikana kabisa. Hakutaka kuachana naye kwani aliamini mwisho wa siku angekubali na hivyo kufanya kama alivyokuwa akitaka kufanya.
Siku ziliendelea kukatika huku Hamisi akiendelea kumwambia Hawa kwamba lingekuwa jambo jema kama tu angekubaliana naye kumfuata rafiki yake huyo na kufanya naye mapenzi kama alivyokuwa amezungumza naye.
“Ila pesa ipo?” aliuliza Hawa kabla ya yote.
“Ipo!”
“Ila zungumza naye, yale mambo yao sitaki mie!” alisema Hawa, aliipenda pesa lakini wakati mwingine alikuwa na wasiwasi tele.
“Hahah! Hawa bhana! Sawa nitamwambia!” alisema Hamisi na hivyo kuondoka huku akimuacha msichana huyo afanye kile alichomwambia.
Hawa hakuwa na presha, alijiamini, alikuwa na umbo matata sana, kwa nyuma alijaa na kifua chake kilikuwa kidogo kabisa, sura yake iliita na mapaja yake manene yaliwachanganya wanaume wengi waliokuwa wakimwangalia.