Simulizi: Mapenzi ya dhati

[
B]
MAPENZI YA DHATI

SEHEMU YA KUMI NA MBILI:[/B]​


Miaka ilizidi kukatika wazo la Bi. Gaudencia kumtoa Adam katika jumba lile lilikuwepo kichwani mwake kwani udhaifu alioupata Reshmail pamoja na kashfa mbaya anazozipata pale chuoni zilimsononesha sana lakini ataanzia wapi kuificha aibu yake pale ambapo Adam,akasababisha uovu wa mama huyu uwekwe hadharani.

Ni jambo hilo lililomuumiza kichwa mama huyu.

"Reshmail na baba yake watanielewaje kwa mabaya niliyowafanyia,nimeishusha heshima ya mume wangu aliyekuwa na heshima kubwa bungeni" alizidi kuwaza

Huku Iringa maeneo ya Ruaha Adam alikuwa anauanza mwaka wa tatu,akiishi kama nyumbani kwake,lakini hakuridhika hata kidogo maisha hayo ya ufungwa.

Miaka mitatu ilikuwa mingi sana "Mama na baba yangu wanahisi niko wapi? vipi kuhusu mpenzi wangu Reshmail,hapana imetosha nahitaji kutoka hapa,lakini lazima nijiulize nitatoka vipi hapa katika ngome hii" alijisisitiza Adam japo ulinzi madhubuti ulioongezwa kutokana na kutoroka kwa Bite katika mazingira ya kutatanisha pale ngomeni

***

Mwaka wa pili uliisha hivyohivyo kimateso makali yaliyojawa na kumbukumbu mbaya na isingekuwa kuhamishwa kwa darasa la sheria mwaka wa pili kwenda katika maghorofa ya Mwanjonde chuoni hapo basi Reshmail angefeli vibaya masomo yake kutokana na msongo wa mawazo.

Akiwa mwaka wa tatu afya yake ilirejea tele kwani hakuwa akiiona tena picha kubwa ya Adam machoni pake hali hiyo ya afya kurejea ilizusha msemo mpya tena,tofauti na mwanzo walivyosema ana Ukimwi,sasa walisema "Akikonda ana virusi,akinenepa ameanza kutumia dozi"

Yote hayo alituhumiwa Reshmail lakini kamwe hakuwahi kuthubutu kunyanyua mdomo wake kujibu vijembe hivyo yeye alikuwa mkimya huku akipambana na masomo hadi alipoumaliza mwaka wake wa nne vyema.

Mnamo mwezi wa kumi na moja familia yake yote ilisafiri kuelekea jijini Mwanza kusheherekea kwa pamoja mahafali ya mtoto wao,Eveline ambaye tayari alikuwa kazini baada ya kuwa amemaliza miaka yake mitatu chuoni na kufaulu vizuri pia alijumuika katika kukamilisha furaha hii ya rafiki yake mpenzi huku akiongozana na mchumba wake Benjamin Simon.

Reshmail alifurahishwa sana na ujio wa Eve kwani alizidi kudhihirisha kuwa ni kiasi gani yeye ni rafiki wa kweli.

Yalikuwa ni mahafali makubwa na ya kipekee kuliko yote yaliyowahi kutokea ambapo chuo cha Mt.Augustino kilifanya mahafali ya pamoja na matawi yake yote Tanzania,yaani Iringa,Mtwara na Tabora. Kwa ufupi yalikuwa yamefana.

Ni katika pirikapirika na pitapita za huku na huko za sherehe hiyo ndipo Reshmail akiwa na Eveline ana kwa ana anakutana na familia ya Adam yaani baba na mama yake,aliwatambua kwa uwepo wa Rosemary yule mdogo wake Adam.

Rosemary alikuwa ndio kwanza amehitimu shahada ya elimu katika chuo kikuu cha mtakatifu Augustino tawi la mtwara hivyo yeye na familia yake pia walikuwepo katika viwanja vya Raila Odinga kusheherekea mahafali yale.

"Mchawi...mchawi!" alianza kupiga kelele mama yake Adam wakati Reshmail akisogea taratibu katika eneo walilokuwepo kwa furaha.

"Uuuwii" alipiga makelele kwa sauti ya juu jambo lililovuruga usikivu katika eneo lile na watu kuanza kumwangalia yeye kama mtu aliyechanganyikiwa, Reshmail na Eve walikuwa wameganda tu na mama Adam akizidi kupiga kelele,

Jitihada za baba yake Adam kumtuliza mkewe hazikufua dafu,mara ghafla mama Adam akakurupuka akiwa na chupa iliyokuwa na soda ambayo haijafunguliwa bado na kwa kasi akaenda kumkabili Reshmail ambaye akili yake ni kama ilikuwa imesimama na umati uliokuwa umemkazia macho kwa kitendo cha kuitwa mchawi ulimzidishia hofu na fedheha kwake, Eve alimshika mkono Reshmail na kujaribu kumvuta watoke eneo lile lakini tayari mama Adam alishawafikia na kwa nguvu kabisa akaituliza chupa ile juu ya kichwa cha Reshmail palepale akaenda chini huku damu nyingi ikimtoka kichwani.

Wanaume watatu akiwemo pia baba yake Adam walifika na kumbeba juu juu,mama Adam ambaye alionekana dhahiri kuwa bado hajaridhika na kipigo alichotoa kwa Reshmail kwani bado alikuwa anaangaza huku na huko kama palikuwa na silaha nyingine. Alikuwa kama mwendawazimu.

Wengine walimbeba Rshmail ambaye joho lake la kipekee kabisa lilikuwa limechafuliwa vibaya na vumbi la uwanja wa mpirawa miguu wa Raila Odinga ambapo ndio sherehe zilifanyika. Hali ya sintofahamu ilitawala sherehe zile kwa takribani nusu saa nzima hadi Reshmail alivyoondolewa na familia yake kuelekea hospitali na mama Adam kutiwa katika nguvu ya dola

***

Halikuwa jeraha kubwa sana nyuzi mbili zilipita katika kichwa chake kushona jeraha lile

“kwa nini mama mkwe wako akutende hivi” eve alimuuliza Reshmail akiwa pale kitandani

“ni haki yake hata kunipiga risasi mimi ni chanzo cha maumivu haya wanayoyapata” alijibu Resh huku akilazimisha tabasamu

“kwa hio hapa amenionea huruma sana mimi ni sawasawa na muuaji tena wa kukusudia na haki yangu ni kuuawa pia” aliendelea Reshmail huku akitoa tabasamu hafifu tena

“usiseme hivyo mamii sio wewe uliyetaka iwe hivyo ni Mungu pekee” aliongea kwa upole Eve huku akivibinyabinya vidole vya Reshmail

“mama mwambie baba afatilie mama mkwe asije kulazwa selo hata kwa saa moja hana kosa lolote” Reshmail alimwambia mama yake alipoingia katika chumba cha hospitali ya Agha khan aliyokuwaelazwa kwa ajili ya matibabu maneno hayo yalimshangaza sana mama yake aliyetegemea Reshmail atakuwa na hasira ya kutendwa vile mbele ya hadhara

Nafsi ilikuwa inamsuta sana mama reshmail,moyo uliomba msamaha lakini mdomo ulikuwa mzito sana kufanya hivyo. Hali hiyo ilimkondesha sana na kumkosesha raha ndani kwa ndani unene wake wa asili uliyafunika yote hayo na hakuna aliyejua jambo zito alilobeba mama huyu.

Kweli badala ya bwana na bibi Manyama kuegemea upande wa mashtaka ili mama Adam apewe adhabu la wao waliunga mkono kwamba Reshmail alikuwa na makosa mahakama ikatupilia mbali mashtaka hayo na mama Adam akawa huru,jambo hilo badala ya kurudisha undugu liliongeza chuki na uadui

“si nilikwambia ukabisha?? Kama hawajamtoa mwanetu kafara kwanini sasa wamekubali niachiwe huru??” mama Adam alimwambia mumewe jambo ambalo wakati huu hata yeye alikubaliana nalo kuwa motto wao mkubwa wa kiume(Adam) alitendwa vibaya na familia ya reshmail .

kuamini kwa mzee Michael baba yake Adam ni sawa na familia nzima kuamini kabisa na sumu ya chuki ikamwingia kila mwanafamilia na kuwa aadui wakubwa wa familia ya mzee Manyama.



* * * * * * * * * * *


ITAENDELEA..........
 
MAPENZI YA DHATI

SEHEMU YA KUMI NA TATU:


Siku mbili alizokaa pale hospitali hakuja hata mwanafunzi mmoja kutoka pale chuoni kuja kutoa pole kwa Reshmail wote waliogopa wakiamini alikuwa mshirikina .

Eve hakukubaliana hata kwa mbali na shutuma hizo kwani alimwamini sana Reshmail hivyo aliendelea kuwa pale hospitalini pamoja na mchumba wake kumuuguza Reshmail ambaye alitoka siku tatu baadaye.

“baba mimi nitaenda na Eve kwake nitakaa siku tano ndio nitakuja huko” Reshmail alimpa taarifa hiyo baba yake naye hakupinga kwani amani aliyokuwa nayo Resh akiwa na Eve ilikuwa kubwa mno hali iliyowapa faraja hata wazazi wake hivyo walimruhusu bila kusita.

Siku hiyohiyo walipanda ndege kwa gharama za mchumba wa Eveline aitwaye Benjamin Simon,kuelekea Iringa ambapo Eve alikuwa amepata ajira katika benki ya N.B.C tawi la hapo.

Maisha yao yalikuwa mazuri sana kwani Benny alikuwa mwalimu wa shule ya sekondari hivyo katika majukumu waliweza kusaidiana na upendo wa dhati kati yao ulipendezesha zaidi nyumba yao.Reshmail alivutiwa sana na maisha hayo na kumkumbuka sana Adam wake “laiti angekuwepo tungeishi hivi siku moja “ alijiwazia Reshmail wakati akiwaangalia Eve na Benny wakiwa kwenye kochi wamebebana kwa furaha huku wakitaniana

Ilikuwa jioni moja Reshmail na Eve wakiwa katika mizunguko ya hapa na pale mizunguko ambayo kwa namna moja au nyingine iliibua ghafla safari ya kuingia sokoni,waliingia hapo kununua matunda matunda,zilikuwa zimepita siku tano na tofauti na alivyowahaidi wazazi wake hata hakuwa amefikiria kurudi Dar maisha ya Iringa yalikuwa yamempendeza sana .

“Eveline ona eveline jamani angalia kale katoto!!!” Reshmail alimgusagusa begani Eveline huku akimwonyesha kikundi fulani cha watoto pale sokoni

“wewe achana hao machokoraa walionikwapua pochi langu sina hamu nao hata kidogo,kisimu changu cha mchina na shilingi elfu thelathini zikapotelea hewani looh!! Wabaya hao” aliongea kwa hasira Eve huku akisitisha zoezi la kula chungwa aliliokuwa anafanya kwa wakati ule.

“mh!! Eve jamani achaga uongo yaani katoto kama kale jamani hebu kaone kale kadogo “Reshmail alizidi kusisitiza lakini Eve alionyesha bado ana uoga na uchungu moyoni wa kuibiwa vitu vyake na watoto aliowaita machokoraa

“Reshmail shauri zako vitakuliza hivyo we endelea kusema ni vitoto………..mh!! Resh lakini kale kadogo kazuri kweli” aliongea Eve alipokaona kale katoto ambako Reshmail alisisitiza sana.

“toto zuri jamboo!!”

“sijambo shkamoo!!” kalijibu katoto kale kwa uchangamfu sana baada ya Reshmail na Eve kukasogelea na kukasalimia.

“marahaba mtoto mzuri mbona upo hapa! Mwenyewe au hawa ni kaka zako?” Resh alimuuliza

“a a sio kaka zangu mi namsubiri mama ameondoka na watu wameenda huko amesema anarudi nimsubiri” alijibu tena kwa sauti ya kitotototo

“umekula??” aliuliza Eve.

“looh!! Eve hujaacha tu maswali yako ya kichoyo ya uchagani kwenu mh! Unataka aseme amekula ili umnyime au ?” Reshmail alimshushua Eve kiutani

“mh! Limeniganda shoga,una mashushu wewe!!” alijibu Eve kiaibuaibu huku akimpa yule mtoto chungwa lililokwisha menywa tayari.

“mama anarudi saa ngapi??” Reshmail alimuuliza yule mtoto tena
“sijui nimemsubiri hata hajaja amenipa chai tu akaondoka na wale wanaume wawili” alijieleza vizuri motto yule

“mh!! Mjini mjini tu katoto kanajieleza utadhani mtu mzima dah!” Eve alimnon’goneza Reshmail

“haya twende ukale eti motto mzuri!” Reshmail alimwambia yule motto naye akakubali kwa ishara ya kichwa,akiwa pekupeku akafuatana na Reshmail hadi kwenye mgahawa ulioandikwa “MAMA FRED MGAHAWA” uliokuwa pembeni kidogo ya soko kuu la Iringa.

“utamsalimia mama eeh!!” baada ya kumnunulia chakula walilipa na kumuaga

“haya mamdogo!” alijibu yule mtoto

“unaitwa nani vile”Eve akamuuliza

“naitwa Christian motto wa mama Bite” alijibu na wote kwenye mgahawa wakacheka


Kuifananisha na picha ya Adam, dimplez za yule mtoto zilimfananisha kabisa na Adam, achilia mbali rangi yake ya maji ya kunde na ucheshi wake.

"Eve hapana,mbona kesho naenda kumtafuta Christian ili nimjue baba yake anavyofanana,haiwezekani kufanana kwa kiasi hchi hapana "Aliongea Resh huku akiifunika album ile .

Eve alikubaliana naye na siku iliyofuata majira ya saa nne,walikuwa katika hoteli ya yule mama ambapo walimwacha Christian.

"Nyie watoto ni kesi gani hyo mmetaka kuniachia jana" mama mnene kiasi mmiliki wa mgahawa wa Mama Fred aliwapokea kwa maneno hayo makali huku akifunga kanga yake vizuri kiunoni.

Resh na Eve hawakuwa na jibu la kutoa walidhani amewafananisha labda

"Mama ni nini tena,mbona sisi...." alijaribu kujieleza Eve huku akiishiwa maneno ya kujieleza.

"Mmenitekelezea mtoto hapa anaanza kunililia hapa usiku he! jamani mnataka mniuwe kwa presha mkurya wa watu mie" aliongea kwa ghadhabu na mshangao mkubwa sana yule mama.

"Mama sisi tumempata hapo sokoni,ndio kumleta hapa kwako kwa ajili ya kupata chakula tu mama yangu" Reshmail alinyanyua mdomo wake na kuzungumza kwa sauti iliyojaa mshangao pia.

"He! mauzauza gani haya jamani,mi nimempeleka pale kituo cha polisi usiku uleule ndugu


**************************************


ITAENDELEA............
 
Mbona haujamalizia isabela ndani ya mpango hasi?Au sio wewe msimulizi?
 

MAPENZI YA DHATI

SEHEMU YA KUMI NA NNE:


Baridi kali ya Mbeya ilikuwa imemkataa motto wa Bite (Christian) kwa hali hiyo alipotimiza miaka miwili waliondoka na kurudi tena Iringa ambapo Bite alitaka kukaa kidogo halafu aende Mwanza kuweka makazi mapya huko.

Jambo la kushangaza licha ya baridi ya Iringa hali ya Christian ilianza kuwa njema kama awali jambo lililosababisha Bite aendelee kukaa katika mkoa huo.

Hadi anatimiza miaka mine hali yake kiafya ilikuwa njema sana na tayari Bite alikuwa amesahau suala la kwenda Mwanza. Akaanzisha genge la kuuza uji na karanga mida ya jioni na mihogo ya kukaanga majira ya asubuhi.

Ilikuwa biashara ndogo lakini iliyomuingizia kipato kizuri tofauti na matarajio yake.aliweza kupanga nyumba ya chumba kimoja na sebule aliyoishi na mwanae kwa furaha sana tu bila masumbufu yoyote hadi siku hiyo asubuhi alipokuwa anauza mihogo yake ambapo wanaume wawili ambao sura zao hazikuwa ngeni machoni pake walipofika eneo la biashara yake.Aliwapokea kwa furaha sana na bashasha kama wateja wengine aliozoeana nao.

”Bite tukuone pembeni kidogo samahani lakini’ wawili wale walimvuta pembeni Bite

“mh! Mikopo asubuhi asubuhi hamna kwakweli mtadhalilisha hizo suti zenu” aliongea Bite kwa utani huku akiwafata walipo wawili hao

“funga biashara tunaondoka na ukithubutu kupiga kelele au kukimbia nasambaratisha ubongo wako nadhani hujawahi kufikiria kifo cha namna hiyo,hivyo basi fanya kama unavyoagizwa” aliambiwa Bite na wale wanaume huku mmoja akifunua koti lake jeusi la suti na kumwonyesha Bite kitu ambacho hakujiuliza mara mbili mbili kuwa ile ilikuwa ni Bunduki,

Kwa kuutambua uoga alioupata Bite,yule mwenye bunduki alimbandika kitu mfano wa kishikizo cha nguo na kumwambia “hiyo ni sound recorder nenda ukawaambie wateja wako sisi ni ndugu zako tumekuletea taarifa za msiba nitakuwa nakusikiliza hapa, ole wako nasema ole wako usifuate maelekezo” alipewa masharti hayo ya uongo Bite ambaye laiti isingekuwa pensi yake ya jinsi ambayo huwa anavaa kwa ndani ili kuhifadhia pesa zake za mauzo basi mkojo uliopenya bila yeye kujua ungemwagika palepale hadharani na wala asingepatwa ma aibu yoyote ile.

Kama alivyoagizwa aliwaeleza wateja wake wawili waliokuwa wanamalizia kuitafuna mihogo waliyokuwa wameinunua,wakampa pole za dhati .

jasho lilikuwa linamtoka alitamani kutumia ishara kuwaambia kwamba yupo katika hatari lakini alipowazia mdomo wa bunduki alikaa kimya kabisa,bila kificho Bite aliiogopa sana bunduki na hakupenda kumwacha Christian katika umri ule.

Tayari akili ilisharudi nyuma akatambua hasa,hao watu alikutana nao wapi,walikuwa ni baadhi ya wafanyakazi katika ile ngome aliyekaa miaka miwili na ni hao waliomleta Adam pale ngomeni

“nimekwisha mimi Beatrice” alijiwazia Bite huku akitetemeka.

Baada ya kuifunga biashara yake aliwafuata akiwa na mwanae amemshikilia mkono.

“nadhani unajua hatuhitaji mtoto!!! Tunakuhitaji wewe tena sasa hivi” aligombezwa Bite na bila kujijua akajikuta akimwacha mwanae pale

“Christian narudi sawa nisubirie pale sokoni sawa mwanangu!

“haya mama alijibu Christian kwa furaha kwani alijua amepata fursa kubwa na ya kipekee kwenda kucheza na watoto wenzake pale mtaani

“ulidhani unaweza kutuzidi ujanja sisi,umepotea sisi hatupimiki hata kidogo umeumia tena umeumia sana aliambiwa Bite na wale wanaume wakiwa kwenye gari kuelekea kwenye gari kuelekea kule katika ngome jambo hilo Bite hakulitamani hata kidogo,japo alimpata Christian kwa bahati mbaya lakini alikuwa akimpenda sana kutoka moyoni na hakuwa tayari kutenganishwa naye kwa namna yoyote ile.

Alijiuliza maswali mengi sana ni nani atakayempa chakula mwanaye siku hiyo na nyingine zitakazoendelea wakati yeye hayupo,michezo ya kukimbizana aliyoipenda Chriss pia ilimtia hofu Bite na kuhisi huenda mwanae anaweza kupoteza uhai wake kwa kugongwa na gari.

Funda la hasira lilimkaba kooni alitamani kufanya lolote lile wakati huo lile jambo liwe ndoto kwake, machozi yaliyotoka ndio yaliyeyusha lile fundo japo kidogo,hasira kali ilikuwa imemkaba Bite aliyekuwa amekaa siti ya nyuma na jamaa mwenye Bunduki katika koti lake lakini maskini hakuwa na la kufanya hadi gari lilipoingia ndani ya ngome ile


* * * * *

Macho ya Reshmail yalitawaliwa na taswira ya yule mtoto Christian, zilikuwa ni siku nyingi zimepita tangu afungue album yake kumwangalia mpenzi wake (Adam) aliyeaminika kuwa tayari ni marehemu.Ni katika usiku huu alipokuwa akipitia album ya Eveline ndipo tena anakutana na picha ya Adam ambayo yeye (Adam) alimpa Eveline walipoenda Mwanza.

”Eveline,Eveline,Eve……….huyu hapa ni nani???”

“we umechanganyikiwa tena eti hebu acha mambo yake ya ajabu huyu Adam” Alijibu Eve kwa uoga.

“ na tuliyemwona leo kule sokoni ni nani??” aliuliza Reshmail

“we Reshmail jamani wanafanana Mungu wangu mbona wamefana hivyo lakini eeh!! Eve alijikuta picha ya mtoto Christian ikiumbika kichwani mwake na Zangu kwa sababu nimekaa naye hadi saa nne tumemsubiri huyo mama yake aje wapi!! Nikaona isiwe shari ngoja nimpeleke polisi penye usalama kuepuka balaa kumbe na nyie hamjui ni wa nani he!!” alitoa maelezo hayo yule mama na kueleweka vyema kwa Reshmail na Eveline.

“hicho kituo cha polisi umesema kipo wapi?” aliuliza Eve

“kile pale kinaonekana hata kwa hapa,lile jingo la bluu nyuma yake” alielekeza yule mama
Ndani ya dakika tano tayari Reshmail na shoga yake walikuwa mbele ya mapokezi ya kituo cha polisi Iringa mjini, na walikuwa kwenye foleni wakisubiri zamu yao ya kuhudumiwa ifike.

“nyie ni ndugu zake? Au mmoja wenu ndio mama yake?”

“hapana sisi si ndugu zake ila……”aliishia njiani katika maongezi yake Resh baada ya kukatishwa na yule askari “ila nini? Yaani nyie wanawake wa siku hizi suala la kujali watoto wenu hamtaki kabisa kulisikia mnachojali ni urembo tu wa sura zenu”

“jamani sio kwamba kuna ndugu yake hapa kati yetu ila sisi tumemkuta jana kule sokoni ndio tumemnunulia chakula halafu tukajiondokea zetu,leo hii ndio tunapita pale kwa mama Fred yule mwenye mgahawa yeye ndiye ametupatia taarifa hiyo tukaona sio vibaya nasi tukifika kumwona huyo motto” aliongea Eve aliyeonekana kutokuwa na hofu na kituo cha polisi lakini Reshmail alikuwa ana uoga kwa mbali kama vile anatuhumiwa kwa lolote lile.

“haya yupo tumemuhifadhi na tumepeleka taarifa kwenye vyommbo vya habari wataanza kutangaza kama mama yake bahati mbaya haya atakuja kumchukua na kama amemtelekeza akajiandae kwenda kuishi kwa watoto yatima sisi hatuna uwezo wa kuhifadhi watu hapa zaidi ya mahabusu” alijieleza askari yule huku akijipepea joto kwa kutumia kofia yake iliyochakaa


Majuma mawili yalipita bila mama wala ndugu wa motto kupatikana licha ya kituo cha redio maarufu mjini iringa cha Ebon fm kutangaza kila siku bila kukoma

“Eve naenda kumchukua yule motto nafsi yangu inanishauri hivyo na ni lazima nifate ambacho nafsi yangu inaniamuru” Reshmail alimwambia Eve siku moja wakiwa wamekaa sebuleni wakiangalia habari katika luninga.Eve alikuwa amejenga tabia ya kutobishana na rafki yake huyo kwani furaha yake ilikuwa ni kumwona Reshmail akiwa na furaha tele

“lakini Resh,mama yake si atamtafuta ssana??”

“Eve yaani imetangazwa hivyo redioni na hajajitokeza leo hii mie tu kumchukua ndipo ajitokeze? Looh! Acha nae ahangaike kidogo” alijibu Reshmail kwa jeuri

“mh! Haya sikuwezi mwanasheria wangu”

Polisi hapakuwa na usumbufu ni wazi kwamba walikuwa wamechoshwa na matukio ya watoto kutelekezwa na wazazi wao pasipo sababu zilizo wazi,hivyo kitendo cha Resmail kuamua kumchukua Christian ilikuwa ahueni kwao.aliandiokishwa maelezo mafupi tu kabla ya kuruhusiwa kondoka na mtoto ambaye alikuwa dhaifu tayari kutokana na lishe duni na upweke wa kutomuona mama yake kwa siku hizo zote.

Reshmail alikuwa ameyafurahia sana maisha ya Iringa,kampani kubwa kutoka Eveline na mchumba wake ilibeba nusu ya furaha yake huku nusu nyingine ikikamilishwa na uwepo wa Christian mikononi mwake,mara kwa mara alipenda kuwa naye karibu huku akimwita mume wako jambo lililompa faraja kubwa moyoni

”Eve jamani nitakumiss kipenzi changu lakini nitarudi tena asanteni sana kwa ukarimu wenu mlionionyesha tangu mwanzo nimeishi kwa furaha kubwa sana hapa” Reshmail aliyazungumza hayo alipokuwa anawaaga Eve na Benny usiku ambapo kesho yake alitegemea kurejea Dar-es-salaam akiwa ameandamana na Christian mtoto aliyempata katika mazingira ya kutatanisha
Kwa Christian safari ya kutoka Iringa kwenda Dar ilikuwa safari yake ya kwanza ndefu zaidi kuwahi kusafiri

Siku iloyofuata wawili hawa walikuwa ndani ya basi la ‘budget’ litokalo Mbeya kwenda Dar likipitia Iringa.

“Mama alisema baba yupo pale kwenye ile nyumba, tushuke nikamsalimie!” Chriss aliongea hayo huku akielekezea kidole chake kwenye jingo lililoonekana kwa mbali mno kutokea pale barabarani na hapakuwa na dalili ya kuishi mtu pale hivyo Reshmail akachukulia kuwa ni akili ya utoto imemtuma Chriss kuzungumza akaamua kupuuzia

“chriss alikwambia nani we muongo!!”

“alinambia mama siku moja hivi tulipita hapa ,halafu mama alinikataza kusema uongo ni dhambi” alijieleza Christian haraka haraka

“mh! Haya tutakiuja siku nyingine sawa mfalme wangu” Reshmail alimjibu Chriss ili kumlidhisha kwa aliyokuwa anasema


** ** ** **
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…