SIMULIZI: Mama mkwe

Nimefarijika kuwa mama mzazi Ni MTU wa fireeeee,kitaeleweka tuu.
Ni true story au?
 
We back as we nevel left....ngoja nitupiemo maepisode yakinyama fulu maujanjaaa, mbilinge kama zote....twenzetu....
 
Mwendelezo lini?
Kama lisaa hivi, nipo naandika wangu...hii kitu natoa kichwani kwaiyo ilibidi nianze kusoma upya nisije walisha matango pori
...maana kichwa kina mengi hiki...leo tutapata mwendelezo kipenzi, episode tatu za kushiba munooo
 
SEHEMU YA TISA:


VITA YA NNE YA DUNIA....


Walisemaga pepo ya Dunia ipo chini ya miguu ya mama zetu eeeh, niliona simanzi ya mume wangu kutengana na familia yake, hasa mama ake kipenzi, mama aliemlea na kumsimamia tangu utoto , mama aliepambana kama single mom baada ya kifo cha mzee, mama aliegoma kuolewa tena kisa hakutaka kuchanganya dam ya Koo mbili kwa familia yake, leo hii hamudu hata kumpa salamu... nikawaza siku ikitokea familia yangu imenitenga nitamudu kusonga kweli?

Nikampigia mamangu mzazi, nikamueleza yanayomsibu mume wangu, jinsi anapambana kua baba bora, na wakati huohuo abaki kua mtoto bora kwa mamake na kaka bora kwa wadogo zake...mamangu kipenzi akanambia atakuja tuzungumze, yapo mambo japo ni ya familia ya mme wangu ,yeye hayamuhusu, lakini mwisho wa siku mimi nabaki kua mwanae, usalama wangu unamuhusu kwa asilimia nyingi sana.

Mamangu kipenzi alikuja baada ya siku kadhaa, alinambia amekawia kuitikia wito maana alikua katika maombi maalumu kuombea ndoa yangu, mama alinisema sana kwa kuacha kusali na kuishi kwa kumtegemea Mungu. Mama alinambia amefunga siku Saba ili apate maono ya kile kinachonisibu maana ni kama ninasita kuelezea kwa undani.

Mama alinambia mambo mazito sana, alinambia kua kitovu cha kijana wangu wa kwanza nilikipeleka wapi? Sikua na kumbukumbu yoyote maana ni miaka nane sasa tangu nimpate mwanangu wa kwanza. Mama akanambia jaribu kukumbuka, kitovu cha mwanao kinabeba uhai wa mwanao, kiroho ina maana kubwa sana. Nilivuta kumbukumbu kwa utulivu sana, nikakumbuka kua nilimuita mama mkwe nikamuonesha, mama mkwe aliondoka nacho hakunambia zaidi.

Mama alinambia ulipata kumuuliza amekihifadhi vipi? wewe kama mama mzazi wa Lameck unapaswa kufahamu wapi kitovu cha mwanao kimehifadhiwa...niliona mama ananichanganya tu, nimemuita tuzungumzie jinsi ya kurudisha uhusiano wa familia yangu na ya mume wangu, ananambia tena habari ya kitovu cha mtoto, mi nitajuaje, ili kumridhisha nikamwambia mama nitamuuliza dommy labda mama mkwe alimwambia kitu.

Tuliongea habari zingine na mama akaniaga na kuondoka, alichonisisitiza ni kusali kama familia jinsi nilivyolelewa. Nikamuitikia na kumshukuru kwa kuja kunitembelea na kunisikiliza. Mume wangu alirudi kazini, baada ya kula na kupumzika pamoja chumbani nikaona ni muda muafaka nimuelezee kua mama alifika hapa nyumbani mchana, na pia nikamuelezea Kwa kifupi lengo la mama kufika. Nikamwambia najisikia vibaya kwa yanayoendelea yeye kujitenga na familia yake sababu yetu, maana hata mtoto wa pili hamjui bibi wala shangazi.

Mume wangu aliniangalia kwa upendo akanambia,wife...najua una umia sana, Mimi naumia zaidi, umelelewa vema na ndio sababu iliyonifanya nikakuoa mama...nahitaji hayo malezi wayapate wanangu, kuhusu familia yangu sitoweza kuzungumzia, na nakuomba usije kumpigia mama...nipo hapa nitawalinda hadi siku yangu ya mwisho.

Nikamueleza kuhusu mama kuulizia habari ya kitovu cha mtoto, mme wangu alishtuka sana, akanambia mama anajua nini kuhusu kitovu, nikamwambia ameniuliza kua kilihifadhiwa vipi, nami kumbukumbu zangu zinanijia kua nilimpatia mama mkwe...mme wangu aliinama chini aliponyanyuka akawa ameloana na machozi uso mzima...nikamuuliza mbona sikuelewi baba? Akanambia umemuua mtoto grace, umemuua...

Sikuelewa chochote, sikujua natakiwa kusema nini na kwa wakati ule, kumuona mwanaume wangu naemuheshimu sana akilia kama mtoto iliniumiza sana, nikamkumbatia kwa upendo mnooo...nikamwambia am your wife, I think it's time I know what is real going on...aibu yako ni yangu na yangu ni yako...sisi ni mwili mmoja baba...Just tell me...

Akanambia nahofia utaniacha, nikamwambia kama kukuacha ningekuacha ile siku napata ufahamu hospitali na kuambiwa niliugua ukichaa kwa miaka miwili mfululizo na hakuna ndugu ako hata mmoja aliekanyaga hospitali, hadi sasa wewe ni fungu langu, nambie...Dommy akanishika mikono miwili na kuanza kunambia simulizi ya kuogofya mnooo....nikiri tu mimi sio mpenzi wa filamu za kutisha, na kwanini niangalie filamu jicho moja ilhali kuna love films za kutosha tu na zingine nyingi za kupendeza.

Dommy anasimulia....

Nakumbuka nilikua darasa la tatu, babangu mpendwa alianguka ghafla wakati tunapata chakula cha usiku, nilikua mtoto pekee kwa wakati huo, mama alipiga simu wakaja ndugu wa baba waliokua karibu....sifahamu nini kiliendelea lakini kesho yake nyumbani palijaa ndugu wengi waliotoka sehemu mbalimbali...ninachokikumbuka hadi sasa na utoto wangu ni hekaheka zisoisha, kuchanjwa chale na kulishwa madawa ya kila namna...mama hakua na usemi maana ndugu wa baba walikua wengi mahala pale.

Nadhani ndio siku iliyotoka utaratibu maalumu jinsi ya kuadhimisha siku zetu za kuzaliwa, nikaja kufahamu baadae baada ya kukua kua marehemu baba baada ya kutoka masomoni ulaya na kumuoa mama hakutaka kujishughulisha na mila hizo, Sasa mambo yamewazidia na kulikua hakuna namna tena. Baba na mama walikubalina kuadhimisha mila za mizimu maana kwa kucheleweshwa huko ingeondoka na uhai wa baba na uzao wake wa kwanza.

Tumekua tukifanya hivyo kwa miaka mingi, na ndio maana palikua na utulivu, na ndio sababu ya sisi sote kusoma shule za kutwa tena ndani ya mkoa wa dar ili iwe rahisi kufanya matambiko...Grace nisamehe sana, hii miaka yote ambayo unaumwa nimejitenga nao na napambana kuhakikisha mnakua salama...Sitaki wanangu waishi kama nilivyoishi, nipo tayari nilipie gharama ya uhai wenu na tayari nimeshalipia kwa kwenda kijijini na kufanya matambiko ya kafara za wanyama, ila sitotaka kujihusisha chochote na mamangu, nahisi mama aliendelea zaidi na akifanyacho ni zaidi ya matambiko, nahisi mamangu imani ya mizimu ilimchukua sana, na baba alipogundua mama amekua mshirikina , mama aliamua kumuua baba.

Nilibaki nimeachama mdomo wazi, ni familia ya aina gani niliyoolewa nayo ?mme wangu mpenzi akanambia naomba usije kumpigia mamangu...hata akija hapa usithubutu kumruhusu kuingia ndani...nikaona huu sasa ni mtihani mwingine jamani, ni nini hiki kinanikuta grace mimi...

Kesho yake nikasubiri mme wangu ameondoka nikampigia mamangu kumueleza yaliyojiri katika mazungumzo na mme wangu,japo si heshima ila niliona sina namna...haya mambo ni mazito kuliko ninavyowaza. Mama akanisikiliza akanambia ndio maana nilikuuliza kuhusu kitovu cha mwanao, nilishaona katika ulimwengu wa roho kua mwanao hayuko salama...Grace sali sana ....sali mnoooo mwanangu...nami nakuombea lakini ulinzi kamili wa nyumba yako ni wewe...nakuonea huruma maana mama ako mkwe ni adui yako...Mungu akupambanie mwanangu.
 
SEHEMU YA KUMI:

Yalipita mawiki kadhaa, ilikua asubuhi najiandaa kutoka kwenda kwenye biashara zangu, school bus inayombeba Lameck ilikua imeshaondoka kama nusu saa hivi, dada alikuja mbio akanambia mama baba amenipigia simu anasema pokea simu yako.
Nilikua metoka bafuni kuoga, kwahiyo simu itakua ilipigwa wakati nipo bafuni...

Nikakuta missed calls kama nne za mme wangu, sio kawaida yake, niseme tu nilipatwa na mshtuko ila nikajikaza...mme wangu akapiga tena wakati najiandaa kununua salio nimpigie, nikaipokea kwa kihoro...dommy akaniuliza kama nimeshatoka nyumbani, nikamwambia hapana...nipo najiandaa, akanambia usitoke nakuja...nikamuuliza dommy mbona hivyo kuna nini? Akanambia naomba tu nisikilize mke wangu, usitoke nyumbani...

Nikakaa katika msongo wa mawazo, nikamuita dada na kumuuliza baba alipokupigia alisemaje? Dada akanambia alinambia nikwambie upokee simu...nikasema sawa hamna tatizo, nikaamua kutumia huo mda kumsaidia dada kumuogesha mwanangu wa pili, huku nikimsubiria dommy arudi, baada ya kama lisaa na nusu dommy akafika, nadhani foleni ilimchelewesha, dommy akanambia chukua mkoba na vitenge kuna mahala tunaenda, nikamwambia vitenge? vya nini tena? akanambia nitakueleza wife...hebu fanya nachokwambia .

Nikawaza tugombane kisa vitenge tu jamani, nikaingia ndani nikatoka na vitenge viwili, hao tukaingia kwenye gari na safari ikaanza...dommy hakua yule niliyemzoea , muongeaji na mcheshi, akaendesha gari kwa umakini sana hadi Amana hospitali, nikaona nivunje ukimya ....honey hospitali asubuhi yote hii tunakuja kumuona nani? mbona hunielezi vizuri...mme wangu akainama aliponyanyuka alikua ameloana machozi, akanambia nisamehe grace...nimeshindwa kwa mara nyingine kuwalinda, nikiwa katika sintofahamu nikaona gari ya nyumbani kwetu inaingia pale hospitali, baba na mamangu walishuka wakiwa wameongozana na wadogo zangu wote wawili...

Nikaona kama wananichanganya, nikataka kushuka, kwa Kasi Dominic akaniwahi nisifungue mlango, mama na baba wakaja pale tulipopaki gari, baba akafungua mlango na kuniambia grace ....pole mwanangu kipenzi...mama akanichukua hadi nyuma ya gari, akanifunga vile vitenge style ya kinyakyusa, kitenge kikakazwa tumboni...mama akanambia nisamehe grace...sikusimama vema katika kuombea ndoa yako kabla hujaolewa, nisamehe mwanangu...

Nikamwambia mama, wewe ni mamangu mpenzi, naomba uniambie nini kimetokea....mama hakujibu kitu akanikumbatia kwa upendo akanambia atakwambia mmeo...dommy akaja akanambia twende tukamuone mtoto...
Nikapatwa na kama mshtuko wa ghafla, mwanangu ameondoka asubuhi na school bus, mwingine memuacha na dada , huyu naekuja kumuona Amana ni yupi? Baba na mama wakazidi kuniambia nijikaze...

Tukaingia ndani hospitali, badala ya kuelekea wodini tukaelekea upande wa mochwari, nikasimama kwanza, nikawaambia ...hata kama mwanangu yupo hapa, ndio awe huku? hebu acheni masikhara jamani..
Nikaanza kuita jina la Lameck kama mtu aliechanganyikiwa, baba na mme wangu wakashauri nirudishwe kwenye gari, nikarudi pamoja na mama, sikua na nguvu nikakaa chini kwanza.

Nikamwambia mama, mnanikosea ....naomba uniambie kilichotokea, mama akanambia niahidi utakua mtulivu grace, nikamwambia naahidi mama...akanambia gari ya shule aliyopanda Lameck imetumbukia mto msimbazi, watoto kumi kati ya 40 waliokuwepo wamefariki hapohapo kwa kunywa maji, watoto wengine wamesombwa na maji...tupo hapa kuweza kutambua mwili wa Lameck...wewe ni mama unamjua vema mwanao katika hali zote, maiti zimevimba sababu ya majeraha na kunywa maji mengi...jikaze uweze kumtambua mwanao....

Huwezi amini sikuweza hata kulia, nilimuangalia mama nikamwambia twende huko kwenye utambuzi , mama akiwa bado hajaamini kama natumia akili yangu ya kawaida au wazimu umenirudia , akashangaa nimeshanyanyuka na kuelekea walipoelekea baba na Dommy.

Mtoto wako uliemuweka miezi tisa tumboni ni wako jamani...ile bond ni ya ajabu sana, nilizipiga hatua kama kichaa, mama alikua anafanya kazi ya kunikimbiza, mamangu ana mwili kiasi, nilimtesa sana ile siku...
Nikafika huko mochuari , mlangoni nakutana na baba na Dommy, wananishangaa nimefikaje pale,.mara wakamuona mama anakuja mbiombio, mama akafikia kukaa kwanza...

Nikamwambia dommy nipeleke nikamuone mwanangu,dommy akanambia hawajamuona labda atakua katika wale waliondoka na maji, nikamwambia mwanangu yupo hapa nipeleke ...baba akamwambia sawa acha aingie na yeye akaangalie...niliingia ndani, masikini vitoto vyote kumi vilikua vimehifadhiwa sakafuni...vimefunikwa na mashuka ya hospitali, wakasema wameshindwa kuwaweka kwa majokofu ili kurahisisha zoezi la utambuzi, nikapiga jicho moja tu, nikagundua alama ya weusi kwa mbali chini ya jicho la Lameck..mwanangu mpenzi alikua amelala pale chini, mwanangu, malaika wangu alikua amelala pale chini bila uhai...oh dear Lord...
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…