Simulizi: Kwako Sikujua wangu

Simulizi: Kwako Sikujua wangu

Tajiri Mapesa

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2020
Posts
707
Reaction score
742
Kwako sikujua wangu,

Sikujua mpenzi wangu wa jadi,wa zamani,Leo hii nina mengi yakukujulisha ,naomba dakika zako chache.Nisikilize,nakuahidi sitachukua,sitakuyang’anya mda wako.Nimeandika barua hii,kama nimelewa chopi ,ulisema niwache pombe ,samahani sana ,ulivyoenda,ulivyoniacha mimi na moyo wangu,pombe alinipa kufua,MTO,paja LA kulaza USO wangu. Sikujua ,usisisitishe kusoma,endelea tafadhali.

Sikujua, hivi majuzi nimekuona na mwanaume wa ndoto zako,wa maisha yako,mtanashati,mcheshi,mweledi wa mapenzi,mfalme wa mapenzi.Yakushangaza mwanaumehuyo si mimi.Niliumia sana lakina sikua na budi ,mwanaume nikuvumilia,mwanaume kamili halii,ungekua karibu nami,ungeona machozi yakitengeneza mifereji miwili usoni mwangu.Laaazi,najua moyoni unaimba nyimbo fulani ya bushoke…”Leo nimepata barua kutoka kwa mpenzi was zamani, anasema eeeeh,amelimisi mapenzi yetu ya zamani…Ni yuleyule aliyetesa moya wangu”Kweli nalimisi penzi letu LA zamani.

Sikujua bado nakumbuka siku ya kwanza macho yangu kutua machoni mwako,siku ya kwanza hapo zamani kidogo,siku ya krisimasi,kanisani, nilipoigiza kama Joseph wewe ukaigiza kama Mary,tuwe wazazi wa mkombozi wa dunia.nilijua Mungu,Mola wa mbigu na nchi katupangia maisha,sijua mambo yalienda kinyume na yalivyo pangwa.Ulisema unanipenda ,kwa sauti ya ulegevu,nyororo,nyepesi uliyonifanya niishiwe na nguvu,tukiwa darasa la sita,ukasema tutajenga nyumba ya kifahari kama ile ya king Solomon, ukasema tutazaa watoto wengi,tano sita saba nane….Ukanitizama machoni ,ukanisongelea,huku Mimi sijiwezi,nahema jujuu kama mgonjwa wa pumu.Ukanipa bus u LA kishua,busu LA pinki.Nilihisi moyo ukitaka kupasuka katikati kwa msisimko niliouhisi.Siku hiyo usiku sikulala,akilini ulikua ni we wewe…Sikujua mapenzi,ni nini,,ulianiahidi kunifunza…

Sikujua ,usilie.Bado subiria zijamaliza.Nikaanza kujua mapenzi,mahaba yakanijaa,nikawa mweledi ,jemedari wa mapenzi,mfalme wa mapenzi,nilikupenda,tukapendana.Sijua kwa nini nasema haya yote,Jua nimelewa ,usinikasirikie,,nimebugia lori mzima ya whisky,

Naaandika huku machozi yakiriririka kitabuni ,mate ,jasho,yakivuta wino wa buluu,ninaotumia kuandikia barua hii,itakuuimiza ,utaniwia radhi .

Sikujua,vile ulivyoniacha ndo vle nko,ila nimebadilika kidogo,pombe nabugia nyingi,naandika kama sitawahi andika tena,nimekondaa zaidi ya sindano,nimeishiwa na machozi siku hizi huwa silii,,kalamu inalia kwa niaba yangu.

Natumahi unaye sasa ,anakupenda kutoka moyoni,zaidi yangu.Ni mchesi, anajua mapenzi ,hakupigi hakutesi,ameshakupa watoto,anakupa unachotaka na mwisho anakuheshimu.Msalimu, kweli anabahati he is lucky,mwambie hivyo.Harusi ikiwa mnialike,ntawatungua shairi taaamu ya harusi yenu.Kwaheri

Wako akupendaye kwa dhati,
Masumbuko.
 
Tatizio ni kwamba haukujua,
Ila ss unajua.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom