Mr Acky
JF-Expert Member
- Nov 24, 2019
- 234
- 313
KISANGA!!!
(Hisia za Mrithi)
Mtunzi: Akida Siri Rambao
Contact: 0658328596
Email: akidasiri@gmail.com
MSIMU WA 1
NCHINI ZHONGO
SEHEMU YA 1A
KITONGOJI CHA NYAKWA-WILAYA YA CHOZI
Sauti yenye mchanganyiko, isiyoleweka uhasilia wake si me si ke iliendelea kupita masikioni mwake, ina himizo kuu! “Gotwaaaa! Gotwaaaaa! Gotwaaaa!” ikipambishwa kwa mtetemo wa mawimbi, dhahiri ya ushawishi kumvutia sana kiasi cha kutupilia mbali woga, ujasiri kifuani yu katikati ya mlango akijishauri kuingia au la! Macho akiyapeleka huku na kule, hatua mosi pili ikafata macho ya kutafuta . Chumba au ghala!?
Hakuwa na mpangonayo yu makini akitafuta amuitaye. Huyo kwa hamu ya kujua asiyoyajua tahadhari kiduchu tama kiloba mpaka kwenye kabati kubwa la kioo. Ni kama aliyekuwa akielekezwa cha kufanya! akachutama na kuvuta droo hapo hapo sauti ile ikakoma. Sasa macho yakawa juu ya karatasi iliyofubaa iliyokunjwa kunjwa.
Alibaki kuitazamakwa jicho la tama uzalendo ukamshinda akaishika na kuitoa. Kitendo cha kuitoa karatasa tu nyuma yake wakazuka watu wawili wanaume wazee wa makamo na mavazi yao ya kale kwa pamoja wakastaajabu sura zao zikionekana wazi kushangaa “Nani aliyetuita hapa tulikuwa kwenye mapumziko ya kadri!” mmoja alisema sasa akijinyoosha viungo ihali ni mtu aliye na uchovu mwenzake wakati wote yu kimya tuli lakini mwenye uduwanzi macho katumbua akimkodolea Gotwa, mtu huyo akaanza kupiga hatua akimfata kwa nyuma mwenzake akiwa nyuma yake akimtazama bila kusema neno .
Ni kama Gotwa alihisi kitu maana aligeuka na kutazama upande ule alipo bwana huyo aliye hatua chake toka kwake “Nimesikia kitu…” alijisemea akitazama huku na kule “Lakini nimesikia mtu akiongelea huku” alisema tena na kuwafanya watu wale waliozuka kutazamana kwa mshangao.
Gotwa akapuuza na kurudisha macho mikononi na kuanza kuikunjua, akamaliza, macho yakagandia karatasini yakizunguka kwa mtindo kukagua karatasi hiyo fifi-fii si nyeupe si manjano pau pau! ikiashiria mvua nyingi zilizowahi kupita tangu kucharazwa na kalamu ya wino. Ikiwa na hati ya kipekeee sana hati ya mlalo na maadishi yake ya bluu nyeusi iliyofubaa akatabasamu huku akiitazama vizuri karatasi hiyo ikimshawishi kuisoma “Mwandiko mzuri” alijisemea na kutabasamu.
Viumbe wale wawili wasiojulikana waliko toka mmoja akiwa na tabasamu lakini mwengine akiwa na jazba iliyosomeka machoni mwake waliungana kumtazma Gotwa kwa hamu ndipo Gotwa akaanza kuya soma maneno yale kwa sauti ya kunong’ona pasina Gotwa kuwaona hali ya kuwa walikuwa karibu yake, Ajabu!
“Huyu ndiye mama wa wote, ndiye anaye lisha kote-kote, anachoambulia ni mashuka kukuuu, vitamu-tamu, ving’ao-nga’o, na naniliu…!!! akiahidiwa hivi na vile baada ya kile na yale, eti Utandawazi! Kichwa dafu si nazi ya tui, hovyo kuliko kichwa panzi!!!. Mwenyewe anafurahiii akiimba, kucheza-cheza akiiota ndoto ya ngekewa isiyofika, isiyo na nyenzo! Mwee!
Mama huyu kapotea na hataki njia, ana macho haoni masikio yana ntap hasikii ya muhazini wala mkimu swala.
Anavaa na kula makombo, wakati jiko ni lake sufuria yake vyote vyake, asili yake ni kwake. Alishawapenda mahaba yake yote, kwetu ni kinyaa! Sijui ni kulogwa na sangoma!? Wakilia tu roho itampasuka huyo atahaha kanga kiunoni akienda akinung’una atabeba hiki na kile na kuwapa. Tazama! anawaabudu?! kana kwamba hajawalea na kuwahudumia mahitaji yao walipo kuwa watupu, yu kipofu. Huyu mama vipi!??
Tunajua ukweli wake si watoto wake ni wa kuwalea hawafanani mwendo, rangi wala pua hajulikani baba yao, ni wavamizi! Anawatoto wa kuwazaa walio wema sana kwake, watoto wa tumbo lake na ziwa lake! Uchungu wa mwana ni wa mlezi? Na si mzazi? Mhh ajabu ya karne?!
Loo! Sisi masikini ni mkia wa mbuzi tutafanyaje wakati tumboni hatufiki sembuse kifuani!!!!? Sasa katugawa tu wazuri tu makatili, tuwachoyo tu wahisani hatupendani kama zamani, katikati dosarini fitinani hasadini hatujuani mgeni yu thamani mwenyeji yu jikoni! ni zambi ya nani?! ya mama au ya wana au ya jirani!!? Huyu ndio mama yetu! Zumbukuku."
Alipo maliza kusoma mapigo ya moyo yakaongezeka kasi maradufu, hofu?!
Itaendeleaa.....