kalamu na karatasi
Member
- Jul 26, 2015
- 49
- 30
Simulizi Fupi:AHSANTE
Mtunzi:kalamu na karatasi Foundation
Mawasiliano:
Simu:0655 08 02 90
Barua Pepe:kalamunakaratasi@gmail.com
Mmmh Acha Leo hii nikueleze MANENO haya mke wangu Asali wa Roho
Kila napoyatazama Macho yako kwa namna yang`aavyo ,Nazidi kupata kile ambacho kinasema na kutoka dhahiri Moyoni Mwako. Kwani Safu ya midomo mizuri yenye meno ilojipanga Vyema na Tabasamu unoliachia navyo Vyazidi kulidhihirisha hili Mke wangu Kipenzi.
Nina kila sababu ya kukushukuru na kukupongeza kwa Uamuzi wako Makini Uliouchukua,Kwani ni zaidi ya kujitoa Muhanga kwa hili uliloamua kunitunukia kama Zawadi Ya Pekees.Ni lipi Mpenzi wangu zaidi ya kukubali kuolewa nami tena kwa Moyo Mkunjufu uso na SHAKA Yeyote .Nikwambie tu Ahsantee sanaaa
Ahsaante kwa kuninyanyua pale ambapo wengine walinidondosha huku wakinipita tena bila hata kujali lolote lile.Ukaenda mbali kwa kuniwekea Dhamana katika Mahakama ya Moyo wako,Kuwa Siku zote utakuwa nami kwa hali Yeyote Ile.Ahsante Mke WANGU
Shida zako ziwe zangu,RAHA nazo tugawane,Majabali na Milima tuyapande na Kuyashuka kwa Pamoja.
Siku ile nililia,Nililia kilio ambacho Machozi pekee yalishuhudia kilichopo Moyoni hata yakaungana nao kwa kuamua kutiririka pasi na Kificho chochote kile.Pamoja na Yote sikusita kumwambia Mwenyezi anijaalie Yule ambae atanijali,nami nitamjali,ataniheshimu nami nitamuheshimu,atanilinda na kunithamini,nami nitamlinda na kumthamini.Hivi ni Nani huyo? zaidi yako Barafu wa Moyo wangu.
Mwanamke uliyesimamia na kuwa Mshauri Mkubwa katika Kila Jambo nililokueleza na hukusita kuliboresha ima kwa kuongeza ama kulipunguza ili mradi tu lipate au kufikia Vile ambavyo tulitaraji liwe.Ahsante Asali wa Moyo wangu.
Asali wa Moyo,ulokubali kunilelea wanangu,Pamoja na adha na usumbufu mkubwa unaoupata toka kwao lakini bado ungali Mama na Mlezi Bora kwao.Nini nikulipe katika hili Mke wangu.
Mke ambae unaniheshimu nikiwepo,na hata pale nikosapo katika Mboni na Upeo wa MACHO yako,BADO ningali na hadhi na thamani ile ile kwako .
Wakasema waneni wanenao yenye kunenwa na kuneneka,Kuwa Chanda Chema huvikwa Pete na Mti ULO na Matunda Siku zote ndo hupigwa Mawe Nakiri kweli husemi huu..Kwani ni zaidi ya WANAUME alfu walokuwa wakihitaji Nafasi hii ya kuwa nawe .Lakini Tazama Leo hii Mimi tu Ndo Mume halali kwako,Nakula na kufaidi kila kizuri ulichonacho Wee swity !Wee!
Mke wangu,Nikisema kuna neno zaidi ya Ahsante ambalo laweza toka Kinywani mwangu kuja kwako kuonesha jinsi gani nakupenda,nitakuwa nakudanganya.Japo nataka utambue kuwa nakupenda tena sanaa..Na sioni tabu kwa lolote la halali kuliendea ili mradi tu mimi,nanyi Familia Yangu Mfaidike na Kuishi Vyema huko Mlipo.
Mimi nakupenda saanaaa Mke na Mama wa Wanangu Faraja ya Maisha Yangu..Dira na Mwongozo sahihi Niliuchangua kwako Mke wangu Kipenzi.
Moyo wangu utatulia zaidi kama utakaa na kuusoma Vyema Ujumbe huu ambao kwa Usiku Kucha Nimekaa na Kuutunga Kwa ajili yako Mpenzi wangu.
. Nakupendaa Saanaaa ..
Unaweza pia kuupata Ujumbe huu kwa Njia ya SAUTI kupitia Whatsapp au Barua pepe
Pia waeza toa maoni yako kuhusu Utunzi huu kwa ku ni Pm
au
Mawasiliano
Andika Neno JF Acha nafasi Kisha Ujumbe wako,au Kama unahitaji kutumiwa Andika neno JF NITUMIE,Kisha tuma kupitia
Simu nambari :0655 08 02 90
Au
Barua pepe;kalamunakaratasi@gmail.com
Kalamu na Karatasi
(Chanzo Cha Maarifa)