Shunie
JF-Expert Member
- Aug 14, 2016
- 157,076
- 463,978
Mtunzi Ally Katalambula
Sehemu ya 1
“MWANAUME kutokwa na machozi, iwe kwa sababu ya maumivu au majonzi, si kitu kinachokubalika katika ukoo na kabila letu.
Ukiona mwanaume analia ujue ana roho ya kike. ukilia, huna sababu ya kuvaa kaptula ama surual,vaa gauni au sketi, machozi ya mwanaume yanatakiwa kuwa adimu sana, mwanaume kutokwa machozi ni udhaifu wa kiwango cha mwisho.
” Ni maneno ya marehemu baba yangu, niliyakumbuka nikiwa katika madhila makubwa sana, donge zito lilikuwa limenikaba kooni, uso wangu ulikuwa umechafuka kwa mikunjo iliyotokana na na hasira iliyochanganyikana na simanzi kubwa.
Nilikuwa nimejiinamia mkono ukiwa shavuni, maungo ya mwili wangu yalikuwa yakivuja jasho kama mgonjwa wa homa kali, macho yalikuwa mekundu kama mtu aliyeingiliwa na pilipili
machoni, kila wakati nilikuwa nikiachia msonyo mdogo, huku nafsi yangu ikijilaumu yenyewe. Kwa mara nyingine, nilinyakua simu yangu ya mkononi iliyokuwa kando na kupiga namba fulani. Namba niliyokuwa naipiga, nilikwisha ipiga kabla, zaidi ya mara kumi na moja bila mafanikio. Simu ilipokuwa sikioni, mapigo yangu ya moyo yalikuwa yakinienda kasi kuliko kawaida. japokuwa haikuwa mara yakwanza kuipiga ile namba, ila safari hii nilikuwa na presha kubwa.
Baada ya muda fulani kupita, majibu kupitia simu ile nikayapata: “…namba ya simu ya mteja unayempigia haipatikani kwa sasa...” Nilikata simu baada ya kupokea ujumbe ule.
Donge zito likaendelea kunikaba kooni, wivu na hasira vikaendelea kutanda moyoni mwangu, kwa mara nyingine nilijikuta nikisaliti ujasiri niliofundwa na baba yangu. Machozi yakanibubujika!.
“Kwanini unanifanyia hivi Nasra...kwa nini...Iweje jambo hili lifanywe na wewe!. haya ndio malipo ya pendo langu? Kosa langu ni kukupenda si ndivyo....nini maana yake hii sasa….Eeh!!..” nilinong’ona kwa fadhaa huku machozi yakinitoka.
Kwa mujibu wa saa yangu ya mkononi ilikuwa ni saa sita na nusu usiku, nilichukua pakiti ya sigara na kutoa mche mmoja na kuupachika mdomoni, nikawasha kwa kiberiti cha gesi ambacho kilitoa mlipuko mdogo wa moto, nikaunguza ile sehemu mbele ya sigara.