Simulizi: A spy and assasin in love

Simulizi: A spy and assasin in love

kahawatime

Member
Joined
Dec 21, 2025
Posts
5
Reaction score
1
Hii ni hadithi inapatikana katika app yetu ya kahawa time A SPY AND ASSASSIN IN LOVE - Continue Reading on Kahawa Time ikiwa imeandikwa na mwandishi wako mkali EDDAZARIA G. MSULWA ntakua napost hapa ila tayari hii hadithi imefika mbali huko kwennye app

A SPY AND ASSASSIN IN LOVE 01 MUANDISHI
……………………………….
EDDA ZARIA G.MSULWA WASILIANA NAMI
……………………….0657072588(WHATS APP)/0746787302 @StoryZaEddytz
…………………………

FACEBOOK, INSTERGRAM, TWITTER NA YOUTUBE ANGALIZO: KAMA UPO CHINI YA UMRI WA MIAKA 18. TAFADHALI USISOME HII HADITHI. KILA KILICHO ANDIKWA KATIKA HADITHI HII NI UTUNZI HAKIENDANI NA KISA CHOCHOTE KILICHO WAHI KUTOKEA MAHALA POPOTE ASANTE
****************************************** ****************************************** *

“Hei mambo”

Denzel alimsalimia msichana mrembo aliye kutana naye katika ngazi za kordo ya gorofa analo ishi. Msichana huyo hakumjibu chochote zaidi ya kupandisha ngazi kwa haraka na kukimbilia gorofa ya nne ambapo ndipo Denzel anapo tokea.

‘Mmmm!’

Denzel aliguna na akaendelea kushuka katika ngazi. Akafika gorofa ya chini na moja kwa moja aelekea alipo egesha gari lake huku kila mtu aliye panga katika gorofa hilo ana eneo lake la kuegesha gari lake. Akatoa simu yake mfukoni na akafungua link ya ramani aliyo tumiwa katika simu. Akawasha gari lake aina Toyota Vitz new model na akaondoka katika makazi anayo ishi huku mlinzi wa eneo hili akimfungulia geti. Akaifwata ramani iliyo mtoa nje ya mji.Akafika katika nyumba iliyo katika shamba kubwa la miembe. Kabla yakushuka ndani ya gari lake, akavaa kofia nyeusi, pamoja na barakoa yenye rangi nyeusi. Akaingiza mkono chini ya siti aliyo kalia, akatoa bastola yake, akaifunga kiwambo cha kuzui sauti kisha akaichomeka kiunoni mwake kwa nyuma na ikashikiliwa vyema na mkanda wa suruali yake. Akachukua gloves mgumu za rangi nyeusi, akazivaa na akashuka ndani ya gari. Akatembea hatua kumi ana tano na akasimama mbele ya mlango wa nyumba hiyo. Mlango ukafunguliwa kabla hata hajagonga.

“Nyoosha mikono”

Mwanaume amrefu aliye jazia misuli yake alimuambia na akatiaa amri hiyo. Akampapasa na akaichomoa bastola ya Denzel kiunoni mwake.

“Ingia”

Denzel akaingia ndani ya nyumba hiyo.

“Nifwate”

Mwanaume huyo alizungumza na akaongozana naye, akaingia naye ndani ya chumba kimoja ambacho kina ngazi za kuelekea katika chumba kingine kilicho jengewa chini ya ardhi. Wakashuka katika chumba hicho na akakuta wanaume wanne wakiwa wamezunguka meza moja huku wote wakionekana kumsubiria yeye kwa hamu.

“Denzel my men”

Mwanaume mmoja mtu mzima wa makamo alizungumza huku akinyanyuka na akasalimiana na Denzel huku wakikumbatiana.

“Za masiku”

“Salama mzee shikamoo”

“Marahaba. Karibu sana ukweti”

Denzel akaka kwenye moja ya kiti huku akitazama sura za wanaume watatu huku aliye msindikiza akiwa ametoka ndani ya chumba hicho.

“Kuna kazi moja na muhimu tuliyo kuitia ili uweze kuifanya”

“Kazi gani”

“Kuna kiongozi mmoja mkubwa tuna hitaji upite naye”

“Nani na lini?”

Mwanaume mmoja ambaye muda wote yupo kimya. Akatoa picha katika mfuko wa koti lake na akamsogezea Denzel picha hiyo. Akaitazama na kumtazama mzee ambaye ana fahamiana naye wazee wengine watatu akiwa hawatambui.

“Raisi”

“Ndio”

Denezel akatabasamu.

“Toka inchi hii ipate uhuru hakuna raisi aliye madarakani aliye wahi kuuwawa. Hii kazi ni sawa kuvuta sigara pembeni na tanki la petroli.”

“Una iweza kazi au huiwezi?”

Mzee aliye itoa picha hiyo aliuliza huku akimtazama Denzel usoni mwake.

“Kazi ana iweza ndio maana ndio maana nikamuita. Wenyewe mumeshindwa kuifanya hii kazi ndio maana mukanitafuta niwatafutie mtu wa kuiamilisha kama mungeiweza musinge kuja kwangu.”

Mzee huyo alizungumza kwa ukali na kuwafanya wazee hao kukaa kimya.

“Denzel hii kazi ina pesa nyingi sana. Kinacho hitajika ni risasi yako moja tu ili kuondoa maisha yake”

Denzel akajifikiria kwa sekunde kadhaa.

“Bei yake”

“Watalipa dola milioni moja. Ni zaidi ya bilioni mbili za nchi yetu. Hii ni pesa kubwa sana tofauti na pesa zote ulizo wahi kulipwa kwa kazi ulizo wahi kufanya”

“Lini?”

Denzel aliuliza.

“October kumia.”

Mzee mmoja alizungumza.

“Wiki mbili kutoka leo?”

“Ndio.”

“So nitamfwata ikulu au?”

“Hapana. Tarehe kumi hiyo ata fanya kampeni ya za kugombania tena uraisi katika mkoa wa Dar es Saalam hivyo tuna hitaji hiyo siku iwe ndio siku yake ya mwisho kuishi”

Mzee aliye toa picha alizungumza huku akimtazama Denzel ambaye baada ya sekunde kadha akayahamishia macho yake katika picha ya raisi aliyo ishika kwa mkono wake wa kulia.

“Endapo ita tokea nika kamatwa?”

“Hatuto juana. Wewe na sisi tumeonana leo na hatuto onana tena baada ya leo”

Denzel akatabasamu huku akimtazama huyo.

“Hii ni kazi ya siri sana ndio maana tumeitoa nje ya mfumo wa vyombo vya ulinzi na usalama”

“Denzel hii pesa ni nyingi sana. Ina badilisha mfumo mzima wa maisha yako.”

Mzee anaye fahamiana na Denzel alizungumza.

“Sawa nita ifanya ila kwa sharti moja”

“Sharati gani?”

Mzee aliye toa picha alizungumza.

“Sihitaji kuwe na muuaji mwenine tofauti na mimi. Na endapo kuta kuwa na muuaji mwengine na akajaribu kuniua baada ya kukamilisha hii kazi tambueni nita muua yeye kisha muta fwata ninyi na sio ninyi peke yenu. Bali muta kufa na wapendwa wenu. Hivyo ndiyo nifanyavyo kazi zangu”

Wazee hao wakatazamana.

“Anacho kizungumza ana maanisha”

“Tumekuelewa kijana. Tuna weza kufanya malipo ya awali hivi sasa. Tuna cash dola milioni mia tano”

“Sipokei cash”

Wakatazamana.

“Ndio maisha yangu ninayo ishi ni tofauti na kiasi cha pesa ninacho miliki. Kazi ninayo tambulika nayo ni tofauti na kazi hii ninayo ifanya hivyo kama ni malipo yote fanyeni kwa njia ya akaunti yangu”

“Kululipa kwa akaunti iliyopo hapa Tanzania huoni kama ni jambo hatari”

“Sijawaambia ni akaunti ya hapa Tanzania. Andika akaunti namba yangu,”

Mzee mmoja akatoa simu yake na akaiandika akaunti namba ambayo Denzel ana mtajia.

“Hadi usiku niwe nimepokea asilimia sabina na tano ya malipo ya kazi hii”

“Hayo sio makubaliano. Tuna kulipa nusu kisha baada ya hapo tuta kulipa nusu”

“Tafuteni wa kuwafanyia hii kazi. Sifanyi kazi kutokana na masharti ya mteja. Ila nina fanya kazi kutokana na utaratibu wangu nilio jipangia”

Denzel akanyanyuka na kumfanya mzee anaye mfahamu kumshika mkono.

“Sawa tuta fanya hayo malipo ya asilimi sabini na tano”

“Katika milioni moja asilimi asabini na tano ni dola kaki saba na nusu si ndio?”

Denzel alizungumza.

“Ndio”

“Sawa.”

“Tuna shukuru kwa muda wako tuna omba tuondoke”

Wazee wote wakanyanyuka na mwenyeji wa Denzel akawasindikiza hadi nje na wakaingia katika gari lao na wakaondoka mzee ambaye ni mwenyeji wa Denzel akarudi nadani ya chumba walicho muacha Denzel.

“Ni kina nani hawa?”

Swali la Denzel likamfanya mzee huo kukaa katika sehemu aliyo kuwa amekaa awali.

“Ni viongozi fulani fulani ndani ya vyombo vya ulinzi na usalama”

“Kwa nini wana taka kumuua raisi wa sasa?”

“Denzel kuna mambo katika ulimwengu wetu wa mauaji hatupaswi kuhoji sana. Tuna paswa kupokea kazi na kukamilisha kazi. Sababu za wao kutaka kuuaana sisi hatupaswi kujua. Kumbuka sheria namba tano niliyo kufundisha”

Mzee huyo alizungumza huku akimtazama Denzel.

“Sawa babu nimekuelewa”

“Nashukuru. Hako kagari kako mbona kamechoka. Fanya ubadili gari”

“Labda nikapeleke kupawa rangi ila kukabadili ni uongo babu”

Denzel alizungumza huku akinyanyuka na kumpa babu yake picha ya raisi.

“Denzel kazi hii ni ngumu sana. Ila nimeipokea kwa sababu najua una weza kufanya kazi kama hizi. Usiniangushe mjukuu wangu”

“Usijali babu.”

“Nikuandalie kahawa uipendayo”

“Itakuwa ni jambo zuri sana babu. Leo mwili wangu haujachangamka”

Wakatoka ndani ya chumba hicho na moja kwa moja wakaelekea eneo la jikoni. Denzel akatazama maeneo ya jikoni walipo. Ni maeneo ambayo ameyazoea kuyatoa toka utotoni mwake. Mzee huyo akaendelea kuandaa kifungua kinywa hicho.

“Marehemu mama yako alikuwa ana penda sana kunywa hii kahawa. Kipindi alipo kuwa na ujauzito wako, japo ilikuwa ni hatari kwake kunywa kahawa ila alipendelea kunywa sana kahawa hii na ili nafsi yake imtulie, nilipaswa kumtengenezea”

“Babu”

“Naam”

“Au basi nimesha kuuliza sana juu ya hili swala”

“Kuhusiana na baba yako?”

“Ndio”

“Nimetumia juhudi zangu zote kwa kipindi chote ambacho umeishi, ila sijafanikiwa kujua baba yako ni nani na yupo wapi. Kazi ya mama yako ilikuwa ni kazi ya usiri sana”

Denzel akakaa kimya.

“Ila nakuahidi kabla sijakufa mjukuu wangu nita jua nani ni baba yako”

“Haina haja ya mimi kumjua tena babu”

“No una haki ya kumfahamu.”

“Kwa nini uliwatajia jina langu halisi wale watu?”

“Kazi hii hadi kunifwata walihitaji mtu ambaye amenyooka. Nikawaambia kwa mimi nilisha stafu hivyo mjukuu wangu ndio amechukua nafasi yangu. Nisinge wadanganya kwani wengine pale nina fahamiana nao toka miaka mingi ya nyuma hivyo nilipaswa kunyooka kwenye hili”

“Una waamini?”

“Sheria namba moja. Usimuamini mtu yoyote.”

Denzel akatabasamu kwani babu yake amekuwa ni mtu wa kishi katika mifumo ya sheria anazi jiwekea. Sheria ambazo amekuza nazo Denzel hadi kufika umri wa miaka ishirini na saba.

“Bado hujapata mwanamke wa kuoa?”

“Ahaaa…..una jua wanawake wa sasa ni kipenge babu. Wengi wamejawa na unafki, wengi wana mpenda mtu kutokana na mafanikio yake au kazi yake. Sijaona mwanamke sahihi hadi sasa hivi wa kumuoa”

“Sawa kama hujapata wa kumuoa, ila vunja kiapo chako. Tafuta mwanmke mbebeshe ujauzito. Kabala sijakufa nataka kuona walau kitukuu. Hata nitakapo kufa na kupata bahati ya kukutana na marehemu mama yaoko nita muadithia muonekano wa mjukuu wake”

Denzel akacheka.

“Babu ulinifundisha nisiwe mtu wa kuvunja misimamo yangu”

“Sawa ila haya ni maisha Denzel, sidhani kama itakuwa ni vyema kuondoka hapa duninai bila ya kuacha alama ya kuwa na mtoto”

Denzel akamtazama babu yake anaye mimina kahawa aliyo itengeneza katika vikombe vya kunywea chai. Kila mtu akabeba kikombe chake na wakatoka jikoni hapo na kukaa sebleni. Denzel akatazama picha ya marehemu mama yake iliyo bamdikwa ukutani.

“Mama yangu alikuwa mzuri?”

“Sanaaaa....Alikuwa ni binti mmoja mrembo. Amepanda hewani, ana figa namba nane. Niliumia sana binti yangu kufariki alipo kuwa ana jifungua wewe. Ila aliniachia zawaidi ya wewe, nikakulea ukiwa na siku sifuri, niliacha kila kitu nilicho kuwa nina kifanya hususani kazi yangu na nikapambana kukulea. Nashukuru MUNGU leo hii umekuwa mrithi wa mikoba yangu”

“Babu nina swali ambalo sijawahi kukuuliza”

“Niulize”

“Kwa nini ulinifundisha kuwa muuaji?”

Swali la Denzel likamfanya babu yake kupiga fumba moja la kahawa. Akatoa bastola ya Denzel aliyo kabidhiwa na mlinzi aliye mkagua na akampatia Denzel bastola yake.

“Baba na mama yangu walikuwa ni wauwaji hatari kwa kipindi cha maisha yao. Walinilea na kunifundisha kazi hiyo hadi nami nikawa ni master katika hilo eneo. Hivyo nilimfundisha mama yako na akawa na fanya hiyo kazi nawe pia nikaja kukufundisha na una ishi kwa kuifanya hiyo kazi. Sisi ni wauaji, na muda mwengine kazi zetu zina saidia kuokoa maisha ya wengine. Kuna watu ambao vifo vyao ni furaha kwa wengine kwani wamekuwa ni moja ya watu wanao waumiza wengine kwa kiburi cha uhai na nguvu walizo nazo, iwe ni nguvu ya madaraka au kiuchumi. Watu kama hao wakiwahishwa kupelekwa mbinguni. Ni nafuu kwa wengine ndio maana katika historia ya familia nzima hakuna mabaye aliwahi kukamatwa toka aanze hii kazi. Hivyo hata wewe, hakikisha hukamatwi katika hili”

“Usijali babu. Kazi ita kamilika vyema”

“Nakuamini”

“Nimeshangaa leo hii tumekutana katika hii nyumba”

“Nimependelea kufanyia kikao hapa”

Denzel akamalizia kahawa yake.

“Asante babu”

Denzel akanyanyuka na kikombe chake na akaelekea jikoni, akakiosha kama utaratibu ambao amefundishwa na babu yake toka akiwa mdogo, anapo maliza kupata chakula basi vyombo alivyo vitumia ana viosha na kuvirudisha sehemu yake.

“Babu naomba nirudi mjini”

“Sawa. Hakikisha una pata mwanmake wa kuoa”

Denzel akatabasamu. Akatoka nje ya nyumba, akaingia ndani ya gari lake, akatazama mazingira ya nyumba hiyo ambayo ameyacheza kipindi chake cha utotoni. Akawasha gari na akaondoka kwa mwendo wa taratibu. ‘Kumuua raisi ni jambo zito sana’ Denzel aliendelea kuwaza huku akiendesha gari lake. Akafika mjini na moja kwa moja akaelekea katika mgahawa anao pendelea kununua chakula chake.

“Boss karibu sana”

“Nashukuru. Nifungie kama kawaida yangu”

“Sawa boss”

Denzel akasimama eneo la kuhudumiwa huku akitazama wateja wengine wanao endelea kula na kunywa.

“Mambo”

Binti mmoja alimshtua Denzel ambaye ana onekana yupo kwenye dimbwi la mawazo

“Ahaaa poa. Mambo”

“Safi. Wewe ni Denzel yule muandishi wa riwaya ehee?”

“Ndio”

“Jamani weee kaka stori zako ni nzuri sana. Nimenunua kile kitabu chako ulicho kitoa juzi, nikizuri jamani naweza tukapiga selfie”

“Bila shaka”

Denzel alizungumza huku yeye na msichana huyo wakisogeleana na wakapiga picha kadhaa.

“Asante sana kaka Denzel”

“Nashukuru”

“Namba yako ya simu naweza kupata”

“Katika kitabu kuna namba yangu. Ila kama hujaichukua basi ngoja nikuandikie”

Msichana huyo akampatia Denzel simu, akaiandika namba yake ya simu na kamarudishia msichana huyo.

“Boss oda yako ipo tayari”

Denzel akatoa elfu ishirni katika wallet yake na akampatia muhudumu wa mgahawa, akabeba mfuko wake wenye kontena zeye chakula. Akaondoka eneo la mgahawa na akarudi eneo analo ishi.

“Khaaa nani huyu kapaki gari yake katika eneo langu?”

Denzel alizungumza kwa kukereka kwani kila mpangaji katika gorofa hilo kubwa ana eneo la kuegesha gari lake.

“Huyu ni jeuri acha nimuonyeshe mimi ni jeuri zaidi yake”

Denzel akasimamisha gari lake nyuma ya gari hilo kiasi cha kumfanya aliye simamisha gari lake kuto weza kutoa gari lake katika magesho hayo. Akashuka ndani ya gari na akaanza kuelekea katika mlango wa kuingialia katika gorofa hilo. Akakutana na mrembo ambaye alikutana naye katika ngazi, safari hii akiwa amevalia vizuri huku akinukia vyema. Akataka kumsalimia mrembo huyo ila simu ya mrembo huyo ikaita katika pochi yake na kumfanya ampite Denzel kana kwamba hajauona. Denzel akasimama huku akimtazama makalio ya mrembo huyo jinsi yanavyo tikisika.

“Nani tena kapaki kiuchafu chake nyuma yangu”

Kauli ya msichana huyo alisikika vyema masikioni mwa Denzel na kumfanya atambue kwamba gari aliyo izuia kwa nyuma isitoke katika maegesho ni gari ya mrembo huyo anaye onekana kuwa na haraka na anapo kwenda.

ITAENDELEA

Utamu umeanza. Denzel kijana muuaji aliye pewa jukumu la kumuua raisi wa nchi. Jukumu ambalo ni gumu na hatar sana katika maisha yake. Je Denzel ata fanikiwa kukamilisha mission hiyo ambayo babu yake mzaa mama ndio aliye mtengenezea mchongo huo? Usikose kufwatilia kisa hichi cha kusisimua, kuburudisha na kufurahisha. Ungana nami katika sehemu inayo fwata, sehemu ya 02
 
Ha

Haya
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom