1. In too deep - Omar Epps aliweza kujichanganya kuingia kwenye dola ya wauza madawa ya kulevya, kumbe hawakujua mwenzao alikuwa askari kanzu, wakafanya nae matukio mengi bila ya kujua mwenzao ni askari. Mwishoni wanakuja kumstukia tayari wapo chini ya ulinzi na ushahidi wote umerekodiwa.
2. Romeo must die - Hum(Jet LI) akiwa lupango nchini mwao China, mara ghafla anakuja mfungwa mpya anamletea taarifa ya kuwa mdogo wake(wa kiume) ambae alikuwa akifanya maisha yake US ameuawa. Jet baada ya kupata taarifa hizo alishikwa na hasira nyingi sana, ikabidi atoroke gerezani na kuanza safari US kwenda kuwatafuta waliomuua mdogo wake(wa kiume) ili alipize kisasi.
3.Honey - Inamuhusu mlimbwende ambae ndoto yake ilikuwa kufungua shule ya kuendeleza vipaji vya watoto wanaochipukia kwenye uchezaji(unenguaji) lakini ndoto zake zilitaka kuzimwa ghafla pale ambapo mmoja wa mapromota akataka amtumie kimapenzi ili amuinue, lakini mlimbwende alijitahidi sana kuonyesha msimamo pamoja na kuahidiwa ahadi kede kede ikiwemo kumtafutia eneo la vipaji vya watoto ili atimize ndoto zake, lakini mlimwende alijitahidi kuonyesha msimamo wake na kuachana na yule promota, pamoja yule promota alijitahidi amzibie milango ya mafanikio lakini haikusaidia