Ramlis
JF-Expert Member
- Aug 22, 2013
- 602
- 519
Wana JF ambao wametumia simu za android katika matumizi ambayo sio ya kupiga, kutuma sms na kuchati Whatsapp na FB tu, aliye tumia simu katika kazi mbalimbali kama kucheza game aina yoyote, kuchora ramani, ukiwasha data na kutumia internet kwa mda mrefu haichemki sana, ukipiga simu sauti inasikika vizuri, uimara wa betrii katika kutunza chaji nk. Tueleze ni simu ipi yenye sifa hizo ili hata mimi niweze kununua. Hapa tuzungumzie simu zenye kioo cha HD au full HD, Camera ya kupiga picha nzuri, ukubwa kuanzia nchi 4 hadi 6, internal memory kubwa, ram, OTA update nk.
Wengi tunalazimika kununua simu za tecno na itel na hizi huawei zenye uwezo mdogo maana ndo zimejaa madukani, kwenye maduka makubwa utakuta kuna zile Samsung, lg au htc zenye android 2.x.x os au matoleo ya zamani na bei yake inakuwa kubwa sana. Huku kwetu kuna duka moja tu linauza simu za Samsung galaxy kuanzia s2 hadi s4 na bei ni kuanzia million moja na kuendelea. Ukipata ya kuanzia laki tano unakuta ni clone.
Nimetumia simu za tecno sana na huawei hakuna hata moja yenye kuniridhisha, nyingi zina matatizo ambayo utayakuta kwenye simu zingine za matoleo husika.
Tecno H6.
- Inatabia ya kuchemka sana unapowasha data au unapoichaji ikiwa on.
- Ukifatilia vizuri kamera ya mbele inatoa picha nzuri kuliko ya nyuma (hii ni kwa simu nyingi za tecno)
Tecno C5/C8 ( na zenye android ya lollipop)
- Gps haifanyi kazi
- Kuna mda majina ya kwenye line yanapotea hadi uzime na uwashe tena
- Ukisave namba kwenye line inagoma au ikikubali baadae ukiitafuta huioni
- Message za whatsapp, emails, nk zinaingia pale unapofungua app husika, hii inafanya kutopokea message kwa wakati.
- Ukiwasha kamera au tochi ukatumia kwa mda kuanzia dk 10 chaji inapungua kwa asilimia kubwa sana kama ilikuwa asilimia 80 utakuta kati ya 20 hadi 35
- Kama unaichaji simu ina asilimia kuanzia 75 ukiizima na kuiwasha itakuandikia asilimia 100
- Haina factory recovery mode, akitokea mtu mwingine akaweka pattern kwenye simu yako itakulazimu kuiflash na njia hii hua inafuta IMEI namba.
Simu nyingi za tecno zenye bei kuanzia laki mbili kushuka vioo vyake havina quality nzuri. Tecno Boom J7 betrii yake inauwezo mdogo sana.
Kwa baadhi ya matoleo ya Huawei zinasumbua screen touch na kuganda ghafla, nyingi zinagoma sehemu ya Home, menyu, na back. Hata ukibadilisha screen touch unaweza ukatumia kama mwezi ikagoma.
Itel hakuna simu yenye ubora katika matoleo yao.
Kama unasimu eleza matatizo yake uliyokutana nayo ambayo ni common kwa toleo lote au ubora wake.