Simu zilizotingisha miaka ya 2000 - 2003 (Part 1)

Simu zilizotingisha miaka ya 2000 - 2003 (Part 1)

TheChoji

JF-Expert Member
Joined
Apr 14, 2009
Posts
6,551
Reaction score
20,260
Kama ilivyo kwa siku hizi ambapo kila mtu anataka awe na simu latest, hali ilikua hivyo hivyo miaka ya 2000 ambapo simu ndio kwaanza zilikua zinaingia. Zifuatazo ni simu ambazo zilikua maarufu kipindi kile na ukiwa nayo ulikua unajiona mtu wa maana sana..

1. NOKIA 1100 - Simu iliyouza zaidi katika historia ya simu duniani. Hadi sasa, imeuza nakala milioni 250! Pia ni kati ya simu ngumu sana kuwahi kutengenezwa. Miaka ile ilikua ni kawaida kukuta mtu anazo tatu au nne mfukoni..
101217_01_1100_high.jpg

2. NOKIA 3310 - Hii ndio simu inayoshikilia rekodi ya kuwa simu ngumu kuliko zote katika karne ya 21. Unaweza kuitumia kama mtwangio na bado ikaendelea kuchapa kazi.. Ndio simu ya kwanza kuja na game ya "Snake"
nokia-3310-071111.jpg

3. Sony Ericsson T28: Simu hii ndio iliyobadilisha muonekano wa simu kutoka kwenye maumbo makubwa na manene na kuleta umbo jembamba. Pia ilikua mwanzilishi wa "Flip phones" yaani simu zinazofunguka kwa mbele.. Ilikua kali sana.

T28%20Ericsson.jpg

4. SIEMENS C25: Huwezi ukawa ulikua na akili miaka ya 2000 halafu uwe hujawahi kuona simu hii.. Ilitesa sana enzi zile na kila mtu alitamani kuwa nayo.. Shuleni kwetu alikua nayo headmaster tu!

28377_320.jpg


5. MOTOROLA C200: Haka kasimu kalikuwa maarufu sana miaka ya 2003 na wadada walikamatika sana hapa.. Kaliuza nakala milioni 60.

8.jpg

6. PANASONIC GD55: Haka kasimu kalikua ni kadogo mno.. yaani hadi ilikua sida kukabeba ila kalijizolea umaarufu sana hasa miongoni mwa wadada na masista duu wa enzi zile..

GD551.jpg


7. SAMSUNG Double-screen: Hivi visimu navyo viliibuka enzi zile na kusumbua sana.. Wadada ndio walivipenda zaidi visimu hivi vilivyokua kama yai..

samsung+a500+8.jpg

8. BLACKBERRY 6230. Simu ya mwanzo kabisa kuwa na uwezo wa ku connect kwenye internet na kumuwezesha mtu kusome e-mails na mambo mengine.. Mtu wa kawaida enzi zile uliishia kuziona simu hizi kwenye muvi kwa jirani..

8MB7KEPV4UO30009.jpg

Kama uliwahi kumiliki mojawapo ya simu hizi gonga "like"
Itaendelea 2003 - 2005
 
Hapo mchina alikuwa bado hajaanza kazi.
Ila kuna mtu kaibuka juzi na kusema alikuwa anauza simu za mchina zikampa utajiri
 
Hapo mchina alikuwa bado hajaanza kazi.
Ila kuna mtu kaibuka juzi na kusema alikuwa anauza simu za mchina zikampa utajiri

Ni kweli mkuu. mchina alikua hajulikani sana enzi hizo.. vitu vilikua "jenuini"
 
umenikumbusha mbali mkuu. nilinunua hiyo motorola C200, nilitesa mtaani kwa kuonekana nina kasimu ka kijanja
 
hiyo SAMSUNG Double-screen kuna jamaa alichekesha sana,aliitamka "Samsam double screeM",basi ilikuwa ni fyongo ya msimu..
 
Kwakweli ukiangalia jinsi teknolojia ya simu ilivyokimbia ndani ya miaka kumi iliyopita utashangaa sana.. Mimi simu yangu ya kwanza kabisa kununua mwaka 2002 ilikua hii hapa..
pic_3_39.jpg
 
Hahahaha! Umenikumbusha mbali mkuu. Kwa mara ya kwanza kumiliki simu nikauziwa na wahuni wa Temeke hiyo Nokia 3310 second hand, daah ilikuwa full kucharge kila baada ya saa moja. Hata hivyo nilionekana mjanja mitaani.
 
Hahahaha! Umenikumbusha mbali mkuu. Kwa mara ya kwanza kumiliki simu nikauziwa na wahuni wa Temeke hiyo Nokia 3310 second hand, daah ilikuwa full kucharge kila baada ya saa moja. Hata hivyo nilionekana mjanja mitaani.

Hahahaa.. Kipindi kile simu ilikua inabadilishwa "housing" ukiuziwa utadhani mpya
 
umenikumbusha mbali mkuu. nilinunua hiyo motorola C200, nilitesa mtaani kwa kuonekana nina kasimu ka kijanja

Hizi Motorola hazikubamba kweli nazo?
 

Attachments

  • IMG_3104.JPG
    IMG_3104.JPG
    3.6 KB · Views: 620
  • IMG_3105.JPG
    IMG_3105.JPG
    4.6 KB · Views: 611
  • IMG_3106.JPG
    IMG_3106.JPG
    9.7 KB · Views: 276
Nakumbuka nilinunua Nokia 1100 kwa shilingi 110,000 mwaka 2004. Wakati huo zilikuwa zinajulikana kama Nokia za tochi. Hii ilikuwa ni simu ya kwanza kuwa na tochi. Ilikuwa ni simu nzuri ila keypad yake ilikuwa inachakaa haraka sana.
 
Kuna mzee mmoja,jirani yetu.Yeye alikuwa akiplay Ringtone muda wowote kwenye mkusanyiko wa watu,Hata hata akiwa peke yake lazima a play tuu.Basi ukiskia ring,tunasema mzee flan huyo anapita.
 
Uongo dhambi simu yangu ya kwanza kabisa ni nokia3310 nilinunua mwaka2003 Tsh's70,000 napo ilikua ya mchongo ya pili nokia1100 mwaka huo huo mwishoni kwa 95 nayo ya mchongo dah!! Ila nokia siwahami hadi leo nina lumia800 naona poa tu.
 
Back
Top Bottom