Mkuu Chupaku, sio rahisi message na simu kurekodiwa. Kinachoweza kuonenekana kwenye system ni billing list ikionyesha namba ya simu iliyopigwa, muda, rate, na salio. Ni history kwa maana hiyo wala sio actual text au conversation. Ila wakitaka kukurekodi for specific purpose wanaweza kama ilivyo TTCL.
mkuu nani kakuambia sio rahisi maongezi kurakodiwa? kwa taarifa yako maongezi yote huwa yana rekodiwa kwa masaa 24 baada ya hapo yana futwa.kwa upande wa sms hilo sina uelewa nalo.sio rahisi mitandao kutoa siri za mteja kwa kiasi flani cha pesa,wanaweza kutoa data za mteja wao pale linapotokea tatizo na mahakama kuomba kufuatilia nyendo za mtuhumiwa.
Jamani usiseme zipo halafu tukaua ndoa na mahusiano mengi!!! Hili litajeuka kuwa balaa. Kwa hakika matumizi yako ya number ya sim yanarekodiwa, nisichofahamu ni kama pia wanaonyesha ile text uliyotuma yaani yale actual maandishi!!! Vinginevyo kama hii inafanyika basi wengi wafa, hasa wale wadanganyifu areas tofautitofauti!!! But nafikiri kwa teknolojia ya leo kila kitu kinawezekana!!!
Jamani usiseme zipo halafu tukaua ndoa na mahusiano mengi!!!
Kama ilivyo kwa mawasiliano mengine (barua, email etc) yoyote hakuna absolute privacy.
Hakuna siri ya watu wawili! Kama unataka kitu kiwe siri basi ukae nacho mwenyewe tu. Kitendo cha kuwasiliana au kutumia system ambayo kwa namnna fulani ina involve mtu mwingine, siri inakuwa si siri tena.
Mkuu Maane zipo,nami pia nilikuwa mbishi kwa hilo lakini ilitokea kwa rafiki yangu,jamaa yake alikuwa anayanasa mazungumzo yake yote anapopigiwa simu na kutumiwa msg na ulitokea mtafaruku mkubwa sana katika mahusiano yao,ikabidi rafiki yangu a-trace kwa nini kila anayewasiliana nae jamaa anajua na hata akitumiwa msg jamaa anajua,sasa jiulize nini hapo kilikuwa kinaendelea?