Simu yangu iliyofungiwa na TCRA imeanza kufanya kazi leo hii asubuhi

SNAP J

JF-Expert Member
Dec 26, 2013
7,106
8,044
Ni matumani yangu mmeamka salama. Eid Mubarak kwa wale ndugu zangu waislamu.

Leo asubuhi nilipoamka nikashangaa kuona kasimu kangu cha nokia ya tochi cha mchina kalichokuwa kamefungia mwezi wa sita na TCRA kana piga kazi tena kama kawa. Nimeweza kupokea simu , meseji na hata kupiga simu.

Nashindwa kuelewa nini kimetokea, kwani baada ya kufungiwa nilikuwa naitumia kama tochi tu na kusikilizia redio tu.

Au ndio tumepewa ofa ya siku kuu leo na TCRA!!?.Nawasiii wengine mliofungiwa vimeo vyenu mjaribu kuviwasha leo kwani huenda vikawa vimevunguliwa.
 
Unasema tena? We kaushia mkuu si unajua bahati haiji mara mbili
 
TCRA hawafungii simu, wanaofungia ni makampuni ya simu kupitia agizo la TCRA. Unategemea kampuni ya simu itakubali hasara!?
Nilishasema hii kampeni ishafeli kabla ya kuanza.
 
Mitambo yao ya kufunga simu ni mitambo fake. Inafanya kazi kwa muda tu. Si ajabu simu nyingi zitaanza kupumua tena hivi karibuni.

Ni matumani yangu mmeamka salama. Eid Mubarak kwa wale ndugu zangu waislamu.

Leo asubuhi nilipoamka nikashangaa kuona kasimu kangu cha nokia ya tochi cha mchina kalichokuwa kamefungia mwezi wa sita na TCRA kana piga kazi tena kama kawa. Nimeweza kupokea simu , meseji na hata kupiga simu.

Nashindwa kuelewa nini kimetokea, kwani baada ya kufungiwa nilikuwa naitumia kama tochi tu na kusikilizia redio tu.

Au ndio tumepewa ofa ya siku kuu leo na TCRA!!?.Nawasii wengine mliofungiwa vimeo vyenu mjaribu kuviwasha leo kwani huenda vikawa vimevunguliwa.
 
Mimi mwenyewe simu ya mrs waliifunga tukampa dogo akawa anacheza game sababu ni smartphone ina game nzuri juzi tumeweka laini ikasoma fresh laini moja nyingine ikagoma....
 
Isijeikawa uliweka line mpya maana kinachofungiwa ni line na kila ukiweka line tofauti nailiyokuwemo Kabla Wakati inafungiwa itafanyakazi tu
 
hahahaha tanzania ina maajabu kibao
haswa awamu hii kila kitu kinakosewa ............. anzia uteuzi mpaka kufunga simu
 
Isijeikawa uliweka line mpya maana kinachofungiwa ni line na kila ukiweka line tofauti nailiyokuwemo Kabla Wakati inafungiwa itafanyakazi tu
Hapana mkuu sikuweka line mpya.
 
mkuu naomba nikusaidie kidogo.hebu weka imei ya hio sim mara moja hapa jukwaani tucheki kama unachosema ni cha ukweli
 
Back
Top Bottom