Mr Bean.
Senior Member
- Jan 25, 2015
- 185
- 128
Wadau kwa jinsi nionavyo katika hili zoezi la kuzima simu feki, Nahisi lazima kutatokea mkanganyiko wa kiteknolojia. Halihiyo itazifanya hata zile simu zetu tunazoamini ni original kuzimika. Sasa je swali langu hawa watu wa TCRA kwanini hawatoi kabisa mwongozo kwamba ikitokea jambo hili fanya hivi au hivi au wasiliana na huyu nk.Kwamba ndugu mwananchi ikitokea simu yako ambayo unauhakika ni original ikizima!fuata utaratibu huu hapa. Nilitegemea TCRA wangefanya hivyo kwa tahadhari. Maana kwa bongo yetu hii chochote chawezekana. Unaweza shangaa system yao inaziona simu zote nchi nzima ni feki.Nawasilisha.