Sodoku
JF-Expert Member
- Feb 3, 2016
- 1,095
- 2,429
Kumekuwa na matumizi mabaya sana ya simu za mikononi hasa hizi smart phone kwa sasa. Unakuta mke na mume wamerudi kazini jioni baada ya kula wakapanda kitandani kila mtu yupo busy sana simu akichat na kuangalia nini kinaendelea kwenye insta n.k
Kama kawaida linapotokea jambo lolote la maendeleo waathirika wakubwa sana ni sisi waswahili au waafrika. Hatujui muda gani wa kutumia simu na wakati gani wa kutotumia. Si ajabu kwa sasa ukapanga appointment na mtu mkakae sehemu mpige story ukakuta mmeishia kunywa na kula ila muda mwingi wote au mhusika mmoja yupo busy na simu. Akichat, akisonya na wakati mwingine kutabasamu. Jambo hili limesababisha kukosekane upendo kwa kiasi kikubwa.
Kitandani kumekuwa balaa zaidi. Sasa mke au mume anatumia muda huu wa kuwa kitandani kujibu text zote ambazo alitumiwa asubuh na kuangalia kwenye pages za watu mbalimbali nini kimejiri na wakati mwingine ndIo hapo huanza kuchat na michepuko. Ukija kushtuka mtu anakoroma na usiku umeanza mkali. Siku imeisha.
Kuna wale wapuuzi ambao saa nne anakupigia simu anataka kukupa hi tu au wakati mwingine mtu anakupigia simu saa tano usiku unaamka unapokea anakwambia " mwanangu upo? Mbona kimya sana? Nipe story" huu ni ustaarabu mmbovu sana. Mimi binafsi mwisho kumpigia mtu simu ni saa mbili na nusu. Nami ifikapo saa tatu huwa sipokei simu isipokuwa kutoka kwa watu ambao nadhani pengine wana dharula.
Wenzangu lazima tuwe na heshima na ndoa au mahusiano. Simu zina wakati wake, si wakati wote mtu unapiga simu. Unanipigia simu asubuhi saa 12 au saa 1 na huku hauna jambo la maana. This isnt right. Kama tuna utaratibu flan its ok lakini kuna mida mizuri ya kumpigia mtu simu. Subiri weekend au lunch time kwa wafanyakazi. kama una dharura its ok. Ukipiga mara moja hajapokea tuma text. pia si akili kupiga simu mara 3 na kuendelea ikiwa mhusika hapokei.kawaida mara mbili inatosha sana ukiona hapokei unaacha unatuma text.
mida hiyo ya usiku ndo huwa wanaume na wanawake wengine wanajikuta wanaavyochat nawe wanaingia tamaa na kukutamkia maneno au kukuandikia maneno ya kimahaba...maana obvious mhusika anaona upo free sana hivyo utakuwa mpweke. mwenzako anapopata text au kusikia sauti kama hiyo tayari ni ugomv na hatimaye week mbili zilizopita mfanyakazi mwenzangu kamwacha mkewe baada ya kukuta texts nyingi zinazotumwa usiku kumtakia usiku mwema. kumbe mke anachat muda wote jamaa akiomba mke anajibu amechoka sana.jamaa aka conclude basi anayechat naye ndiye humchosha. wakaachana kwa ugomvi mkubwa sana.