giftcharles
Senior Member
- Aug 11, 2015
- 147
- 77
Simu feki zinapingwa duniani koteKila mtu anafahamu kwamba mwezi wa 6 mwaka huu, wametangaza kuzizima simu zote feki Tanzania, imeleta utata sana ukizingatia kwamba asilimia kubwa ya watanzania walikuwa wakizitegemea simu feki.
Kwa zaidi ya miaka kumi dunia ilizikubali hizi simu ziwe kwenye soko, Baada ya kushtuka kwa kiasi gani simu hizi zinaleta hasara kwenye jamii, sehemu nyingi za dunia zinachukua hatua na walioahi walichukua hatua muda mrefu uliopita, kama Kenya walivyofanya matangazo yao mwaka 2012.
Kwa mtazamo wangu mimi, Tanzania imechelewa sana kuamka, Lakini nadhani ni kwa sababu inaeleweka ni kiasi gani watu wanazitegemea simu hizi.Pamoja na kwamba zinakaribiba kupotea, kuna mambo ambayo watu bado hawayaelewi kuhusu simu hizi.
simu feki
Nakupa hapa list ya mambo ambayo inawezekana hauyajui kuhusu simu hizi, nitaacha na links chini ya post hii kwa mtu anayetaka kusoma zaidi kuhusu mifano nitakayoitumia ndani ya post hii, twende basi…
1.Uchafu alioutupa Marekani ndio vifaa vya simu feki kutoka china
Marekani inatengeneza taka nyingi sana zinazotokana na vifaa vya kompyuta na simu mbovu, kwa miaka mingi sana nchi kubwa huwa zinasafirisha taka zao kwenye nchi ambazo zinaendelea, lakini hiyo ilikuwa kabla ya mwaka 1989 baada ya watu kulalalmika, ziliwekwa sheria dhidi ya mambo hayo.
Lakini Marekani haikuacha kutuma taka zake kwenda China, Unaweza ukadhani kwamba China ingeweza kuzikataa, lakini hawafanyi hivyo kwa sababu taka hizo ndizo zinabadilishwa kuwa simu nyingi feki zinazosafilishwa kwenye nchi zetu.
China inamji unaojihusisha na kazi ya kuzipokea taka hizi na kuzifanya ziwe tayari ili kubadilishwa kuwa bidhaa nyingi tofauti tunazoziita feki(sina jina kwa sababu ni limewekwa siri), Kwa muujibu wa “60 minutes” ya BBC1, mji huu hautembelewi na watu wengi, kwa sababu “hewa ya huo mji ni mchafu na maji yake yanasumu“.
simu feki
2. Kulipuka kwa simu feki ni rahisi kuliko unavyoweza dhania
Watu wengi huwa wanasikia hiki kitu na kupuuzia kwa sababu hawasikii kikitokea lakini “simu feki zinalipuka vibaya kama bomu”, maneno hayo alisema Michael Sathre, baada ya kulipukiwa simu yake mkononi mwake mwenyewe.
Kuna ripoti nyingi sana hapa duniani za simu kulipuka, zote zilihusisha betri feki iliyoshindwa kustahimili kazi, Sio utani kupoteza mkono kisa tu ulishindwa kutumia kuongeza hela ili upate orijino.
Hii nadhani ndyo sababu moja ambayo mimi inanifanya nikubali kuzimwa kwa kwa hizi simu feki zote.Unaweza ukasoma zaidi kuhusu simu iliyolipuka hapa www.cbsnews.com/news/exploding-cell-phones-spur-recalls.
3.Kama ulidhani soko la simu feki linatisha Tanzania, nakwambia China ndio linatisha zaidi
Wachina wakiona upenyo wowote wakuingiza hela, hata kama ni kwa kutumia jina la mtu mwingine watautumia, tena kwa kujazana bila aibu yoyote, Hii ilithibitishwa mwaka 2011, Kuna duka la Apple lilifunguliwa ndani ya Shanghai,China likiwa na mwonekano kama wa maduka ya Apple, wahudumu waliovaa kama wahudumu wa kawaida wa apple na bidhaa zao zote zikiwa za apple.
Lakini kinachochekesha ni kwamba duka lile halikuwa na mahusiano yoyote na kampuni ya apple, hakuna bidhaa yao hata moja iliyokuwa ya apple. Watu wanaotumia duka lile kununua simu zao wakiulizwa, wanasema kwamba wao hawajali kama simu zao ni feki au ni orijino, kama zinafanya kazi basi zinafaa kutumika.
Japokuwa duka hilo limevuta macho ya watu duniani kote kiasi cha kuongelea na BBC kwenye habari zao za kimataifa, Apple hajaongea chochote kuhusu duka hilo.
Ukiangalia hiyo video hapo chini ndio utaelewa vizuri zaidi…
(SAMAHANI! ili nisizidishe links video nimeiweka hapa simu feki: Mambo yanayowezekana hauyajui - TzaLive)
4.Fungulia mbwa ya simu feki ilikuwa baada ya China kujiunga na WTO
Kama hauifahamu WTO, ni makubaliano yaliyofanya na mataifa ili kuweza kufanya biashara pamoja bila ya kuwa na matatizo, Kabla ya mwaka 2001, China ilikuwa hairuhusu kampuni za ndani ya nchi yake kufanya biashara na nchi za nje, kwa hiyo bidhaa kama simu feki zilikuwa hazizoki.
Baada ya Kujiunga na WTO, ndipo simu viwanda vingi vidogo vilipoibuka ndani ya china na soko la simu feki lilipoanza kuteka dunia.
5.Dhana ya kwamba zimetengenezwa kwa ajili ya waafrika ni uwongo.
Kuna watu wanaosema kwamba hizi simu zilitengenezwa kwa ajili ya kuwauzia waafrika, Lakini hiyo sio kweli kwa sababu hata nchi kubwa kama marekani inayotumia mitambo ya kisasa kukagua bidhaa, bado inaidadi kubwa tu ya bidhaa feki zinazoingia ndani.
Kwa mtazamo ni rahisi kusema kwamba zimeletwa kwa ajili ya waafrika kwa sababu soko lake kubwa ni la waafrika, Lakini hiyo ni kwa sababu tu ya bei yake rahisi inayowavutia watu wengi wanaishi kwa kipato kidogo.
6.China ndiye msambazaji mkubwa lakini zipo nchi zingine kama Vietnam, South Korea na Thailand
Kila sehemu mada ya simu feki inapoingia, nchi itakayitajwa huwa ni China tu, hiyo ni kwa sababu china ndiye anayesambaza kwa wingi zaidi ukilinganisha na wengine lakini, wapo wengine wanaofanya biashara kwa ukubwa kama China.
Swali la kujiuiza tu hapo ni kwa nini nchi zote hizi zipo ndani ya bara moja, Asia.
Mambo madogo…
7.Simu feki zinachangia asilimia 2-3 ya mzunguko wa fedha hapa duniani.
Zingatia kwamba nimesema duniani, hela inayoongelewa hapo ni kubwa mno.
8.Simu feki zimechangia watu wengi sana kupoteza kazi zao.
Ni rahisi sana kuelewa watu wanapotezaje kazi kwa sababu ya simu feki, baada ya kuja simu hizi, watu wengi sana waliamia kwenye simu feki, kwa sababu ya urahisi wake wa bei, ndio maana marekani nafasi za kazi zaidi ya 700,000 zilipotea kwa sababu ya simu feki.
Mwisho
Kusema kwamba dunia ilipata hasara tupu baada ya kuja hizi simu ni uwongo kwa sababu zimewasaidia watu wengi sana, Kama mimi simu yangu ya kwanza nakumbuka ilikuwa ni mchina uliofeki kati ya feki, zimejitahidi kudumu muda mrefu kwenye nchi nyingi kwa sababu zinakubalika na watu wengi lakini kila mtu alikuwa anajua tayai kwamba lazima kuna siku zitapingwa.
Kama umeipenda hii post unaweza share na majamaa na marafiki kupitia link zilizopo juu na chini ya hii post.
Kama unamaoni unaweza kuniachia kwenye sehemu ya comments hapo chini.
Links
1.Counterfeit electronic components - Wikipedia, the free encyclopedia
2.Exploding Cell Phones Spur Recalls