OK, Kwa sababu umesema unaweza kuafford budget ya simu yoyote hakuna haja ya kuchukua low end na mid range, nakushauri uchukue high end phones i.e flagship phone kati ya hizi, Samsung galaxy S7, Samsung galaxy S7 edge, LG G5, Sony Xperia Z5 kwa simu za android, na kwa upande Apple iPhone 6S au 6S plus au iPhone 7 au 7 plus, ila kwa upande wa simu za Apple nakushauri ununue tu iwapo hujawahi kutumia Android phone, ama ka,a huko nyuma uliwahi kutumia Apple devices vinginevyo kwa simu za mwanzoni utahisi kama upo kifungoni ila ukishazoea hutajutia kamwe.
Ingelikuwa ni mimi nataka kununua simu na nikachagua upande wa simu za Android ningelivuta subira mpaka simu za Google Pixel zitoke I think ni kuanzia tarehe 20 hivi mwezi huu ingawa unaweza pre-order kwa sasa. Sababu zifuatazo zinanisukuma kuwa na simu hii
1. Mi ni mpenzi wa stock Google android experience, mpaka sasa hakuna kampuni yoyote inayotengeneza simu za android iliyonishawishi kwenye UI, zaidi hizi UI zao zimekuwa zikipoteza pure android user experience na kufanya simu kuwa nzito
2. Kuja na Google Assistant, hii AI ya Google kwa kweli ni moto wa kuotea mbali, kwa upande AI kampoteza Apple na siri AI yake, na hii ni msaada mkubwa sana ingawa kibongo bongo haina msaada sana kwa sababu nimekuwa nikiitumia kwenye Allo kuna saa inatoa info zisizo sahihi lakini inajifunza kutoka kwako, hii simu inakuja na pre built Google Assistant
3. Kuwa na mategemeo ya kupata updates bila ukakasi (hapa nazungumzia security patch na new versions of android angalau kwa miaka miwili hadi mitatu hivi), halafu we unakuwa wa kwanza kupata updates
4. Free unlimited photos and video storage, ingawa hapa Google wenyewe hawajaweka itadumu kwa muda gani au itakuwa lifetime, ukiwa na hii simu kamwe hutawahi kulalamika out of storage