Katika hali isiyoeleweka, hali ya hewa ya shirika la mafuta la TPDC imechafuka ghafla mwezi huu baada ya kugawanywa kwa barua 11 za kuwahamisha wataalamu wa shirika hilo bila sababu za msingi na huku barua nyingine 14 zikiwa chini ya meza kupima upepo wa watumishi. Sakata hilo linaratibiwa na mama Simtengu ambaye alihongwa nafasi ya ukurugenzi hivi karibuni. Mama Simtengu amekua akiratibu zoezi hilo nyuma ya meza.
Sakata hilo lilizua tafurani kubwa kwa watumishi na kusababisha utendaji wa shirika kushuka sana baada ya watumishi hao kugundua kuwa ajira zao haziko salama tena. Busara kubwa ya mkurugenzi mkuu mpya ilitumika kuwashusha munkari na kuwaomba watumishi watulie ili aweze kuchunguza mambo yanayoendelea ambayo hata yeye mwenyewe hayajui.
Wadau waliohojiwa kuhusu kashfa hii wameeleza kuwa hali ni mbaya sana kwa mama huyo aliyepatiwa cheo bila kufuata taratibu ambaye ana kashfa nzito kwenye mamlaka ya takukuru kuhusu ukwapuaji wa mamilioni ya pesa za shirika na sasa amemchongea mhasibu mkuu wa shirika kuondolewa kwa vile alishindwa kumlinda kwenye kashfa hiyo. Mhasibu mkuu alifanya kazi yake kisheria na hapaswi kuondolewa kwa kufanya kazi yake ipasavyo kwa vile tu ni hawala wa kigogo.
mmmh! ka kaumbea flani hivi...!
Tuwe wa kweli katika hili mama hana hatia, hana madaraka ya kufanya hivyo.
Watanzania Majungu Hayalipi Tuachane Nayo.
Huku TPDC (Mafuta na Gesi) , Mbona Hapatulii; Inaonekana Kuna Watu Wapo Hapo wao Ni Majungu Kila siku na Walizoea Kubebwa; Ukiona Mtu analalamika sana ohoo, Flani Kaamishwa sijui Kafukuzwa bila sababu ya Msingi ujue atakuwa Mnufaika wa aliyetolewa either direct or indirect.
Watanzania Epukeni Majungu kazini kwa Maana Hayaleti Tija; Kama Mtu Kaamishwa Shida Iko wapi?, Wewe Piga kazi Watakuja wengine watashika Nafasi na Kazi ya Umma Itasonga Mbele.
Mna Bahati Mpo Kazini, ni Jambo la Kumshukru Mungu, kwa Maana wengi Hawana hiyo Bahati. Sasa Basi epuka Majungu Chapeni Kazi ili Shirika Lilete Ufanisi Taifa Lisonge Mbele.
Tabia ya Kuabudu Watu waliowasaidia Kupata kazi badala ya Kuheshimu kazi na Kujituma ni tatizo sugu hapa Tanzania; Ni vema Waajiri wawaelekeze Wafanyakazi ktk ufanisi wa kazi, Badala ya Kukalia Kutamka Neno "Sawa boss" hata pasipostahili.
Mkuu hili shirika lina watu walizoea kubebwa bebwa! Sasa kuna wengine bila kubebwa ni shida tupu! We mtu sijui una vyeti kibao kabatini huwezi kujibeba mwenyewe! What a shame!
Mama wa watu hana hayo mamlaka ya kumwondoa mtu pale, haya ni maamuzi ya juu toka wizarani na wala siyo mama, pale wanaoondolewa ni wale waliokaa mda mrefu shirikani bila kuleta ufanisi! Kazi yao ni kujisifia tuu! Na kupanga namna ya kupiga pesa za umma.
Mbona hajiulizi idara iliyoguswa ni utawala na fedha na mtu mmoja wa legal? Why not upstream department!?
Kilaza mkubwa kabisa mleta uzi.
Fanya kazi, acha siasa bwana mdogo!
Wee kilaza lazima utetee hadi povu likutoke manake huyo ni hawala wa aliyekupa hiyo kazi ya kuja kutetea hapa. huyo mama anahusika sana na liko wazi. Na huyo mhasibu mkuu sio mwizi kwa taarifa yako mwenye kesi ya wizi ni mama simtengu hawala wa bosi wako hapo na alikwapua zaidi ya milioni 120 halafu anataka atetewe na mhasibu mkuu