Katika hali isiyoeleweka, hali ya hewa ya shirika la mafuta la TPDC imechafuka ghafla mwezi huu baada ya kugawanywa kwa barua 11 za kuwahamisha wataalamu wa shirika hilo bila sababu za msingi na huku barua nyingine 14 zikiwa chini ya meza kupima upepo wa watumishi. Sakata hilo linaratibiwa na mama Simtengu ambaye alihongwa nafasi ya ukurugenzi hivi karibuni. Mama Simtengu amekua akiratibu zoezi hilo nyuma ya meza.
Sakata hilo lilizua tafurani kubwa kwa watumishi na kusababisha utendaji wa shirika kushuka sana baada ya watumishi hao kugundua kuwa ajira zao haziko salama tena. Busara kubwa ya mkurugenzi mkuu mpya ilitumika kuwashusha munkari na kuwaomba watumishi watulie ili aweze kuchunguza mambo yanayoendelea ambayo hata yeye mwenyewe hayajui.
Wadau waliohojiwa kuhusu kashfa hii wameeleza kuwa hali ni mbaya sana kwa mama huyo aliyepatiwa cheo bila kufuata taratibu ambaye ana kashfa nzito kwenye mamlaka ya takukuru kuhusu ukwapuaji wa mamilioni ya pesa za shirika na sasa amemchongea mhasibu mkuu wa shirika kuondolewa kwa vile alishindwa kumlinda kwenye kashfa hiyo. Mhasibu mkuu alifanya kazi yake kisheria na hapaswi kuondolewa kwa kufanya kazi yake ipasavyo kwa vile tu ni hawala wa kigogo.