Ni kweli Hilo halipingiki, Hata mimi kuna mtu ambaye nilimpenda nikapenda na Kupitiliza Na hata Alipokuja kuachana na Mimi nilijitahidi kumsahau lakini mpaka leo ingawa nina maisha yangu na nimekuwa na mahusiano Kadhaa lakini moyo Wangu Bado unaishi ndani yake
Mie napenda ninapopendwa tu, nisipopendwa nami naigiza vilevile.
Mie napenda ninapopendwa tu, nisipopendwa nami naigiza vilevile.
Sasa wewe unatumia moyo gani kusukuma damu kama wako unaishi kwa mwingine?
Hahaha,nljifunza upendo na principle zake through bible kwamba love is patience,is kind,conquers all,love never end matokeo yake full uvictim,I wish ningejua love is a game mapema sana
Unaishi ndani yake kwa Upendo na Uthamini wake kwEnye hisia Zake, Lakini kwenye Kusukuma damu unanisaidia mwenyewe
Naye alikupenda vivyo hivyo?
Mamiii inakuwa hivyo kama umempata mtu sahihi anayekupenda pia hivyo hivyo au zaidi, na ni raha asikuambie mtu, yaani utaiona dunia yote yako, ila ukimpata popoma ndio utalia na kusaga meno.
nadhani haikuwa hivyo ndio maana leo hayuko nami.. Lakini amecheza sehemu kubwa sana katika maisha yangu
Poyeeeee!! Usijali atakuja atakayeifuta hiyo taswira yake yoooote.
Habari zenu wana jamii
Nimekuwa na kijana mmoja tumekuwa na mauhusiano kwa mwaka mmoja ila tukaachana kutokana na mwenzangu kuonekana anampenda ex wake zaid yangu.Wakati tupo katika mahusiano nkagundua bado anachat na ex wake na ex akimstress hasira zote ni kwangu.Kiukweli iliniuma sana na ilibid tuachane tu niokoe nafsi yangu.kuachana kuliniuma sana maana nilimpenda sana.kwakweli maisha nliona machungu.nilikonda sana stress sana hata kazi nikaacha.
Kinachoniumiza ni huyu mwanaume kutwa haachi kunitafuta nikitulia ananifata na kuappologise.Mm nimemsamehe japo bado kiukweli nina uchungu sana kwa magumu aliyonifanyia na kuniona sina maana.but shida yangu ni kuwa sitaki mawasiliano nae wala ukaribu nae maana nkiwasiliana nae najiskia kumpenda tu na ninatamani kurudiana nae ila yy hayupo tayar kurudiana nami anataka urafiki wa kawaida na mm siwezi.je wanadau nakosea kutaka kukata mawasiliano nae??
Saiz anakuja niwe karibu nae tena coz nimesikia mambo sio mazuri kwake na huyo mpnz wake.kiukweli icho kitendo mi kinantia hasira sana na kufanya nizidi kumchukia maana naona anaiona kama second option..nimfanye nn anitoke for good??staki mawasiliano nae wala ukaribu nae ili ni move on.
QUEENBM Tatizo jamaa anajua huwa anakufikisha kule amabapo hakuna mwingine amewahi kukufikisha huko. Dawa ni kumpata mwingine atakae kufikisha huko. Mtihani ni utampataje? Maana kama jamaa level yake ni juu sana itabidi ujaribu watu tofauti tofauti na hapo ndio utaharibikiwa kabisaaa.
Usahuri: ngoja ukomae kwanza usikimbilie hii michezo ya kikubwa utaumia!