Simpendi, ila naogopa kumwacha

youngsharo

JF-Expert Member
Jan 8, 2015
2,491
500
Habarini ndugu wanajukwaa,

Kama mjuavyo katika mapenzi mda mwingine mwanaume unaweza kuweka mahusiano na mwanamke kwa ajili ya kupunguza stress, nilikuwa namkumbuka sana mchumba wangu ambaye yupo mkoa na tayari nimemtambulisha nyumbani, lakini kutokana na kuwa alikuwa yuko mbali hivyo kuonana nae mara kwa mara inakuwa shida, mara nyingine tunaonana mara 1 kwa mwezi, mara nyingi tunaishia kuchart kwenye simu.

Kwa hapa ninapoishi Nikapata rafiki wa kike ambaye tulijuana na tukazoeana kama marafiki, lakini kadri siku zilivyoenda tulijikuta siku moja tumepeana kile chakula ambacho huwa kinaliwa kwa siri, tangu tugegedane nilianza kumchukia na kujilaumu mimi mwenyewe kwanini nilikubali kulala nae, kwani nilikuwa sitaki hata siku moja nimsaliti mchumba wangu.

Ila huyu niliyemgegeda kusema kweli ananipenda kupindukia na alishaniambia lazima atahakikisha amezaa na mimi, kumbe kweli alikuwa amedhamiria sasa kwa bahati mbaya nimeshamtia mimba.

Akili yangu ya mwanzo kabisa ilinituma kuwa nikisha enjoy nae mara moja basi nisimfatilie tena, kilichokuja kunichanganya ni hiyo mimba niliyomuweka na kikubwa zaidi na kuniogopesha ni kauli zake, ameniambia "nikija kumsaliti(kumwacha) yeye ataandika kinotice kisha atajiua", hapo ndo amekuja kunitia wendawazimu. Nimwache ajiue kwa ajili yangu?

Ebu please wewe kama rafiki yangu naomba unishauri nifanyeje? Kwa sababu mchumba wangu siwezi kumwacha ilihali nampenda na nimeshamtambulisha nyumbani, na huyu nae naogopa kumwacha kutokana na kauli zake anaweza kujiua kweli, alafu kingine sitaki nyumbani wajue kwamba nina mwanamke mwingine nimemtia mimba tofauti na yule mchumba wangu.

Ushauri wako ni muhimu kwangu.
 
Mmmhh Una uhakika Ana mimba?? Umejuaje n yako?? Maji yameshamwagika fanyeni muongee Tu vizur muelewane ila naona kama changa la macho hili unapewa
 
Toroka tu na uhame mji kwani hakuna namna, Vita vikikushinda ni kutimua mbio maana hakuna namna wala jinsi:(o_O:rolleyes:
 
Mmmhh Una uhakika Ana mimba?? Umejuaje n yako?? Maji yameshamwagika fanyeni muongee Tu vizur muelewane ila naona kama changa la macho hili unapewa
Uhakika kama ni mimba yangu kwa kweli sina, lakini ndo kashasema sasa.
 
Kama ulijua ni kwa mda kwa nini hukutumia condom?????na HIV ushapima?????
Itakula kwa Huyo bidada kwani ataishia kuwa single mom,,
 
Back
Top Bottom