Simon Msuva azitosa mazima Simba na Yanga

TAJIRI MKUU WA MATAJIRI

JF-Expert Member
Dec 1, 2010
5,720
10,220
Simon  Msuva Azitosa Mazima Simba na Yanga

Hatimaye nyota wa kimatifa wa Tanzania aliyekuwa akikipiga katika Klabu ya JS Kabylie ya nchini Algeria, Simon Msuva, amefunguka suala la kuhusishwa kujiunga na klabu za Simba SC na Young Africans.

Kwa sasa Msuva hana timu baada ya kuachana na Klabu ya JS Kabylie ya Algeria ambayo alijiunga nayo Desemba 19, 2023, akitokea Al-Qadsiah ya Saudi Arabia, ambayo ilimsajili tangu Julai 24, 2022 akitokea Wydad AC ya Morocco.

Hivi karibuni kumekuwa na taarifa kuwa Young Africans imekuwa ikifanya mchakato wa kumtaka kumsajili Msuva kwa mkataba mfupi ili awasaidie kwenye michuano ya kimataifa.

Msuva ameweka wazi kuwa, baada ya kuachana na JS Kabylie kwa maelewano ya pande mbili, sasa haangalii nyuma na hana mpango wa kucheza Tanzania.

Ameongeza siku si nyingi atatoa taarifa za nchỉ gani ataenda na hana mpango wa kurejea nyumbani kucheza iwe Young Africans au Simba SC, anachoangalia kwa sasa ni kujikita kwenye soka la kulipwa kutokana na ukubwa wa wasifu yake na muda ukifika basi atarejea Tanzania kumalizia soka lake.

Kwa sasa naweza kuweka wazi kabisa kuwa maisha ya Algeria yameshapita kwani nimemalizana nao vizuri tu kwa maana ya pande zote mbili tumekubaliana, ila nafahamu wazi kabisa kuwa kwa sasa kila mtu ataongea lake ila mimi najua nini nafanya. Si unajua Tanzania yetu.

Ninachoweza kusema nina CV kubwa hivyo siwezi kukosa timu kwa uwezo wa Mungu nitapata tu na nitakwambia mapema tu wapi naelekea ila siwezi kurudi kucheza nyumbani mapema hii,” amesema Msuva.
 
Ila wabongo !! Kwakuwa tu kasema hawezi cheza Yanga kwa sasa mmeanza kumnanga et kachakaa ,kaisha. Ila angesema anakuja Yanga sasa hivi ingekuwa ni kumsifia na kumshushia umri kwamba ana miaka 21.
Wabongo ni sawa na hadithi ya shairi la Sungura na ndizi SIZITAKI MBICHI HIZI
 
Ila wabongo !! Kwakuwa tu kasema hawezi cheza Yanga kwa sasa mmeanza kumnanga et kachakaa ,kaisha. Ila angesema anakuja Yanga sasa hivi ingekuwa ni kumsifia na kumshushia umri kwamba ana miaka 21.
Amesema hawezi kucheza Yanga wala 5imba, inakuwaje unawaandama wana Yanga tu? Mbona wana Yanga kibao wameonyesha hawamtaki toka tetesi za kwamba anaweza kusajiliwa Yanga zianze? Nenda page zote za Yanga mitandaoni then cheki reaction zao kuhusu Msuva
 
waliozungumziwa wanataka kumsajili ni yanga, tena kijarida chenu cha mwanaspoti kiliandika kabisa ameshasajili . Sasa Simba inaingiaje hapo au story yako isingenoga bila kuitaja Simba.
 
Ila wabongo !! Kwakuwa tu kasema hawezi cheza Yanga kwa sasa mmeanza kumnanga et kachakaa ,kaisha. Ila angesema anakuja Yanga sasa hivi ingekuwa ni kumsifia na kumshushia umri kwamba ana miaka 21.
Tangu mwanzo kabla hajahusishwa na kusajiliwa yanga nilisema msuva ameshafika peak na ameanza ku decline ukiangalia performance yake stars.
Ni kweli alikuwa mchezaji wa Kiwango cha juu lakini ugomvi wake na wydad na kukaa nje muda mrefu kulimuadhiri pakubwa huenda angekuwa tayari anacheza klabu kubwa ulaya.
Msuva ni mtu wa kujituma na ni aina ya Mpira wa ulaya unavyochezwa lakini sijui Kama ataweza kurudi Kiwango chake cha zamani .
 
Jamaa anajiona bado keki kumbe andazi 😀😀😀 Hata kucheza Yanga ingekuwa bahati kwake. Mpira Tanzania umekua
 
Simon Msuva Azitosa Mazima Simba na Yanga

Hatimaye nyota wa kimatifa wa Tanzania aliyekuwa akikipiga katika Klabu ya JS Kabylie ya nchini Algeria, Simon Msuva, amefunguka suala la kuhusishwa kujiunga na klabu za Simba SC na Young Africans.

Kwa sasa Msuva hana timu baada ya kuachana na Klabu ya JS Kabylie ya Algeria ambayo alijiunga nayo Desemba 19, 2023, akitokea Al-Qadsiah ya Saudi Arabia, ambayo ilimsajili tangu Julai 24, 2022 akitokea Wydad AC ya Morocco.

Hivi karibuni kumekuwa na taarifa kuwa Young Africans imekuwa ikifanya mchakato wa kumtaka kumsajili Msuva kwa mkataba mfupi ili awasaidie kwenye michuano ya kimataifa.

Msuva ameweka wazi kuwa, baada ya kuachana na JS Kabylie kwa maelewano ya pande mbili, sasa haangalii nyuma na hana mpango wa kucheza Tanzania.

Ameongeza siku si nyingi atatoa taarifa za nchỉ gani ataenda na hana mpango wa kurejea nyumbani kucheza iwe Young Africans au Simba SC, anachoangalia kwa sasa ni kujikita kwenye soka la kulipwa kutokana na ukubwa wa wasifu yake na muda ukifika basi atarejea Tanzania kumalizia soka lake.

Kwa sasa naweza kuweka wazi kabisa kuwa maisha ya Algeria yameshapita kwani nimemalizana nao vizuri tu kwa maana ya pande zote mbili tumekubaliana, ila nafahamu wazi kabisa kuwa kwa sasa kila mtu ataongea lake ila mimi najua nini nafanya. Si unajua Tanzania yetu.

Ninachoweza kusema nina CV kubwa hivyo siwezi kukosa timu kwa uwezo wa Mungu nitapata tu na nitakwambia mapema tu wapi naelekea ila siwezi kurudi kucheza nyumbani mapema hii,” amesema Msuva.
Kwahiyo Tanzania kuna soka la ridhaa?
 
Sizitaki mbichi hizi!!. Asijidanganye!! soka lake linaporomoka!!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom