Mwanantogakulya
Senior Member
- Mar 18, 2025
- 130
- 118
Kamati ya Siasa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Simiyu imeeleza kutoridhishwa na kasi ya ujenzi wa Chuo cha Ufundi Stadi (VETA) kinachojengwa katika Wilaya ya Busega kwa gharama ya Sh 1.48 bilioni kwa awamu ya kwanza.
Kamati hiyo imeeleza kuwa licha ya fedha hizo kutolewa na serikali kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, maendeleo ya mradi huo yanasuasua, hali inayotia shaka kuhusu usimamizi na utekelezaji wake.
Akizungumza wakati wa ziara ya kukagua maendeleo ya mradi huo,Mkuu wa mkoa wa Simiyu,Kenan Kihongosi ambaye ni mjumbe wa kamati hiyo amesema kuwa ni muhimu kwa wahusika kuongeza kasi ili kuhakikisha kuwa chuo hicho kinakamilika kwa wakati na kuanza kutoa mafunzo kwa vijana wa wilaya hiyo.
Amesema kuwa Mradi huo wa ujenzi wa VETA, una changamoto kubwa katika utekelezaji wake, lakini ofisi ya Mkuu wa wilaya ya Busega pamoja na Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya hiyo wamekuwa wakichukua hatua mbalimbali ikiwemo kuwakumbusha kwa maandishi juu ya utekelezaji wake na umuhimu wa mradi huo lakini bado kuna shida kidogo.
"Wizara wanapoleta hii miradi, wajue kuna viongozi kama Mkuu wa Wilaya na Mkurugenzi wa halmashauri kwenye eneo husika wanaopaswa kujua utekelezaji wake ili waguswe zaidi na miradi hii,kwa sababu, hapa leo tunaulizana gharama ya jengo, hakuna anayejua zaidi ya wizara"
''Hii ni changamoto, kama fedha zimeletwa zaidi ya Sh 429 milioni lakini bado majengo hayajakamilika, Wizara ya Elimu wana wajibu wa kufanya, hapa sisi kama mkoa hatujaridhika na huu mradi." amesema Kihongosi.
Amesema kuwa changamoto zote zinazojitokeza ikiwemo nondo kuoza, zinaweza kusababisha majengo kubomoka na kuitaka Wizara ya Elimu kuhakikisha wanasaidia chuo hicho kukamilika kwa wakati kwani serikali imeshatoa fedha, hivyo wanachotakiwa ni kutimiza wajibu ili majengo hayo yakamilike kwa wakati.
Naye Katibu wa CCM mkoa huo, Eva Ndegeleki amesema kuwa mradi huo unasuasua licha ya kuwa ni muhimu kwa ajili ya watoto ambao watajifunza utaalamu na ujuzi mbalimbali ili wajikimu na waendeleze maisha yao na Taifa kwa ujumla.
Hivyo amemtaka Mkuu wa mkoa huo kushirikiana chama hicho ili waweze kuwasiliana na wizara ya elimu kwa ajili ya ukamilishaji wa mradi huo, ili ifikapo mwezi juni mwaka huu wananchi wawe na matumaini na waone ukikamilika la wakati.
Awali, akiwasilisha taarifa ya ujenzi wa mradi huo, Afisa Uthibiti Ubora wa Shule wilaya ya Busega, William Thomas amesema lengo la mradi huo ni kupata wataalamu watakaosaidia nchi baada ya kuhitimu mafunzo ya vyuo, kuwajengea vijana ujuzi na uwezo wa kujiajiri pamoja kupunguza tatizo la ajira nchini.
Ameeleza kuwa ujenzi wa chuo hicho ukikamilika utakuwa na majengo 18 ambapo awamu ya kwanza itahusisha majengo tisa na awamu ya pili majengo tisa na kwamba mradi huo unatekelezwa kwa Force Account kwa gharama ya Sh 1.48 bilioni kwa awamu ya kwanza na hadi sasa sh 429 milioni zimepolewa.
"Jengo la utawala limefikia asilima 50, madarasa yako asilima 50, kuna changamoto ya ukosefu wa nondo kwa ajili ya kufunga lenta, nguzo za kunyanyua majengo ya karakana na mbao hazijaletwa ili kuendelea na upauaji wa majengo sita" amesema.