Simiyu; CHADEMA itaisurubu CCM

Simiyu; CHADEMA itaisurubu CCM

Prince Tumbo

JF-Expert Member
Joined
Apr 5, 2013
Posts
910
Reaction score
247
Nimefanya shughuli zangu mkoa mpya wa simiyu kwa miaka 7 sasa. Awali CCM na UDP vilikuwa ni vyama vilivyokuwa vinapendwa sana na wananchi. Hali hii ilibadilika katika uchaguzi wa 2010 ambapo wananchi walianza kuipenda CHADEMA licha ya kwamba, majimbo ya Bariadi Mahariki na magharibi hayakuwa na wagombea wa CHADEMA katika ngazi ya majimbo. kampeni zilizofanywa na wagombea wa ngazi ya udiwani katika baadhi ya maenea ndio ziliowatoa watu usingizini na kuanza kuiona Tanzania mpya inakuja kupitia CHADEMA.

Nimetembelea maeneo ya Sapiwi,Nkololo,Nkoma,Ngulyati, Nanga na Migato (moja ya maeneo wtu wengi vijijini) vijana kwa wazee wanaipenda CHADEMA, hii imetokana na watu kukosa matumaini na CCM na UDP kupoteza ushawishi na mwelekeo kisiasa baada kuendelea kuwa masikini na hasa bei ya pamba kuendelea kushuka.

Ninaona yapo mapungufu makubwa

1. Halijawahi kupita vuguvugu la madiliko-M4C

2. Hajaonekana kiongozi mkubwa wa CHADEMA walao kufanya mikutano kadhaa kati ya maeneo hayo muhim hapo juu

3. Vijana walio na moyo wa kulikomboa taifa ambalo kwa sasa limeharibiwa na viongozi wasio wazalendo (CCM) hawana support na maelekezo ya karibu kutoka kwenye chama

4. Kutokuwapo na ofisi za CHADEMA kwenye mashina jambo ambalo ni muhimu sana.

Kwa utafiti wangu through observation, si CCM wala UDP hawana chao kuelekea 2015
Viva CHADEMA, Viva makamanda..:rockon:

Nawasilisha

Source; mimi mwenyewe
 
viongozi kina makene na wengine hpoe watasimamia M4C iwafikia wana simiyu.Hivi mzee wa vijisenti anaendeleaje
 
Ni ripoti nzuri. viongozi na crue nzima ya CDM bila kujali nafasi uliyonayo katika chama nawalio ndani na jirani ya Simiyu hili lifanyiwe kazi.
 
Mkuu bado lakini M4C inakuja huko wakae mkaa wa kula kama Dr Slaa alivyotangaza mwaka jana kuwa mwaka huu ni mwaka wa maandalizi ya kuingia Ikulu,Hakuna kulala mpaka kieleweke.Peoples Power
 
Back
Top Bottom